Sunday 13 November 2016


Kuna Mzee apata miaka 70 ambaye ana watoto watano wakubwa wenye kujitegemea na uwezo wa kifedha.

Siku moja yule mzee aliamua kuipeleka simu yake ya mkononi kwa fundi kujuwa kama simu yake ni nzima au mbovu.

Fundi wa simu baada ya kuichunguza akagundua kuwa simu haina tatizo lolote lile, akamrudishia yule mzee simu yake na kumwambia kuwa simu yake ni nzima na hakuna malipo yoyote anayotakiwa kulipa.

Yule mzee akamuuliza swali ambalo yule fundi simu akuweza kulijibu.

Mzee wa watu alimuuliza fundi simu hivi:

"Kama simu ni nzima na haina tatizo lolote lile, mbona Watoto wangu hawanipigii simu!?"

Unaweza kuona kuwa ni kisa kisicho na maana yoyote ile lakini hiki ni kisa ambacho kimetokea na kinawatokea wazee wengi wa zama hizi za ubize, zama ambazo kila mtu anakwenda mbio na dunia kiasi cha kusahau wajibu wa kuwatunza na kuwaangalia wazee ambao ndio pepo na mafanikio yao kwa maisha ya baadae.

Kama unaye mzazi/wazazi wako tafadhali kama yupo karibu nawe waweza tu kumkumbatia na kumwambia neno moja tu kuwa unampenda, kama yupo mbali na uwezo unao wa kwenda kumtembelea basi fanya hima ukamtembelee mzazi wako na kama yupo mbali basi mpigie japo simu na kumjulia hali mzazi wako.

Hiyo ni Nasaha yangu kwa mwenye kujali, si lazima uikubali...!

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!