Monday, 22 April 2019

JUMUIYA YA NATION OF ISLAM (NOI)

- Wallace Fard Muhammad,
- Elijah Muhammad,
- Warith Deen Mohammed
- Malcolm X
- Louis Farrakhan

Wengi wetu wamewahi kuona na kusikiliza Miadhara/Mahubiri ya Louis Farrakhan (Louis Eugene Walcott), kiongozi wa sasa wa Nation of Islam, dhehebu jipya linalijinasibisha na Uislamu nchini Marekani ya Kaskazini (USA).


Tunapo taka kumzungumzia Farrakhan, hatuwezi kuweka kando itikadi yake inayotokana na mafundisho yao yanayo shabihiana na Uqadiyyan.

Farrakhan kabla ya kujiunga na harakati za NOI, alikuwa ni mwanamuziki wa mtindi wa calypso Muimbaji na mpiga fidla (violin), na alitambulishwa NOI na rafiki yake na mwanamuziki mwenzake Rodney Smith, kwenye mkutano mkubwa wa mwaka uliojulikana kama Siku ya Waokozi (Saviours' Day).

Mkutano ambao ulikuwa unahutubiwa na Elijah Muhammad, alierithi uongozi kutoka kwa Wallace Fard Muhammad ambae ndio mwanzilishi wa NOI.


Na mwaka 1955, alikubaliwa kujiunga na NOI baada ya maombi yake kukubaliwa rasmi na Elijah Muhammad, na kupokea jina la X uku akisubiria jina jina, kutoka kwa kiongozi wa NOI (Wote wanaojiunga na NOI, upewa ubini wa X wakati wakisubiria majina mapya),  kwa hiyo akawa anaitwa Louis X, kabla ya kupewa jina Farrakhan, na baada ya hapo akatambuliwa rasmi kwa jina la Louis Farrakhan akiwa chini ya mafunzo kutoka kwa Malcolm X.

ELIJAH MUHAMMAD

Elijah Muhammad (Elijah Robert Poole) alizaliwa October 7, 1897 na kufariki tarehe 25 February, 1975.

Kulingana na maelezo yake mwenyewe, Elijah Muhammad, alifundishwa na Fard (mwanzilishi wa NOI) na mafunzo yake yalikua kila siku kwa miezi tisa mfurulizo, kisha mara kwa mara kwa muda wa miaka miwili.

Mnamo Mei 1933, muda mfupi baada ya kuhitimu na kusilimu na kupewa jina la Elijah Muhammad, Wallace D. Fard alipotea bila kuwajulisha wafuasi wake au kumtaja mrithi wake na hajaonekana mpaka leo.

Ndipo hapo Elijah, alipokamata uongozi, baada ya kuwashinda wapinzani wake kadhaa, Elijah Muhammad alisema kuwa Fard amemchagua kuwa mrithi wake na kumfundisha "mchana na usiku" kwa miaka mitatu. Alisema kuwa Fard alikuwa Mungu katika mwili (God incarnate), na kwamba Fard amemfunulia yeye peke yake na ndio Mtume wake.

Elijah Muhammad alianzisha gazeti, (The Final Call to Islam) Mwito wa Mwisho wa Uislamu, awali aklifundisha kuwa Fard ni nabii na baadaye akafundisha kuwa Fard ni Mwenyezi Mungu katika umbo la kibinadamu. (https://www.noi.org/noi-history/)


Elijah aliweza kupata wafuasi wengi kutokana na wengi wao walikuwa ni hoe hae kiuchumi, na NOI iliweza kuwasaidia kuwapatia kazi, kuwasomesha na kuwapa nyumba za kuishi.

Katika miaka ya 1970, NOI lilikuwa inamiliki Bekari za mikate, saluni za kunyolea, Migahawa, maduka ya vyakula, Maeneo ya kufulia nguo, Madanguro na klabu za usiku (night-clubs), mitambo ya uchapishaji, maduka ya rejareja, majengo mengi na mali zisizo hamishika, Mashamba Kadhaa makubwa, uko Michigan, Alabama, na Georgia.

Mpaka kufikia Mwaka wa 1972 NOI walikuwa na hisa kubwa kwenye mabenki ya Guaranty na Trust Co. NOI walikuwa wakimiliki shule kadhaa katika miji 47 nchini Marekani. Mwaka wa 1972, Muhammad aliwaambia wafuasi kwamba NOI lilikuwa na pesa zipatazo dola milioni 75.

UONGOZI MPYA

Alipofariki Elijah Muhammad mtoto wa Elijah Muhammad, Warith Deen Mohammed akachaguliwa kuwa kiongozi wa NOI. Na baade kubadilisha jina la harakati zao na kuita Jumuiya ya Kiislamu ya Ulimwengu wa Magharibi (World Community of Islam in the West). na baadae ikaitwa kwa jina la Jumuiya ya Waislamu wa Marekani (American Society of Muslims).


Warith Deen Mohammed alikuwa hakubaliani na mafundisho ya mwanzilishi wa NOI yaliokuwa yakifundisha kuwa Wallace D. Fard ni Mwenyezi Mungu katika Umbo la Kibinadamu na ndio Mahd na Masihi alie ahidiwa.

