Thursday, 9 June 2016

Hivi inakuwaje Wafanyabiashara Wengi wa Kiislamu kwenye Mwezi Huu ndio upandisha bei bidhaa muhimu zinazohitajika katika mwezi wa Ramadhani?

Mwanzoni kabla sijasafiri na kwenda Ughaibuni, nilifikiria kuwa Waislam wa Uku wapo tofauti kitabia, nilipatwa na mshtuko kidogo pale nilipogundua kuwa Tabia zao hazina tofauti na uku nilipotoka lbda kwa kuwa Wengi wao ni Wahamiaji.

Na wengi wao walio hamia kwenye hizi nchi, si kwamba walikuja wao tu au walikuja wao na familia zao na Uislam wao, lah hasha, wengi wao walikuja wao na tabia zao.

Ndio utakuta wengi wao haswa wale waliotoka nchi ambazo kidogo kuna sheria kali kuhusiana na mambo ya kijamii kama vile unywaji wa pombe, uasherati, uchezaji wa kamali na mambo mengine yalio kinyume na Uislamu. Ndio wamekuwa mstari wa mbele kwenye kutekeleza hayo yote.

Kwa wale ambao wamehepukika na urahibu huo na wakabaki kuwa Waislamu wenye kwenda misikitini nao wamekuwa na matatizo yao mengine.

Nao pia wamekuja kwenye hizi nchi si na Uislamu wao tu, ila wamekuja na zilezile tabia ambazo uku Afrika tunaziona kuwa ni za kawaida.

Mfano utakuta misikiti mingi yenye kuongozwa na Wahamiaji aidha wawe wanatoka Afrika Magharibi au Mashariki au Afrika ya Kati au Kaskazini mwa Afrika, misikiti hii mara kwa mara imekumbwa na matatizo ya kiuongozi, ulaji wa pesa za msikiti na mambo mengi kadhaa yalio nje ya Uislamu.

Wale ambao wamejihusisha na biashara nao hawapo nyuma kwenye janga ili, wengi wao inapofika mwezi wa ramadhani, basi kwao ndio mwezi wa kujiongezea faida zaidi kwa kupandisha bei za bidhaa, na haswa zile bidhaa ambazo wanajuwa Waislamu wengi mwezi huu ndio wanazihitaji zaidi.

Wakati huo huo yale maduka ambayo si ya Waislamu wamegundua kuwa kwa kupunguza kwao bei za bidhaa wanaweza kuwavutia Waislamu kuja kununu vitu mbalimbali kwenye maduka yao. Kiasi ya maduka mengine wameamua kuyabadilisha na kuanza kuuza bidhaa halal ili biashara zao ziende vizuri.

Swali la kujiuliza, Waislamu sisi, tuna matatizo gani na Uislamu wetu?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!