Monday 17 October 2016

MALAZI YA KISAIKOLOGIA

UKOZIMENI au MPIGA CHABO ni maradhi ya kisaikolojia ambapo mwenye maradhi haya anakuwa na tabia ya kupenda kuangalia watu wasio na nguo. Mtu mwenye maradhi haya huitwa kitaalamu Voyeur (inasomwa vouya). Kwa Kiingereza cha kawaida, mtu huyu huitwa Peeping Tom, Waswahili humwita KOZIMENI au MPIGA CHABO. 

Mara nyingi kozimeni huwa na tabia ya kuchungulia watu walio kwenye faragha, na yeye roho yake hufurahi kuwaona watu walio wazi bila nguo, na furaha yake hufikia kilele kama atawaona mke na mume wako katika kitendo cha ndoa. 

Katika jamii yetu leo, maradhi haya yameingia kwa kasi. Tunao watu wengi waliozama hapa, na iko haja ya kupambana na maradhi haya, na hakuna anayeweza kupambana nayo bali sisi wenyewe.

Siku hizi, wenye maradhi haya huwezi kuwakuta sana wanachungulia madirishani au sehemu nyingine, kwa sababu wanaweza kushikwa na kuchomwa moto.

Kuna mbinu mpya za kukidhi haja ya wenye maradhi haya. Zamani, wengi walikuwa wakiangalia magazeti ya ngono au kanda za video. Siku hizi mitandayo ya Internet imewarahisishia kazi. Hawana haja tena ya kujifungia ndani na kuangalia magazeti ya ngono au kanda za video, maana wamerahisishiwa, wanachofanya ni kufungua simu zao za mikononi na kutembelea zile website zenye kuweka mambo wanayoyapenda. Hawa ni wagonjwa mahututi. 

Kuna wagonjwa wengine ambao sio mahututi sana, lakini nao pia ni makozimeni fresh. Kwa mfano, binti wa Kiislamu anaweza akaomba avae hijabu shuleni/kazini, lakini wapo watu hawakubali binti huyu afunike viungo vyake. Utamkuta mwalimu au boss wa kazini anakuwa mkali kabisa, kwani na yeye ni miongoni mwa watu ambao roho zao haziridhiki hasa anapo mwona mwanamke amejihifadhi.

Hawa ndio wale wale ambao huandaa kile kinachoitwa "mashindano ya uzuri" na kuwapitisha mabinti waliovaa "vichupi" mbele ya kadamnasi, na mwisho huwapa zawadi. Kwa bahati mbaya sana, wenye maradhi hawa ni pamoja na viongozi wa nchi. Wao hufungua na kushiriki katika mambo haya ya kukodolea macho watu walio uchi.

Vilevile wapo mabinti ambao wameathirika na ugonjwa huu kiasi ya kwamba wanaona kutembea nusu uchi ndio usasa, kiasi cha kuwaona wenzao wenye kujistiri kuwa wamepitwa na wakati.

Si ajabu leo kuwaona kinadada na kinamama wakicheza miziki ya dansi wakiwa nusu uchi na wengine ufikia hata kuvua nguo adharani, angalia kwenye maharusi pale tunapoambiwa kungwi anasaula zawadi za bibi harusi. 

Na vijana wa kiume nao hawapo nyuma katika ili, uatwaona wakitembea uku suruwali zao zikiwa zimeanzia chini ya makalio yao, kisa eti ndio kwenda na wakati.

Binafsi najiuliza, sasa uku ndio kwenda na wakati au kurudi nyuma ya wakati!?

Mtume amesema: "Jinsi mlivyo, ndivyo mtakavyotawaliwa", kwa hivyo, kama viongozi wetu ni wapiga chabo au ma Peeping Tom na ma Voyeur au Makozimeni, je wanaoongozwa watakuwaje!? 

Kiboko ya maradhi haya hakuna zaidi ya Uislamu kwani ndio unaotekeleza maamrisho ya MwenyeziMungu yasemayo: 

"Wala msiikurubie zinaa hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya kabisa".
Qur'an Sura Al Israai (Bani Israil) 17:32 

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!