Sunday 7 February 2021

REINCARNATION (REINKARNASHEN) 

KUZALIWA UPYA - MU'JASSIMA

Uwezo wa Majinni na Ulaghai wao kwa Binadamu.

Reincarnation (Reinkarnashen) Kuzaliwa Upya au Mu'jassima, Ni dhana ya kuamini kuwa mtu aliyekwisha kufa kisha roho yake kurejeshwa tena katika mwili wa kiumbe kingine. Aidha anazaliwa kwenye mwili wa Binadamu au mwili wa Mnyama Kisha kuanza maisha mapya kwa sura tofauti ya mwili mwingine baada ya kifo cha kibaolojia.

Dhana ya mu'jassima, inataka kufanana kidogo na dhana ya Ufufuo (Resurrection), tofauti yake kubwa ni kwamba, ufufuo ni pale ya roho ya mtu aliyekufa hurejea tena kwenye uhai wa kidunia katika mwili uleule wa mwanzo, na hili kwa imani ya dini nyingi litatokea mwisho wa maisha ya kidunia. 

Katika imani nyingi zinazojumuisha kuzaliwa upya Mu'jassima, roho huonekana kama isiyoweza kufa na kitu pekee ambacho kinaweza kuharibika ni mwili. Baada ya kifo, roho huhamishwa (transmigrated) kuwa mtoto mchanga aidha wa kibinadamu au mnyama na kuendelea kuishi tena. 

Neno _transmigration_ linamaanisha uhamiaji au kupitisha roho kutoka kwa mwili mwingine hadi mwingine baada ya kifo.

Imani za kuamini Mu'jassima, ni jambo kuu kati ya dini zenye asili ya India na kusambaa kwenye nchi za Ashia (Asia), kama vile China, Japan n.k. Dini zenye kuamini Mu’jassima kwa uchache ni dini ya Jainism, Buddhism, Sikhism na Sanatana Dharma kwa jina maarufu Dini ya Kihindu. 

Na kuna aina nyingi za dini za Kijadi na Upagani zenye kuamini mu'jassima, ingawa kuna vikundi vya Wahindu na Baadhi ya Wapagani ambao hawaamini kuzaliwa upya, badala yake wanaamini maisha ya baadaye, yaani kufa na kufufuliwa siku ya Kiama.

Dhana ya mu'jassima, yaani mtu baada ya kufa roho yake inamwingia mtu mwingine haikubaliki ndani ya dini za Kiyahudi, Uislam na Ukristo (Abrahamic religions). Uyahudi, Uislam na Ukristo unaamini katika Ahela, kiama, kuhesabiwa na kulipwa lakini siyo roho ya mtu aliyekufa kumuingia mtu mwingine!

Japokuwa kuna makundi machache kwenye dini hizi tatu zinazo amini mu'jassima, hii ni kutokana na baadhi ya wafuasi walioamia kwenye dini hizi, kutoka kwenye imani ya reincarnation.

Kwa mfano; maandishi ya fumbo la Kiyahudi (Kabbalah), kutoka kwa orodha yao ya zamani ya Enzi za Kati na kuendelea, hufundisha imani ya Gilgul Neshamot (Kwa Kiebrania ina maana ya kuhama kwa roho ikiwa na maana ya Mzunguko wa Roho “soul cycle”). Lakini fundisho hili haliungwi sana mkono na madhehebu Kiyahudi ya Orthodox na halitiliwi mkazo mzito, kwa ufupi imani hii huikubali na wengi kama fundisho kweli.

Pia kuna dini za jadi za Kiafrika pia zina amini swala la kuzaliwa upya au kurejea kwenye maisha ya awali, mfano wa Babatunde au Babatunji (Kwa Mwanaume), Yetunde (kwa Mwanamke).

Na hata kwa makabila ya Afrika mashariki, kwenye koo mbalimbali kumekuwa na mila na utamaduni wa kufanya matambiko kama yalivyo makabila mengine duniani, kwa kuamini Mizimu ambayo kwa imani zao ni wale wazee waliofariki zamani, ambao kazi yao ni kulinda Koo zao au Kabila lao.

MAJINNI NA UWEZO WAO

Imani nyingi za jadi zina amini tu katika uwepo wa Mizimu, kuwa mababu waliokufa zamani uendelea kuishi na kulinda koo zao.

Lakini basi vipi mtu anaweza kusikia au kusoma kwenye vitabu au mitandaoni kuwa kuna watu wanaodai kuwa wanakumbuka baadhi ya mambo ya zamani kabla ya wao kuzaliwa, yaani mambo ambayo yaliwahi kutokea na wao wakayaelezea ilihali awajawahi kusimuliwa na yeyote yule?

Hili ni swala lenye utata mkubwa kiasi, kwa sababu wengi wanaodai hayo mambo awana uthibitisho wa kuthibitisha madai yao kiuyakinifu au Kisayansi (Japo kuwa si matukio yote yanaweza kuthibitishwa kisayansi).

Kumekuwa na uchunguzi na utafiti mwingi wa mambo yalio jificha (Paranormal), matukio yanayotokana na Psychokinesis/telekinesis au Clairvoyance ambayo ni zaidi ya upeo wa ufahamu wa kawaida wa kisayansi.

Kwenye ulimwengu huo wa mambo ya ajabu Paranomal ndiko kunako patikana viumbe visivyo onekana, lakini vyenye kufanya harakati zao kama binadamu. Kwa lugha rahiisi ni ulimwengu uliojificha wa Majinni, japokuwa wanaofatilia maswala haya ya Paranormal wao wanawatambua kwa jina la Ghost kwa Kiswahili tunaita Mizimu.

