Saturday 2 April 2016


Nilikuwa nikiperuziperuzi kwenye kurasa mbalimbali za kwenye mitandao, nikisoma iki na kile. Ghafla nikakamatika na habaari yenye kichwa kisemacho:

"BAKWATA WATOA MSAADA WA MADAWATI 500 KWA SERIKALI"

Kabla zijasoma habari yenyewe akili yangu ikawa ikitafakari kwa haraka sana kuhusiana na habari ile. Nikajiuliza maswali ya haraka haraka, BAKWATA hii hii au nyingine, BAKWATA hii ambayo shule zake zenyewe zimeshindwa kuendelea vema miaka na miaka, BAKWATWA hii hii ambayo inashindwa hata kuwa na mfuko wa kukusanya zakkah, BAKWATA hii hii ambayo Waislam hawana iymani nayo leo hii ndio imeweza kutoa msaada serikaliili hali inashindwa kuwasaidia Waislam kwenye mambo mbalimbali ya msingi, leo hii imeweza kutoa msaada serikalini, hii habari ni ya kweli au...!

Nilipoamua kuisoma habari yenyewe ndio nikakutana na jambo lingine ambalo ndio limenifanya niandike makala hii.
"BARAZA Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wamekabidhi msaada wa madawati 500 kwa serikali ili kusaidia upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari."

Hii habari ukisoma juujuu tunaweza sema kuwa ni jambo zuri la kusaidia jamii yako bila ya kujali iymaani zao, kama alivyonukuliwa
Mufti na Sheikh Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Abubakar Bin Zuberi kuwa "...BAKWATA hawaangalii suala la dini kinachoangaliwa ni watakaolia madawati hayo ni watanzania."

Baadae nikaja kugundua kuwa kumbe wamewezeshwa na jumuiya ya Kishia nchini Tanzania na wala si mfuko wao wenyewe BAKWATA. Kwa sababu shule zao BAKWATA wenyewe ziko hoi bin taaban vipi leo waweze kusaidia serikali wakaziacha shule zao zikikosa vitendea kazi yakiwemo hayo madawati.

Na Mwenyekiti wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka kuweza kuchangia madawati 1000.

Habari hii ya madawati ni moja ya harakati nyingi za Mashia kujipenyeza kwenye mioyo ya Watanzania na kuweza kupata mapenzi kwao ili hiwe rahisi kwao kuweza kupata wafuasi. Na ili wameanza kufanikiwa kwa kasi kubwa sana, uku Waislam wengine tumekalia marumbano ambayo hayana tija kwenye ulimwengu wa Kiislam uku tunawasahau vijana na watoto wa Kiislam wakipotea.

Shia wanajipenyeza kwa haraka sana uko Vijijini na haswa Pwani na yale maeneo yenye Waislam wengi. Na si shia tu, kuna Ahmadiyah nao wameshika kasi sana mikoani haswa uko Rufiji, Mikoa ya Lindi, Morogoro, Mtwara na maeneo kadhaa na wamewekeza nguvu zao vijijini ambako Waislam sisi hatuna habari nako.

Kama vile haitoshi, kila kukicha tunangalia kuongezeka kwa Wasio Waislam na Taasisi zao katika kujizolea ardhi hasa maeneo ya pwani na uchukuaji wao wa ardhi kubwa kubwa  katika maeneo yenye Waislam wengi.

Nikikumbuka maneno ya Walimu wa Madrassa Juu ya kuporomoka kwa ufundishaji wa Qur’an hasa vijijini kunakochangiwa na hali zao mbaya za Uchumi.

Nikifikiria juhudi tuzifanyazo sisi "Waislam tunao jiona Wasomi na Wafanyabiashara" kwenye swala zima zima la kuendeleza Uislam na Waislam, michango yetu ya mawazo kwenye mambo ya msingi yaani nachoka kabisa.

