Tuesday, 16 June 2015


Mke wa pili! Ni maneno yaliyorindima na kutoa mwangwi katika kichwa changu. Nilimuuliza: “Kwa nini? Je mie sio mrembo? Abadan! Kamwe sitakubali suala la mke wa pili. Kama unataka mke wa pili waweza kwenda kumchukua lakini utambue kuwa ukirudi hutanikuta hapa!” 

Hayo yalikuwa maneno yangu niliyomwambia mume wangu miaka kadhaa iliyopita aliponitamkia kuwa anakusudia kuoa mke wa pili. Alinieleza kuwa ni mwanamke ambaye alikuwa ameachika muda si mrefu na alikuwa na watoto 4. Yuko katika wakati mgumu na hajui mahali anapoweza kupata chakula au hana uhakika wa kuwahudumia wanaye. 

"Baba yao yu wapi?" Nilimuliza. "Huyo baba hawezi kuwatunza wanaye? Kwa nini wewe mtu wa mbali ubebe mzigo wa mwanaume mwingine? Kuna njia nyingine za kumsaidia kiuchumi bila kulazimika kumuoa! 

Nilikuwa sipati picha kuwa katika ndoa ya wake wengi. Kuchangia mume na mwanamke mwingine; kuchangia penzi lake, tabasamu lake, utani wake na mwanamke mwingine. Nilikuwa sipati picha nikiwaza kuwa mume wangu atakuwa akimkumbatia na kumnong'oneza maneno matamu ya mahaba. 

Ni jambo ambalo kwangu halikubaliki. Nilikasirika na kusema: "nimemfanyia mangapi? Hana hata shukrani? Nimekuwa mkewe, daktari wake na mlezi wa nyumba yake. 

Nimemzalia watoto 3 wazuri. Ni kama tusi dhidi yangu kwenda kuoa mwanamke mwingine. Kwani mimi si mrembo? Kwani mimi sina nguvu?" 

HAPANA! Sikuweza kulikubali hilo kabisa na niliweka wazi msimamo wangu. Huyo mwanamke akiingia, basi mie nitaondoka! Sikutaka kuzunguka mbuyu katika msimamo wangu. Akitaka kuihatarisha ndoa yetu, maisha yetu, na watoto wetu kwa sababu ya mwanamke mwingine, basi aendelee na mpango wake huo. 

Sitamzuia! 

Sasa inaonekana miaka mingi imepita. Nilidhani kuwa maisha yatadumu milele na kwamba hakuna kitakachobadilika. Lakini yalibadilika... 

Mume wangu hakuoa mke wa pili. Baada ya maonyo na vitisho vyangu aliachana na wazo hilo. Sijui kilichompata mwanamke yule na watoto wake. Nahisi walihamia mji mwingine. 

Mume wangu hakuthubutu tena kuzungumzia mke wa pili, na hilo lilinifurahisha. Niliweza kumzuia mume wangu lakini sikujua kuwa muda ulikuwa ukikimbia.

Kauli yake ya mwisho aliniambia kuwa anahisi maumivu ya kichwa na anaenda kujipumzisha mpaka wakati wa swala ya 'Isha. Usiku huo hakuweza kuswali 'Isha kwa sababu hakuamka tena. 

Nilichanganyikiwa mno kwa kifo hicho cha ghafla. Ndani ya sekunde nimenyang'anywa mume niliyeishi naye. Niliomboleza kwa muda mrefu kifo cha mume wangu kipenzi. Punde nilianza kuondokewa na kitu kimoja baada ya kingine. Kwanza gari, duka na kisha nyumba. 

Tulihamia kwa kaka yangu aliyekuwa na familia. Mimi pamoja na wanangu 3 tulisongamana katika nyumba yake. Punde wifi yangu akaanza kukereka kwa uwepo wetu. Nilihitaji kutoka, kufanya kazi na kutafuta sehemu yetu wenyewe badala ya kuishi kwa kula masazo ya watu wengine. Lakini sikuwa na stadi na utaalamu. 

Mume wangu alipokuwa hai tuliishi kwa raha mustarehe. Sikuhitaji kwenda nje na kujipatia utaalamu. Maisha yakaniwea magumu mimi na wanangu. Sikuwa kijana tena, umri ulikuwa umenibadilisha. Kila mara nilimkumbuka na kila moyo unapodunda. Mambo yanawezaje kubadilika namna hii? 

Siku moja kakangu aliniambia kuna mtu anayejuana naye anatafuta mke. Ni mtu mzuri, mwenye akhlaq nzuri na mwenendo mzuri sana. Ananifaa, lakini anataka niwe mke wa pili. 

Ni mara ya pili katika maisha yangu ninatajiwa neno hilo la MKE WA PILI lakini katika mazingira tofauti. 

