Thursday 3 December 2015


Walicho Kitaka Wanakifanya Sasa

Na vita hii ni lazima ifanyike kwa namna yoyote ile hata kwa kuwatoa muhanga raiya zao wachache, ili waweze kutimiza malengo yao.

Nchi za KIGAIDI (NATO) zikiongozwa na UK na kwa upande wa pili wakishirikiana na USA, kwa kupitia bunge la Uingereza, zimeadhimia kuiangamiza ISIS lakini haswa lengo lao si ISIS kwa sababu ISIS ni mtoto wao wenyewe walio mzaa na kumpatia mafunzo yote yanayotakiwa, ili kuwawezesha wazazi wake kuendelea kuiba rasilimali za Mashariki ya kati.

Nchi hizi zenye kujivunia technolojia mbalimbali haswa za kivita, watakuja na ngonjera nyingi sana, ili kuishawish dunia kuwa wao watakuwa makini sana na watawalenga tu ISIS. Kitu ambacho hakita wezekana katu, kwa sbabu lengo haswa ni kuharibu miundo mbinu yote ya nchi ya Syria na kuhakikisha kuwa raiya wa Syria wanakuwa hawana huduma zote za kijamii na kuirudisha nyuma mika 2000 na zaidi.

Niliwahi kuandika makala moja kuwahusu ISIS na malengo yao, wachache wasio jitambua wakaona kuwa si kweli lakini sasa kile nilichokiandika awali ndio kinaanza kuchipua na kinamea kwa haraka sana na punde jiti lenye majinamizi litakuwa kubwa na mizizi yake yenye sumu kali itatambaa Mashariki ya kati yote na baadhi ya nchi za Afrika.

Na nchi zote ambazo zitapinga uvamizi huu,kama hazitashawishika kisiasa basi zijiandae kuripuliwa na ISIS ili kuwashawishi kinguvu, kwa kuonyeshwa kivitendo kuwa ISIS awana mapenzi na yoyote na watamripua yoyote Yule na hapo ndio nchi husika zitakapo unga mkono mashambulizi na hata kupeleka majeshi kuwasaidia wavamizi hao.

Nchi za NATO na Amerika (USA) na serikali zao hazina mapenzi yoyote na nchi zenye rasilimali haswa mafuta, na pale nchi zikitaka kuwa tofauti nao kimaslahi basi watawazalishia maadui na kujinasibisha na akida wanazo zitaka wao kisha watawapa promotion kubwa ili dunia iwatambue kuwa ni wabaya. Kisha baada ya hapo ndio utaona wakipanga milipuko kwenye nchi zao na kuuwa watu wawili watatu, na matangazo ya saa 24 hewani kuonyesha kuwa maharamia hao ni kutoka nchi fulani na ni kikundi fulani cha kigahidi.

Kitakacho fuata kila mtu anajuwa ni kupeleka maangamizi kwa raiya wasio na hatia wa nchi husika. Tutashuhudia mauwaji mengi sana na dunia haitanyanyua mdomo kwa sababu zinazo julikana tayari.
Wale wote wenye kufuatilia siasa za kimagharibi wanatambua kuwa, nchi za Uingereza, Amerika, Ufaransa na nchi zote za NATO, ndizo zenye kuwafadhili kwa hali na mali hao ISIS.

Hizi Nchi angamizi baada ya kuanzisha itikadi potofu (ideology) za kigahidi na kuzinasibisha na Uislam, na uku wakijuwa kabisa kuwa si kweli, wakaifanyia matangazo (Promotion) kiasi ambacho wananchi wao wakaingiwa na hofu kubwa na kujazwa chuki kiasi cha kuwachukia Waislamu na Uislam kwa ujumla. Baada ya kuwashibisha sumu raiya zao ndio tukaona uharibu mkubwa wa nchi za Iraq, Afghanistan, Libya na sasa Syria.

Raiya wengi wa nchi za kimagharibi si walewa na si watu wenye kufuatilia vitu kwa kina sana, wengi wao utegemea habari zao kutoka kwenye television na magazeti na haswa yale yenye ushawishi na kufadhiriwa na serikali zao.

Raiya wenye kupinga umwagaji damu huu ni wale ambao kwa namna moja au nyingine waliwahi kuathirika na vita hivi aidha wao wenyewe au ndugu zao. Au wale ambao waliwahi kutembelea baadhi ya nchi za Mashariki ya kati na kukirimiwa vizuri na Waislam wa nchi hizo. Wananchi awa ndio wanaofanya kampeni za kupinga umwagaji damu haswa vita dhidi ya Ugahidi kwa sababu wameshagundua kuwa si kweli kinachoelezwa kwenye vyombo vya habari.

Raiya hao wachache wenye kujitambua, wanajuwa kabisa kuwa matukio mengi ya Kigaidi ni matukio yaliyopangwa na nchi zao wenyewe na zikiongozwa na kuratibiwa na nchi ya Marekani.
ISIS wapo hapo wakiwakilisha uhalali wa nchi za kimagharibi ili wawape sababu za kuvamia nchi za Kiislam kwa kisingizio cha kuwatafuta ISIS.

Mnapaswa kujuwa kuwa hizi nchi haziwezi kuishi bila ya kuwa na adui atakayewapa sababu ya kuendelea kuchukuwa rasilimali za nchi wanazozitaka.

Ugaidi huu unaofanyika nchi za mashariki ya kati na nch za ulaya ni biashara na kazi ya mikono ya hayo mataifa kwa malengo yao maalum.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!