Saturday 24 December 2016


Assalamu Alaiykum

Kwenye Group hizi za WhatsApp, kumezuka magroup mengi ya Waislamu, ambao wana maradhi ya kimaadili ya kupenda simulizi za NGONO (paraphilia - Mwenye kupenda ngono), na kwa kupenda kwao zinaa na kwa kutaka kukubalika kwenye macho ya memba wa group wamezipa group zao kwa majina kadhaa mazuri yakiwemo group za ndoa n.k.

Maradhi haya ya wendawazimu wa parafilia ni maradhi ya kimaadili na yameanza kuingia kwa kasi zaidi katika jamii yetu, na haswa bada ya teknolojia ya simu kuwezesha watu kutumiana picha na meseji za aina mbali mbali.

Ugonjwa huu wa kupenda simulizi za NGONO (paraphilia) unaongezeka sana tena kwa haraka mno kiasi cha kushangaza, wamefikia sasa kuwa na group zilizofichika kwa anuani mbalimbali na wakitumia neno NDOA nakadhalika.

Tunao watu wengi waliozama hapa, na iko haja ya kupambana na maradhi haya, na hakuna anayeweza kupambana nayo bali sisi wenyewe Waislamu.

Wenye maradhi haya huwezi kuwakuta wanachungulia madirishani au sehemu nyingine, kwa sababu wanaweza kushikwa na kuchomwa moto. Kuna mbinu mpya za kukidhi haja ya wenye maradhi haya.

Wengi wao uogopa kuweka filamu au video za ngono kwenye simu zao, ila walicho kigundua sasa ni kusimuliana hatua kwa hatua jinsi jimai inavyo fanyika, tena bila ya kuficha kitu, kwa kufanya hivyo wanakuwa tayari washa sisimua ile hali ya kujisikia faraja ya kingono kwenye bongo zao na kujiona kuwa wamejifariji kama vile wale wanao angalia video za ngono.

Lakini hoja kubwa na zinazopendwa ni NGONO na yanayo husiana na hayo ndio maana kuna jitokeza wahuni kwa sababu group tayari limekosa hishma ya kuitwa group la Waislamu.

Kama watu wanaweza kuelezea jinsi ya kungonoana na Admin wakanyamaza kimya inaonyesha ni jinsi gani wengi walivyo wagonjwa wa simulizi za ngono kwa visingizio vya kufundishana au kuboresha ndoa.

Mfano mwingine wale wanaume na wanawake wenye maradhi haya ni wale wanaoshabikia na kutetea kwa hoja kuwa wanajifunza ili kuborosha ndoa zao na wale ambo hawapo kwenye ndoa ujitetea kuwa wanajifunza ili wakiingia kwenye ndoa basi wasiwe wageni wa hayo mambo.

Kuna wagonjwa wengine ambao sio mahututi sana, awa ni wale ambao, zikiletwa hizi simulizi uzisoma na kuzipenda, kisha ukaa kimya kama vile awakuzisoma na hata kukitokea malumbano, wao uwa kimya tu. Na ikitokea kuwa Admin wa group kupendelea ziwepo basi wao upata faraja na zikikataliwa wanaugua kimyakimya.

Wendawazi hawa ndio chanzo cha matukio mengi ya zinaa na hata ubakaji, kwani wanaume wengine hushindwa kuendelea kuvumilia hali hii na matokeo yake ni kuwafata au kufatwa memba wa jinsia tofauti kwenye inbox zao.

Tunategemea Jamii ya Kiislamu kusalimika na maradhi haya kwa kusisitiza stara kwa wanawake na wanaume, kwa kuacha mambo hayo ambayo upelekea kwenye zinaa. 

Haya hayawahi kutokea si enzi ya Mtume (salla Allahu 'alayhi wa-sallam) wala maswahaba zake, wakawafundisha vijana jinsi ya kuyaendea mambo kwa kuwakusanya.

Lakini tunajuwa kuwa hata uko majumbani kwetu, ni pale tu vijana wanapofikia umri wa kuoa na wanatarajiwa kuingia kwenye ndoa ndipo hapo upewa mafunzo na humo hakuna ruhusa kuingia ambaye hajapata kuwemo kwenye ndoa.

Lakini leo hii kila mtu hujitia unyakanga na ukungwi wa kuelezea mambo ya unyumba bila ya kuzingatia adabu na hishma ya hayo mambo.

Jukumu kubwa sana mnabeba Admin wote wa haya magroup ya ndoa na hata yale ambayo yanapendelea simulizi hizi, na kila mtu atakae ingia kwenye kuyatenda basi nyie pia mtagawana kwa watakayoyapata, hiwe kwa kheri au kwa shari sababu yamefundishwa kwenye uangalizi wenu.

Na masheikh wetu awa wakina Gugo Ibn Intanetii Bin Midia Bin Wasab ibn Fasibuk, wanacho kijuwa wao ni kutukanana na kukashifiana Kiitikadi na Kimadhehebu uku vijana wa Kiislam wanaangamia kwa kukosa masheikh wa kuwafundisha mambo ya msingi ya dini yao.

Kwa ujumla, jamii kufuata Uislamu ni kusalimika na kila janga la ulimwengu huu, hasa yale yanayosababishwa na sisi wenyewe kwa matendo yetu. Hivyo janga la ili vile vile litaondoka kwa kufuata maadili ya Kiislamu.

Maamrisho ya Mwenyezi Mungu yasemayo: 
Wala msiikurubie zinaa hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya kabisa.
Qur'an 17:32

Wala msiukaribie uzinzi, kwa kuziingilia sababu zinazo pelekea uzinzi. Jambo hilo ni jambo la aibu na uovu usio fichikana, na hapana njia mbovu kama hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!