Alikuja nyumbani kwa kakangu. Tulionana moja kwa moja. Nilimpenda na nilipenda kila kitu kuhusu yeye. Aliniambia kuwa mkewe wa kwanza anajua kuwa anataka kuoa mke mwingine lakini anaonekana wazi kuwa haungi mkono wazo hilo na kwamba hajui atajibu nini atakapomweleza kuwa amepata mtu. 

Akasema kuwa jibu lake litategemea iwapo mkewe atashawishika na hoja ya ndoa ya matala. 

Usiku huo nilianza kuswali Istikhara. Pia nilikuwa nikiomba kwa shauku jambo hilo lifanikiwe. 

Nilikumbuka miaka mingi iliyopita pindi maisha ya mwanamke mwengine yalipotegemea uamuzi wangu na jinsi uamuzi huo ulivyokuwa. Niliumia sana. Nilihisi kuwa kwa sababu sikumpa mwanamke mwenzangu nafasi katika maisha yangu basi ni zamu yangu kuadhibiwa na Allah. 

Nilijuta na kutubu. Wakati wa uhai wa mume wangu dhamiri haikunisukuma kutubu kwa nilichokuwa nimemfanyia mwanamke mwenzangu, kwa sababu akili yangu ilikuwa ikiniambia kuwa sina kosa kwa dhana kuwa nilikuwa nikilinda mali yangu. Sasa nikiwa katika hali hii nilitambua ukubwa wa kosa nililolifanya kwa kumkatalia mwanamke mwenzangu fursa ya kuwa na mume. Niliomba sana mwanamke huyu akubali. 

Siku kadhaa baadaye alinipigia simu kunitaarifu kuwa mkewe alikuwa na wakati mgumu kulikubali lakini anataka kuonana nami. 

Nilikuwa na jakamoyo juu ya siku hiyo ya kukutana naye. Siku moja kabla nilisali sana na kumuomba Allah anisaidie. Nilipokutana naye alikuwa kama mimi. 

Alikuwa mwanamke anayempenda mumewe na anayekhofu kumpoteza. 

Aliushika mkono wangu na kuniambia huku machozi yakijaa machoni mwake: "Hili ni jambo zito sana kwangu, lakini ninatumai tunaweza kuwa ndugu". 

Maneno yake yaliupasua moyo wangu. 

Kitu pekee nilichohitaji katika nyakati hizo ngumu ni mkono wenye huruma utakaonipokea na kunikumbatia, mkono utakaonipa tumaini na nguvu ya kusonga mbele. Kwangu mimi, mkewe alikuwa mwanamke wa kipekee na daima nitaendelea kuwa mwenye shukrani kwa hilo. Nilidhani kuwa hakuna mwanamke anayempenda mumewe kama nilivyompenda mume wangu, lakini alinifundisha maana ya upendo wa dhati (unconditional love). 

Huwezi kuijua hali ya mtu mpaka ikufike. Toa uamuzi sahihi kwa mujibu wa Qur'an utaona namna Allah subhanahu wa ta'ala atakavyokumiminka baraka mara dufu.

Leo kidogo, nilikuwa nimejipumzisha ndani ya chumba changu, nilichopanga uku kwa walalahoi wenzangu. Kausingizi kakanipitia kwa mbaaali! Kama unavyojuwa jinsi usingizi ulivyo mtamu kuliko kulala.

Mara nikashtushwa na mazungumzo nje ya dirisha langu. Nikawa najiuliza kuna nini na nini kinazungumzwa? Nikatega sikio, EEh! Kumbe wapangaji wenzangu walikuwa wakimzungumzia mmoja wa wapangaji ambaye amehamia hivi karibuni, akiwa yeye na mkewe.

Nikamsikia mdada mmoja akisema: Mmmh! Menzangu, umemuona huyo mumewe, alivyo kibushuti, sasa sijui uwa anambeba au...! Maana wakitembea kama vile anampeleka mwanawe shule ya vidudu!

Akamalizia na kicheko: Eeeeee! Cheko lako ilooo jilani!

Akadakia na mwenzake: Na huyo mke mwenyewe umemuona jinsi alivyo, yaani kama sanamu la michelini, loh! Hivi dawa zote hizo za kuondoa unene hazioni, yaani akitembea ardhi yote inatetemeka, loh! Mwanamke shepu babu eeh!

Sikuweza tena kuwavumilia, nikanyanyuka zangu, nikatoka na kuwakemea kuwa wanachokifanya sicho. Walicho nijibu, ilibidi nirudi ndani nitafakari zaidi, maana siwezi hata kukiandika hapa.

