Thursday, 14 May 2015

Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

Kwenye jamii zetu, kuna maradhi mbalimbali yanayosumbua siha zetu, kuna huu ugonjwa ambao sina jina rasmi la kuupa, lakini unashambulia sana bongo zetu haswa sisi Waislam.

Ugonjwa huu wa akili uja katika hali tofauti tofauti kulingana na mweuko wa muhusika mwenyewe. Kuna ambao wapo kwenye mashindano ya kifikra, hapa ndipo inazaliwa hali ya watu kutaka kujikweza. Kukosa au kukataa fikra zao kunakuwa kama ni fedheha, na wanakuweka kwenye kundi la hufai na kwanini huwi kama wao.

Maana katika ugonjwa huu ambao uwapata wale wenye akili usababisha kujikweza, kujiona bora zaidi kuliko wengine, na kwamba wao ndio wanaostahili kusema, kukejeri, kutukana wengine, na kila mwenye kukataa fikra zao basi huyo ni mwenye kushutumiwa na hafai katika jamii ya wenye Akili kama wao.

Wenye akili awa upelekea mpaka watu kujiona kuwa pepo ya Mwenyezi Mungu ni yao na funguo za pepo zote wamekabidhiwa wao. Na wao ndio wanaostahili kuwa mabwana, na wengine wote wawe watwana. Kiasi cha kujuwa nani wa kumuingiza peponi na nani wa kumwingiza motoni.

Kuna makundi katika iymaan ya Kiislam, haya makundi yalishatabiliwa uwepo wake, na haya makundi ni katika jitahada za hao walikuwepo nyuma katika kufutu maswala ya kiiymaan na katika fiqh, tatizo linakuja kwa hao wafuasi wa hayo makundi, badala ya kufuata mwenendo mwema wa hao wanao wafuata,

wao wamejikuta wanaathirika na huu ugojwa wa kuwa na akili nyingi wenye kushambulia milango ya ufahamu na kiasi cha kutokuwa na hikma wala busara za kimazungumzo, Akili zao upanda na kujiona wao ni malaika  kiasi kumfanya mwelevu huyu kujikweza na kujiona kuwa ana haki ya kila jambo na kuwapa watu kile ambacho yeye anaona kinastahili kwa muda ule.

Mara nyingi maulamaa awa wenye akili uwa wanashadidia mambo kiasi cha kujisahahu kuwa wao ni Waislam na hao wanaowashadidia ni Waislam na wanastaili hishma na staa kama wanavyo stahiki wao.

Jamii hii yenye akili huwa ina maradhi ya kiakili yaitwayo Prejudice, maradhi ya kuwaona wengine si kitu katika lolote lile na kuwa na chuki bila sababu, wakati mwingine fikra zao uwapelekea kuwaona makafiri ni bora kuliko yule anayepingana na hayo maradhi ya akili... Na hata wakileta jambo la uwongo basi hapana mtu yoyote anayestahiri kulikosoa, maana katika akili zao na maradhi walionayo wanajiona kuwa wao ndio mwisho wa fikra na hakuna ambaye anastahili kukosoa au kuzungumza kuhusiana na jambo walilolileta. Na hawastahili hishma wala hadhi kama walio nayo wao...!

Wenye akili awa wamefanikiwa sana katika kueneza chuki miongoni mwa jamii za Kiislam kiasi cha kuwafanya wawe mbilikimo wa kifikra (intellectual dwarf), wamefanikiwa kuwagawa Waislam katika makundi, kiasi ya kukosa tena ule upendo wa Kiislam katika jamii, ukiwa ukubaliani nao basi wewe ni msaliti, aidha ukubali kujinasibisha na moja ya makundi yao au ukubali wakutusi na kukukejeri na kukuita majina yote mabaya wanayo yajuwa wao.

Wamekuwa vipofu kiasi ya kwamba wanashindwa kusoma hata ayah za Qur'an...!

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.
Qur'an Surat Al I'mran [3]103

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!