Tumekuwa mahodari sana kwenye uchambuzi wa mambo ya kisiasa, umadhehebu na kunyoosheana vidole wakati wenzetu wakifanya mambo kwa vitendo.

Waislamu yahitaji kuzinduka. Tuziache ikhtilafu zetu ndogo ndogo kuwa ndiyo sababu ya kutugawa na kudhoofisha umoja wetu. Kama kulikuwa na wakati ambao Waislamu walihitaji umoja na mshikamano basi huu ndio wakati wenyewe.

Waislamu tembeeni uko mikoani na vijijini ili muone hali halisi ya Waislam na Uislam kwa ujmla hakika tutakuja ulizwa siku ya hisabu.

kumbuka juu ya ayah hii:
"Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema" 102-At-Takathur : 8

2 comments:

  1. Billahi alaikum ya kusemwa ni mengi Sana Na haya yote Kwenye makala hii yasikitisha. Waislamu haswa massuni ambao ndio wako katika Njia ya sawa wamejisahau Na majukumu yao. Wameshughulika Na kurundisha Mali Na kusahau kuzitumia kwa njia ya Keri.

    Mashia Na maahmadiya wakizitumia kwa Njia ya Keri tunachomwa mioyo. Tuzinduke Kama wasunni Na tufanye yaliokuwa jukumu letu.tumebakia Na kushtumu Na vitendo hakuna. Wenzetu wana vitendo Vikubwa Na dini hawana wala imani.
    Angalia vile wanavyotoa scholarship kwa wanaopenda Elimu kwenda Kusoma dini baatil ambao ndio wanaipandikiza ilhali sisi tukipata nafasi Kama hayo tunafanya ubakhili Na khiyana. Wanasaidia panapofaa Na kwa wakati munasib.sisi tutabakia nyuma Na vita visivyokuwa Na Maana Na lawama Za kishenzi tu.

    Waliojitokeza kukemea haya pia bila Shaka watapigwa vita Na sisi wenyewe masunni. Kwani mkijua kuwa Mara zote daawah ya haqqi ikilala daima daawah ya baatil huchukua ushukani. hakuna shaka JUU ya uhalali wa aqeeda yetu ya kisunni wala majukumu yalio JUU yetu Ki daawah. Swala ni Je , TUTALALA MPAKA LINI? NA TUTAMJIBU NINI ALLAH JUU YA AYA HIYO?

    ReplyDelete
  2. Billahi alaikum ya kusemwa ni mengi Sana Na haya yote Kwenye makala hii yasikitisha. Waislamu haswa massuni ambao ndio wako katika Njia ya sawa wamejisahau Na majukumu yao. Wameshughulika Na kurundisha Mali Na kusahau kuzitumia kwa njia ya Keri.

    Mashia Na maahmadiya wakizitumia kwa Njia ya Keri tunachomwa mioyo. Tuzinduke Kama wasunni Na tufanye yaliokuwa jukumu letu.tumebakia Na kushtumu Na vitendo hakuna. Wenzetu wana vitendo Vikubwa Na dini hawana wala imani.
    Angalia vile wanavyotoa scholarship kwa wanaopenda Elimu kwenda Kusoma dini baatil ambao ndio wanaipandikiza ilhali sisi tukipata nafasi Kama hayo tunafanya ubakhili Na khiyana. Wanasaidia panapofaa Na kwa wakati munasib.sisi tutabakia nyuma Na vita visivyokuwa Na Maana Na lawama Za kishenzi tu.

    Waliojitokeza kukemea haya pia bila Shaka watapigwa vita Na sisi wenyewe masunni. Kwani mkijua kuwa Mara zote daawah ya haqqi ikilala daima daawah ya baatil huchukua ushukani. hakuna shaka JUU ya uhalali wa aqeeda yetu ya kisunni wala majukumu yalio JUU yetu Ki daawah. Swala ni Je , TUTALALA MPAKA LINI? NA TUTAMJIBU NINI ALLAH JUU YA AYA HIYO?

    ReplyDelete

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!