Kufika ndani mawazo yakawa yananipitia nikawa najiuliza, hivi Nani amewaambia kuwa ndani ya ndoa kuna Mashindano ya Miss wedi, Hivi kwenye ndoa kuna rifarii au jaji. Si ni wana ndoa wenyewe jinsi walivyochaguwana?

Kama mtu anaonekana kuwa kachagua ''kituko" Si mumuwache na kituko chake! Kwa sababu yeye ndio anayejuwa kwanini kachagua kile Kituko na kinamfaa kuwa Mke/Mume.

Wengi wetu tunafikiria kuwa Mke/Mume ni Muonekano wa nje au maumbile. Wanawake wengi wanafikiria mume kuwa na sijui siksi paki au kuwa na bonge la msuri ndio kapatia.

Na hata wanaume Wengi wanafikiria kuwa Mke kuwa na Makalio makubwa au nyonga nyembamba au mapaja manene ndio kupatia, sasa sijui nani kawaambia kuwa makalio au nyonga ndio yanaendesha ndoa.

Kwa taarifa yenu  hayo yote hayaendeshi ndoa, ndoa ni maelewano kati ya watu wawili. Nyie wengine hayawahusu.

Na nyie Wanawake mnaoshangaa Mwanamke anapoamua kuolewa na 'sura mbaya' na kuanza kumsimanga Shosti nae ndo nini kuolewa na mtu mfupi kama kama kashata. Nasema mkome kabisa na hizo tabia zenu tena Muache. Mwenyewe anajuwa Kashata yake kama ataitengenezea Kahawa au ataila hivi hivi na ndoa itakuwa tamu na maisha yataendelea.

Nyie Wanawake nyie, mwenye akili huwa hawachagui Misuli na siksi paki wala sura nzuri, wanachagua mtu mwenye mapenzi ya kweli na mwenye kujali, anaweza kuwa maskini lakini ndani ya moyo wake kuna Utajiri wa mapenzi ambao nyie manungaembe na magube-gube hamuwezi kuyaona ila yeye ameuona na anajifaidia ile roho inapenda.

Nyie kaeni hapo hapo tu mkisubiri mahandisamu boi ambao kazi kuvaa serawili chini ya matako na wanawake ambao kazi kila kukicha kwenye kioo.


Niliingia nyumbani nikamkuta mke wangu akiniandalia chakula cha usiku. Nilimshika mkonoa na kumwambia: “Nina jambo ninalotaka kukueleza.

 Alikaa na kunisikiliza kwa makini. Dalili za wasiwasi nilikuwa nikizishuhudia machoni mwake.

Ghafla nilijikuta katika hali ya kushindwa kukifungua kinywa changu. Lakini ilikuwa ni lazima ajue ninachokifikiria, hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa upole: “Ninataka tuachane.” Hakuonekana kuudhika kwa hoja niliyokuwa nimeiwasilisha mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa: “Kwa nini?”
Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo alighadhibika sana na kuniambia kwa sauti ya juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule hatukusemeshana, na muda wote alikuwa akilia. Nilitambua kuwa alitaka kujua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu lenye kuridhisha; kwa sababu sikuwa na mapenzi naye tena, moyo wangu ulikuwa umetekwa na binti mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!

Huku nikiwa na hisia za hatia moyoni mwangu, niliandika pendekezo la talaka ambalo lilieleza kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya asilimia 30 ya kampuni yangu. Aliitazama karatasi hiyo kisha akaichana na kuitupa kwenye ndoo ya takataka.

Mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa muda wa miaka kumi alikuwa amegeuka kuwa kama mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba radhi kwa kumpotezea muda, rasilimali na nguvu zake lakini sikuweza kutengua kauli yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli ndani ya huba lake na kuwa teja wa penzi lake. Hatimaye alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo nilikuwa nikitarajia kuliona. Kilio chake kwangu kilikuwa kama faraja. Wazo la talaka lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi kupata nguvu na sasa lilionekana kuwa wazi kabisa.

Siku iliyofuata nilirudi nyumbani nikiwa nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika kitu mezani. Sikutaka kula chochote zaidi ya kuelekea moja kwa moja kitandani kwa sababu nilikuwa nimechoka sana kutokana na mishemishe za siku hiyo nikiwa na Jane. Niliposhtuka, bado alikuwa hajatoka mezani. Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea kuuchapa usingizi.

Asubuhi alinipatia masharti ya talaka: hakutaka mali yoyote kutoka kwangu, bali alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja kabla ya talaka. Alitaka kwamba katika kipindi hicho tujaribu kuishi kama kawaida kwa kadiri iwezekanavyo. Hoja yake ilikuwa wazi: mtoto wetu alitarajia kufanya mitihani ya shule ndani ya mwezi huo na hakutaka tumchanganye kwa tukio la talaka.