Na akaruhusu hata Wamarekani wenye asili ya Kizungu, kujiunga na harakati zao (Kabla ya hapo walikuwa hawaruhusiwi wazungu kujiunga nao, walikuwa wakiamini kuwa Wazungu wote ni Mashetani). Na alifanikiwa kuwavutia wanachama wasiopungua 2,000,000 (Milioni mbili wa NOI) kujiunga nae.

Farrakhan nae hakubaki nyuma, alijiunga na kumfuata kiongozi na Imam wao Warith Al-Deen Mohammed, wakifuata madhdhebu ya Sunni akiwa chini yake kwa miaka 3 1/2 kutoka mwaka 1975-1978. Imamu Muhammad akampa jina jipya la Abdul-Haleem.

KUASI KWA LOUS FARRAKHAN 

Lakini Mwaka wa 1978, Imam Farrakhan alijiondoa kutoka kwenye harakati za Warith Al-Deen Mohammed. Katika mahojiano ya mwaka 1990 na gazeti la Emerge, Farrakhan alisema kuwa alikuwa amekata tamaa na kuvunjika moyo baada ya kutambua kwamba imani iliyokuwa inafundishwa na Warith Al-Deen ilikuwa ya uwongo. Na akahamua kujiondoa kwenye harakati hizo na kuhuisha harakati zile zile zilizo hasisiwa na mwanzilishi wao Wallace Fard Muhammad.

Na Mwaka wa 1978, Farrakhan na akiambatana na idadi ndogo ya wafuasi waliamua kujenga upya Nation of Islam (NOI) kama lilivyokuwa awali na kuhuwisha ile misingi iliyoanzishwa na Wallace Fard Muhammad, na Eliya Muhammad. Hii ilifanyika bila ya kusemwa waziwazi.

Na baadhi ya itikadi yao ndio ile ya kuhitakidi kwamba Wallace Fard Muhammad ni Mungu katika Mwili na Elijah Muhammad ni Mtume wake.

Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa wao wanahitakidi kuwa Elijah Muhammad kuwa ni Mjumbe (Messenger) wa MwenyeziMungu, na uhitumia Ayah hii kutoka kwenye Qur'an:

Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Quran 10:47

Vilevile wanahitakidi kuwa mwanzilishi wa kundi lao Master W. Fard Muhammad, ndio huyo Masihi aliyehaidiwa wa Wayahudi na ndio huyo huyo Mahdi wa Waislamu na Ndio Mungu mwenyewe katika mwili.

Kubwa lingine kwenye vitabu vyao wanasema kuwa MwenyeziMungu alikuja duniani kwa umbo la kibinadamu na kwa jina la Fard Muhammad na kumchagua Elijah Muhammad  kuwa ni mtume au mjumbe wa MwenyeziMungu.

Ndio ukaona wakina Muhammad Ali na hata Malcolm X (Al-Hajj Malik Al-Shabazz) na wengine wakajitambua na kutambua kuwa hili ni kundi potovu wakajitoa.

Kwenye baadhi ya mafunzo yao wanasema kuwa:
- Watu weusi ndio hasa watu Halisi na wa Asili.
- Watu weupe (white people) ni Mashetani (devil).
- Watu weusi ni bora zaidi (superior) ya weupe.

Mtu mweusi nchini Amerika ya Kaskazini (USA) sio Negro, bali wao wanatoka kabila la Shabazz kabila lilipotea zamani, na waliibwa na wafanyabiashara kutoka Mji wao Mtakatifu wa Makka miaka 379 iliyopita.

Mtume (Fard) alikuja Marekani ili kuwaokoa ndugu zake waliopotea kwa muda mrefu, ambao Wazungu wamewapotozea lugha yao ya Kiarabu, utaifa wao na dini yao.
...Wanapaswa kujifunza kwamba wao ni watu wa asili, wa kwanza kabisa wa mataifa ya dunia. Wazungu yaani watu weupe wamepoteza rangi yao ya asili. Kwa hali hiyo basi Watu wa asili wanapaswa kurejesha dini yao, ambayo ni Uislamu, lugha yao, ambayo ni Kiarabu, na utamaduni wao, ambao ni elimu ya Anga (Elimu ya Faraki – astronomy) elimu ya juu ya hisabati, hasa mahesabu. Wanapaswa kuishi kulingana na sharia ya Mwenyezi Mungu, wakiepuka nyama zote zenye sumu kama vile, nyama ya Nguruwe, Bata, Bata bukini, jamii ya ndezi na samaki aina ya Kambare. Wanapaswa kuacha kabisa matumizi ya stimulants (Vihamshi), hasa pombe. Wanapaswa kujitakasa wenyewe - miili yao na nyumba zao. Na kwa njia hii watakua wakimtii Mwenyezi Mungu, nae atawarejesha tena kwenye Paradiso ambayo waliibwa uko kwenye mji wao wa asili- Mji Mtakatifu wa Makka.

Je Mafundisho ya huyu mtu yanafaa kusambazwa, maana itikadi yake haina tofauti na Maqadiyyan, hata huyu ana amini kuwa kuna mitume zaidi ya Mtume Muhammad (saw), je yafaa kujifunza kutoka kwao?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!