Sunday 16 December 2018

KATIKA HILI NAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Wengi wetu/baadhi yetu tutakuwa aidha tumesoma au kusikia tu kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya (European Union) limepitisha maazimio kadhaa dhidi ya serikali ya Tanzania.

Maazimio hayo yana masharti mengi magumu, yakiwemo haki za ushoga (Hapa wengi wanashindwa kuelewa, unaposikia haki za mashoga hapo wana manisha si kutambuliwa uwepo wao tu, lah hasha bali kuwapatia uhuru wa kujitangaza, kuhamasisha wengine kujitokeza adharani na kujianika wazi na hata haki za kindoa za kuoana (Gay pride). 

Maazimio mengine ni kutetereka kwa haki za binadamu na kuminywa kwa demokrasia...

Binafsi namuunga mkono rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na kuyapinga maazimio hayo ambayo kwa uwazi kabisa yameletwa kutokana na misimamo ya Rais ya kulinda rasilimali za Tanzania.

Kizaa zaa cha chuki na nia ya kulipiziwa kisasi kilianzia pale alipotoa amri ya kuzuiya mchanga wa dhahabu (makinikia) na kudhibiti Tanzanite. Vibaraka wachache walijitokeza na kuwaunga mkono wakoloni mambo leo, lakini kwa msimamo thabiti wa Rais wa nchi akisaidia na baraza lake la Mawaziri, walisimama kidete na kukataa waziwazi kuburuzwa na kuuza utu wetu kwa mabepari ambao kila kukicha wanatafuta mbinu mpya za kutubana ili wajichotee maliasili za Tanzania kwa ulahisi, uku wakitutaka kwa nguvu kuachana na mila na desturi zetu.

Tanzania ni nchi huru, yenye mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake yenyewe kama zilivyo huru nchi za ulaya na kujiamulia mambo yao wenyewe. Ustarabu wa ulaya si lazima uwe wa Afrika hususani Tanzania...

Mtuache tupumue

#RaisWanguNchiYangu
#NamuungaMkonoMagufuli
#RaisWanguMagufuli

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!