Hili nililikubali. Lakini alikuwa na nyongeza: alinitaka nikumbuke siku ya ndoa yetu nilipomnyanyua kumpeleka chumbani kwetu. Alitaka kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mzima niwe nambeba kila siku asubuhi kumtoa chumbani mpaka mbele ya mlango wa nje ya nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa ameshikwa na wendawazimu. Nilikubali ombi lake kwa sababu niliona kuwa mwezi mmoja sio kitu, kwani nilitaka tuachane.

Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya talaka yaliyotolewa na mke wangu. Alicheka sana na kuona kuwa ni upuuzi.
“Hata akitumia hila gani lazima apewe talaka,” alisema Jane kwa masihara. Tangu nilipoelezea nia yangu ya kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano wa kimwili na mke wangu. Hivyo nilipombeba siku ya kwanza, sote tulionekana kutokuwa na uchangamfu.

Mtoto wetu alifurahi na kupiga makofi: “Baba amembeba mama”. Kauli yake ilinipa maumivu moyoni. Kutoka chumbani mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea mita kumi nikiwa nimembeba mikononi mwangu. Aliyafumba macho yake na kuniambia kwa upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu kama tunaachana.”

Nilikubali kwa kutikisha kicha huku nikiwa nimefadhaika. Nilipofika nje nilimshusha akaenda kituoni kusubiri basi, nami nikachukua gari langu na kwenda ofisini nikiwa peke yangu.

Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali yoyote ya mifarakano. Aliegemea kifuani kwangu nikahisi manukato mazuri ya blauzi yake. Nilibaini kuwa sikuwa nimemtazama vizuri mke wangu kwa muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza kuwa na mikunjo na nywele zake zilikuwa zimeanza kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa niliduwaa na kuwaza kile nilichokuwa nimemfanyia.

Siku ya nne nilipombeba nilihisi aina ya ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni mwanamke aliyekuwa amenipa miaka kumi ya uhai na maisha yake. Siku ya tano na ya sita, kwa mara nyingine, niliona hali ya ukaribu na mvuto fulani ikirejea kati yetu. Sikumsimulia Jane kuhusu hali hii. Kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo nilivyozidi wepesi wa kumbeba. Yumkini ilisababishwa na ile hali ya kumbeba kila siku kiasi cha kumuona kuwa ni mwepesi.

Asubuhi moja alikuwa akichagua nguo ya kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa lakini hakupata inayomfaa. Alishusha pumzi na kusema: “Nguo zangu zote hazinienei, zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa amekonda na ndiyo maana niliweza kumbeba kwa urahisi. Nilisikitika kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo nilimsogelea na kukipapasa kichwa chake.

Ni wakati huo ambapo mtoto wetu aliingia na kusema: “Baba sasa ni muda wa kumbeba mama”. Tukio la kumuona baba yake akiwa amembeba mama yake lilimuathiri na kuwa sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke wangu alimuita na kumkumbatia kwa upendo. Niligeuza uso wangu pembeni, sikutaka kuangalia tukio hilo nisinje nikabadilisha uamuzi wangu wa talaka. Nilimnyanyua na kumbeba mke wangu, nikatembea kutoka chumbani, sebuleni mpaka nje. 
Aliizungusha mikono yake mizuri shingoni kwangu, nami nikamshikilia vizuri; ilikuwa kana kwamba ni siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili wake ulinifanya niwe mwenye huzuni.

Siku ya mwisho nilipombeba niliingiwa na uzito wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu tayari alikuwa shule. Nilimshikilia vizuri na kusema: “Sikuwa nimejua kuwa maisha yetu yamekosa mvuto”. Niliwasha gari kuelekea ofisini, niliamua kupita kwa Jane. Nilipofika nilitoka haraka bila hata kuubana mlango wa gari. Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia yangu… nikapandisha ngazi. Jane alipofungua mlango nilimwambia: “Samahani Jane, sitaki kuachana na mke wangu”.

Alinitazama kwa mshtuko na kunigusa kwenye paji la uso. “Una homa?” alisema. Niliutoa mkono wake na kumwambia: “Samahani Jane, sitaki kumuacha mke wangu. Yawezekana maisha yangu na mke wangu yalikosa uchangamfu kwa sababu hatukuwa karibu, sio kwa sababu hatukupendana. Sasa nimebaini kwamba kwa kuwa nilimbeba siku ya ndoa yetu, ninapaswa kuendelea kufanya hivyo mpaka kifo kitutengenishe.” Jane alionekana kushtuka sana. Alinizaba kibao, akaubamiza mlango na kuanza kulia.

Nilimuacha nikapanda gari na kuondoka. Njiani nilipita kwenye duka la maua nikaagiza shada la maua kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu ya kadi nikatabasamu na kumwambia aandike: “Kila siku asubuhi nitakubeba mpaka kifo kitakapotutenganisha”.

Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua mkononi, tabasamu usoni, nikapandisha ngazi mpaka ndani. Nilipofika chumbani mke wangu alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Alikuwa akipambana na KANSA kwa miezi kadhaa lakini sikujua kwa sababu nilikuwa nimetekwa na Jane. Alijua kwamba muda si mrefu atafariki dunia na alitaka kuniokoa dhidi ya radiamali yoyote mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama tungeachana. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana kuwa mume mwenye upendo…!

Kumthamini mwenzako ndilo jambo muhimu katika uhusiano. Sio majumba, gari, pesa katika akaunti yako ya benki. Vitu hivyo hutengeneza mazingira ya furaha lakini vyenyewe haviwezi kuleta furaha.

Hivyo, tafuta muda wa kuwa rafiki wa mwenza wako na fanyianeni vitu ambavyo hujenga ukaribu na mvuto.

Ndugu zangu Waislam, nachukuwa nafasi hii kuwakumbusha na kuikumbusha nafsi yangu, kumcha Allah na kuwacha yale yote tuliokatazwa na Mwenyezi Mungu, na haswa tabia ya kuwafanyia wengine Hasadi.

HASADI ni maradhi ambayo yameenea sana katika nyoyo zetu sisi Waislam, kiasi cha kuondoa mapenzi miongoni mwetu.

Hasadi ni jambo baya sana likimvaa mtu, hasadi ni ugonjwa wa kujitakia, maradhi haya ya hasadi, uenea kwa haraka sana kwenye mwili wa binadamu kama vile kirusi cha HIV kinavyoweza kuenea kwenye mwili wa muhathirika, kiasi cha kuharibu ubongo wake na afya ya mwili na akili yake.

Sisi wanadamu ndivyo baadhi yetu tunaishi tukiogelea kwenye bahari ya hasadi na chuki zilizopindukia mipaka. Wapo wenye kuweweseka na aidha ilmu, uwezo, furaha au utajiri wa mtu Fulani, wakati mwingine hata wajihi na mwonekano wa Fulani utaka wao ndio waupate au kustaiki wao.

Pia wapo wenye kuona vibaya jinsi mahusiano au masikilizano kati ya mtu na mtu wangestahiki wao, kwa kuwa tu Fulani anapendwa na wengi au kusikilizwa na wengi kwa ilmu au hikma zake, wakatamani hayo yote wapewe wao na mtu huyo anyimwe rehma hizo kwa kuwa tu anamchukia.

Hasadi ni mbaya, na mwenye hasadi hatazamii jema kwa mwenzie, ila ufurahi kuona mwenzie akiharibikiwa, na utamani kuona mwezie adharauliwe, hasusiwe na kama maradhi yake ndio hayo, basi haridhiki mpaka ahakikishe anafukiwa kaburini tena isitoshe si hasha akatamani nafsini mwake ahadhibiwe hata kama alikuwa mtu mwema, bali yeye ampendi tu, wapo watu wa namna hii.

Uchukia kila zuri la asiyempenda, daima huwa anawaza lini atapata nafasi asimuone adui wake akiwa na furaha. Mtu wa namna hii hata sehemu anapofanyiakazi uwa hana raha na anaweza kuharibu kazi ya watu pale anapoona hasimu wake akifanikiwa au kupandishwa cheo.

Hata humu mitandaoni, utawaona wakikesha kusoma habari za mahasidi wao, ili kuona nini ameandika, ili ajitengenezee uadui, akikosoe kile kilicho andikwa hata kama ni kweli au atukane tu, kwa kufanya hivyo anafikiria kuwa anamkomoa hasimu wake huyo kumbe ndio anazidi kujiangamiza katika kaburi la kisaikolojia, kiasi mtu huyu hukosa raha nafsini mwake, japokuwa mbele za watu hujifanya ni mwenye furaha na mafanikio tele, kumbe moyoni yu ateketea kwa chuki na hasadi zake.

Hasadi hizi ufanywa na wanaume na wanawake dhidi ya wenzao, lakini la ajabu wengine uwafanyia hata ndugu zao wa toka nitoke, uwarambazia uwadui huo.

Kwanini mtu aumwe kwa jambo ambalo hata mwezio akilipata halikupunguzii au kukuzidishia chochote katika maisha yako? Hiwe kapata cheo nawe upendi, kapata elimu, wewe upendi, anapendwa na watu wewe upendi, akisaidia watu wewe upendi, kila jema analofanya wewe upendi.
Kiasi cha kumwendea mafichoni na kumfanyia uhasidi kwa watu na yawezekana ukafika mpaka kwa wachawi na kutafuta kumroga ili ahribikiwe.
Hasidi hajui kuwa hayo yote ni majaaliwa yake Mola, umpa amtakaye, umnyanyua amtakaye, mimi na wewe hatuna uwezo wa kumteremsha au kumpandisha yoyote hapa duniani.