Wachunguzi wa mambo, wanatufahamisha kuwa Majinni ni viumbe kama binadamu tu, ila wao hawaonekani kwa macho kwa sababu wameumbwa kutokana na maada tofauti.

Kwa karne nyingi binadamu amekuwa akisimulia na uwepo wa viumbe hivi vinavyojulikana kwa majina mengi, kama vile Majinn, Mapepo, Vibwengo, Maruhani, Mazimwi, Mizimu na majina kadhaa wa kadhaa kulingana na tamaduni mbalimbali.

Kuna simulizi nyingi sana kuhusiana na Majinn na athali zao katika maisha ya kila siku.

Viumbe hao wana tabia za kuiga matendo na mienendo ya wanadamu na wanapenda kujifananisha na wanadamu.

Ni viumbe vyenye kuishi maisha marefu sana, si ajabu kusikia Jinni ana miaka elfu na zaidi, kwa kuwa ni viumbe wenye kupenda kujifananisha na Binadamu, ndio utaona hata maisha yao upenda kuishi miongozi mwa Binadamu/Watu.

Sasa basi, inavyo fahamika ni kwamba, kila binadamu anaye Jinni anae andamana nae, huyu uitwa Karin (Qarīn). Aidha anaweza kuwa yupo na mahusiano kwa maana ndio hao tunao wasikia wanapandisha vichwani mwa watu, au anaweza asipande, au yupo yupo tu na ndio wenye kumshawishi binadamu kufanya maovu au kuwa na fikra mbaya, kiufupi Jinni anaye jinasibisha na binadamu wanakuwa waongo sana.

Inapotokea sasa mtu amefariki, kwa Majinni wakorofi au wapenda sifa (Kulingana na tabia za marehemu) ndio uja kupanda vichwani mwa watu na kujifanya kuwa wao ni marehemu na kuanza kudai mambo kadhaa wa kadha.

Na wakati mwingine uweka mawazo yao kwenye vichwa vya waanga (Victims) wa harakati zao ndipo hapo utaposikia wengine wakidai kuwa waliwahi kuishi zamani na hata kutaja majina ya watu wa zamani zaidi ya miaka mia iliyopita, kumbe ni yule Jinni ambaye alikuwepo enzi hizo ndio mwenye kuleta habari kwa mlengwa.

DÉJÀ VU - MATUKIO YANAYOTOKEA NA UKAHISI UMESHA YAONA KABLA

Ni hisia za mtu kuhisi kuwa tukio linalotokea hivi sasa mubashara ameishawai kuliona kabla halijatokea sasa.

Hi ina maansha kuwa mtu anaweza kuona tukio linalo tokea sasa hivi na kuhisi kuwa tukio ilo, alisha wahi kuliona kabla, hali hii kwa Kifaransa inaitwa Déjà vu na kwa lugha ya Kiingereza ni Already Seen.

Hali hii mara nyingi usababishwa na matatizo ya neva (neurological anomaly) inayohusiana na magonjwa ya akili mfano wa kifafa katika ubongo, hali hii upelekea kuunda hisia kali kwamba tukio linalotokea hivi mubashara hivi sasa tayari ulishawahi kuliona siku za nyuma.

Hali hii kama itakuwa inajitokeza mara kwa mara, basi ni dalili ya kiashiria cha ugonjwa wa neva au ugonjwa wa akili, tatizo linakuja kwenye akili ya mtu, kushindwa kuchanganua au akili kushindwa kukubaliana na tukio husika kuwa limetokea, sasa ili ubongo usiathirike ndipo hapo ubongo unapo jiridhisha kuwa ilo tukio ulisha wahi kuliona kabla, lakini bila kujuwa wapi na lini limekutokea.

Hali hii inapozidi upelekea mtu kupata matatizo ya akili na kuanza kuhisi kuona vitu ambavyo havipo yaani kunza kuota akiwa macho kwa Kiingereza wanaita Hallucinations.

Hallucinations ni kama aina ya Ndoto lakini unaota ukiwa macho na si usingizini ni aina ya hisia ambazo zinaonekana kuwa za kweli lakini zinaundwa ndani ya akili ya mtu tu.

Mfano wake ni pamoja na kuona vitu ambavyo havipo, kusikia sauti, kuhisi hisia za mwili kama hisia za kutambaliwa na wadudu kwenye ngozi au kuhisi kuguswa, au kuhisi harufu mbaya au nzuri ambazo hazipo. Wakati mwingine kuhisi watu wanakusema au ukiona watu wanacheka ukahisi wanakucheka wewe n.k.

Haya yote ni magonjwa ya akili ambayo usababishwa na nguvu za kijinni au kwa Kiswahili chepesi ni nguvu za Mashetani ya Kijinni.


MAANA YA MANENO

Telekinesis: uwezo unaodhaniwa wa kusogeza au kunyanyua vitu vikiwa mbali kwa kutumia nguvu ya akili au njia zingine zisizo za kisayansi. Kusogeza au kunyanyua vitu (Maada) bila kuvigusa kwa kutumia nguvu zisizo onekana.

Clairvoyance: (Maono): ni uwezo wa kupata habari juu ya kitu, mtu, eneo, au tukio fulani kupitia maono au utabiri.


Maelezo Haya Yamenukuliwa Kutoka Kwenye Kitabu: 

MAJINN (DJINN) Na UWEPO WAO

UCHAMBUZI WA KISAYANSI


0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!