Kwanini tusiangalie nafsi zetu kwanza, kabla ya kurusha vijembe kwa wengine, maana tabia hizi za hasadi uzeesha mtu kiasi cha kuonekana mzee kabla ya umri wake, sababu wewe kila ukimuona au ukiona kile unacho kfanyia hasadi, unakunja sura kama matuta ya viazi, vipi usizeeke kabla ya wakati wako, ili hali hasadi imekujaa kila mahala!?

Hasidi hawezi juwa kuwa kila anapofanya hasadi zake, yule anayefanyiwa hasadi ndio anazidi kufanikiwa, ukimsema vibaya mtu kwa hasadi zako, MwenyeziMungu mtu huyo umjaza mapenzi kwa watu, na uzidi kupendwa na jamii, na mwisho wa hasidi huyu ni kuwa dhalili, mgonjwa na ukonda si kwa maumbile bali analika kwa chuki na hasadi na choyo zake, na kama ni unene basi si wa siha au maradhi au ukoo bali ni kwa safura zinazotokana na hasadi zako.

Kwa wenye maradhi haya ya hasadi basi huu ni wakati wa kujirekebisha na si kumfanyia uhasidi mwandishi wa makala hii, maana kwa husuda na choyo zao, wanatamani maneno haya wangeandika wao.

Nawatakieni kila la kheri-Wabillah Tawfiq. Assalamu Alaiykum wa rRahmatullah wa Barakatuh



Upigaji wa Punyeto au Kujichuwa, ni tatizo kuwa sana kwa watu wengi na haswa vijana, ambao bado hawajaoa, vijana ndio wanaokabiliana kwa hali ya juu kabisa na vishawishi vinavyowazunguka katika jamii mbalimbali wanazoishi. 

Kupiga Punyeto au Kjichua wanaume au kujisaga wanawake ni jambo linalonyika sana katika jamii zetu mbalimbali. 
Na hata jumuiya au mashirika ya kupiga vita magonjwa ya zinaa kama vile Ukimwi, yamekuwa yakiwashawishi vijana au wale wote ambao wanataka kuingia kwenye maswala ya ngono watumie mipira au wapunguze matamanio yao kwa kupiga Punyeto/kujichuwa.

Idadi ya waathirika ni kubwa, janga ili si kwa vijana wa kiume na kike au makapera bali hata wazee na hata waliooa/kuolewa wamejikuta wakishindwa kuacha kabisa tabia hii.

Tatizo la upigaji wa Punyeto au Kujichuwa ni Kubwa na uchukuwa muda mrefu sana kwa aliyeacha kurudi kwenye hali ya kawaida, na wakati mwingine uwa ni tatizo la kudumu.

Sote tunakubaliana kuwa ngozi ya kwenye mikono ni tofauti kabisa na njia ya uzazi ya mwanamke, ngozi ya mkono ni ngumu na haina maji maji, ukilinganisha na uke.

Aliyezoea upigaji punyeto umwia vigumu sana kusimamisha anapokutana na mke wake na hata ikitokea kusimamisha basi ni pale alipovuta hisia na uku akijichuwa hali hii umfanya mwanaume kumaliza mshindo ndani ya dakika zisizozidi mbili tu.
Ndoa nyingi zimeingia kwenye matatizo yasiokwisha haswa kwa mume kutoweza kumtoshereza mke/wake zake katika tendo la jimai.

Hali hii upelekea kwa waathirika wa kupiga punyeto kushindwa kuwaridhisha wake zao na hata wakitakiwa kuendelea raundi ya pili wanakuwa hoi, na kushindwa kuendelea, matokeo yake ni ugomvi ndani ya nymba.

Wanaume wengi wamekuwa wakiacha wake zao, kwa kufikiria kuwa maeneo au tupu za wake zao zimekuwa chapwa, kumbe tatizo ni la wanaume wenyewe kwa kutoweza kuwa na hisia kwenye viungo vyao vya uzazi. Hali hii inatokana na kule kujichuwa kwa kutumia mikono, kiasi cha kuuwa hisia za kawaida ambazo mwanamume anapaswa kuwa nazo kwenye uume wake.

Lakini kwa kutokujua kwao kuwa wameviathiri viungo vyao kwa upigaji punyeto wa muda mrefu na matokeo yake kushindwa kuhisi hali ya ujoto na m’bano wa viungo vya uzazi vya mwanamke.

Hali hii inapojitokeza, wanaume wengi uhamua aidha kutafuta mke mwingine na mwingine na mwingine… Na kila anapoowa hali inakuwa ni ile ile, kwa sababu uume wake umekwisha athirika na upigaji wa punyeto wa muda mrefu.

Wengine ufikia kuvuka mipaka na kuwalazimisha wake zao kuwaingilia kinyume na maumbile, hii yote ni kutafuta kujiridhisha kingono. 
Na mwisho wake ni kutoka nje ya ndoa na kupata maradhi ya ngono kama vile Kaswende, kisonono, gonoria na hata Ukimwi.

Upigaji wa Punyeto, uathiri mwili kwa kiwango kikubwa sana, kesi nyingi zimeripotiwa kama kupatwa na saratani kwenye viungo vya uzazi kama vile Korodani (prostate-cancer). Mgonjwa uwa ni mwenye kwenda haja ndogo mara kwa mara haswa kipindi cha usiku, na upata maumivu kila anapokwenda haja ndogo. Na mkojo na manii ya mwathirika uchanganyika na damu.

Matatizo wanayoyapata waathirika wa upigaji punyeto au kujichuwa uchukuwa muda mrefu sana kurudi kwenye hali ya kawaida, na wakati mwingine uwa ni matatizo ya kudumu.

Baadhi ya madhara ya Waathirika wa Upigaji Punyeto na Kujichuwa.

  • Kupiga Punyeto Kunapelekea kufika mshindo kabla na bila kujijua na husababu matatizo ya Nguvu za Kiume.
  • Kutokwa na manii usingizini bila kujijuwa.
  • Maumivu ya mgongo.
  • Punyeto usababisha udhaifu wa mwili.
  • Kuwa na sura ya ujuvi.
  • Udhaifu wa Macho, kutoona vizuri.
  • Nywele Kutokuwa na Afya.
  • Kupungua uzito chini ya kiwango.
  • Uchovu na udhaifu wa mwili, wa mara kwa mara 
  • Kupata maumivi kwenye kinena.
  • Maumivu kwenye mapumbu.
  • Mbegu za uzazi kuwa dhaifu.
  • Kutosikia raha ya mapenzi/jimai.
  • Kupungua kwa hamu ya kula.
  • Matatizo ya kusimamisha.
  • Kupotea/kutosikia njege.
  • Kufikia mshindo mapema, dakika moja hoi.


Kama kuna fani inayovamiwa kwa nguvu hivi sasa na watu wengi basi ni fani ya habari. Kwa waliokwenda kujifunza fani yenyewe na wasiopata mafunzo, ambao wamejaribu na kuwa magwiji. Wabunifu wa habari katika aina tofauti tokea kusema, kuandika na kuchora picha na hatimaye kuzipeleka watakako aidha kwa walio waajiri au walio wakusudia tu, ili mradi wazipate hizo habari.

Fani hii pia haina rika, yeyote awezaye hujaribu na hata kama haelewi miiko, adabu za uandishi na upigaji wa picha zenyewe. Vibari vitakiwavyo au hata kujali mishahara. Naandika haya si kwamba naifuja fani hii ya habari bali nasikitika kuwa jahazi ili la kuleta faida kwa jamii limeingia wadau fujo, ambao vibari vyao vimo viganjani na vidoleni mwao.

Tumeyasema na tutaendelea kuyasema na ni wajibu tukumbushane, maana sisi binadamu tuna sifa ya kusahau na kujisahau.  Ni vizuri kusikiliza ulimwengu na maendeleo yake ya kiteknolojia, lakini eh! Mengine karaha maana viumbe sisi wa Mwenyezi Mungu tunapovuka mipaka kwa yale au vile vya kutusaidia vikawa ndio vitendea dhambi vya kiteknolojia.

Ugomvi humohumo, kashfa tele, uongo usio mfano, matusi na kujiona kuwa wajua zaidi ya wengine na wizi wa kimambo leo, umbea wa kisasa kwa njia ya teknolojia na waandishi bila fani wamekithiri.

Ni kweli kabisa maendeleo mapya uzaa tabia mpya na spidi tulionayo inachafua hata mashine za kupimia mwendo au gavana. Si majumbani mwetu, maofisini au hata kwenye mchanganyiko wa kijamii, ni zama hizi za kisasa za kuharakisha maendeleo ya kimaisha, Twitter, Youtube, Skype, Facebook, Whatsapp, Telegram, Talkray, Line, Viber na mitandao mingine kadhaa ya kiajabu ajabu.

Basi hiyo whatsapp kwa vijana ndio mbolea yao ya kimaendeleo na kujuwa mfumo wa haraka wa kurahisisha mambo.
Je viandamizi hivi kama nyenzo za kutusaidia ni vibaya kimadhumuni? Ili si swala linalotaka majibu ya ndio au hapana, bali lina mjadala mfupi sana. Vitendea kazi hivi vimesaidia kiasi gani na vimechafua kiasi gani, basi jawabu lake na ndio la kulijadiri na kutoa nukta ya kweli.

Lakini bado tunaweza kwa hasira tukaangalia maharibiko na tukasema kuwa havifai. Basi hatutakuwa tumetosheleza kukiaminisha kilio chetu. Kwa hiyo tutoe asilimia tustahiki, kisha tukanyane, kwamba ili kwa mitandao hii limefeli na ili limepasi liendelee.

Nadhani haya ni mazungumzo tu, kwani maji yamekwisha kumwagika, tuchukuwe tambara au spongi tupanguse au kukamua. Lakini kama ni farasi keshatoka bandani na anatimua vumbi na mlango kuufunga saa hizi ni kupoteza wakati bure. 

Basi dini bado ipo na itaendelea kuwepo na umma huu moja ya kazi yake kubwa ni kuamrishana mema na kukatazana maovu.

Tutokako kifaa kidogo cha mkononi unachozungumza nacho hivi leo, kiliogopesha mno na aliyenacho basi ni mtu wa idara nyeti kwa lugha ya kileo. Ukiharifu sheria basi utazungukwa kabla ujapepesa, kumbe wa ubavuni mwako kakuchuuza wewe huna habari.

Zana hizi tulizo zitaja sasa zimeenea na tena kwa utaalam mara dufu, na ndio ustaarabu mpya, vizibiti siri vipya na wepesi mpya wa mawasiliano na bado tutaendelea kuunda.

Nasema tunatumia kwa faida gani nzuri? Binafsi sijui maana hata kwa faida mbaya kwa wengine imetosha, maana hoja ni kuwaumbua wenzio na kuifurahisha nafsi yako. Kwa Allah tungojee hesabu.

Facebook, Twitter, Skype, whatsapp, Youtube na vinginevyo kweli ni daraja fupi za mawasiliano, lakini kwa wasiotumia vyema utu na heshima zao ni daraja dhaifu mno la kukuelekeza kwenye ghadhabu za Allah, kwani unasimanga, unakashifu, unazuwa uongo, unafitinisha na unaiba siri za watu bila idhini zao. Vyema kwenye ghafla njema, je kwenye yale yasio pendeza?

Jamani kwanini hata wagonjwa wapo ICU, atokee mtu na umbea wake kwa teknolojia ajidai anakwenda kukagua mgojwa, basi nafasi hiyo ya kipekee ya kusimama na kumuombea dua ndio atammulika na whatsapp huyoo dakika moja mgojwa wa watu kajaa duniani kote ana mipira kohoni, puani na waya za vifuani.
Mmbeya huyu keshakonga roho, kawafurahisha mahasimu wa mgonjwa hata maiti nayo upigwa picha akatangazwa bila ya idhini ya wenyewe.

Njoo kwenye huo mtandao wa Skype, matusi humohumo, wanaonana uso kwa uso, wa Ulaya, Marekani au Arabuni wanasutana kwa mtandao kwa walio Afrika. Kila mmoja anamlaani mwenzie kupitia katika kioo, utadhani jogoo pale aonapo ona jogoo mwingine kwenye kioo, kumbe ni mwenyewe anakiparura kioo, ndio tusi linakurejea.

Tizama mitandao inavyo tuchezea, uko kuchorana na kubadirishana sura na kuvalishwa usivyo vivaa au kuunganishwa na mtu husiye pendana naye, basi usiseme, ufundi wa haya upo kiganjani, tuna umbuana tu.

Nasema, hatutumii nehema vyema, tena na wakati hatuutumii ipasavyo, baadhi yetu hivi sasa hatuwezi kustaamiri dakika tano, tusivute simu zetu, tupigiwe au tusipigiwe, kila mmoja kainamia anapangusa kioo cha simu kama bao la kupigia ramli. Anaandika tu akifuta, si mirihi, si shamsi si kamari.

Ebu tukithirishe ibada, Allah tunamsahau, tunatumia vibaya mitandao, je hatujasoma ile ayah ya 148 ya Surat An-Nisaai, inayosema:

"MWENYEZIMUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua"

Basi tuyafanyao Allah anatujuwa, yeye ndiye aliyetuumba, tusijidanganye kwa kuwa ufundi sasa unazidi basi tutakufuru. Tunajuwa sasa simu zetu zinafanya kazi hata kwenye pipa la maji. Nyengine zinafunguka kwa kuzipepesea jicho au kupandisha nyusi, mbali ya hiyo miito ya milio ya mbuzi paka na mingine, inayokera hata msikitini.

Lakini kumbuka wewe na mimi tulikuwa nani kama si tone la maji ya uzazi, tushakuwa wajuwaji kwa kuwakera wengine!?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!