Friday 1 April 2022

 
FUNGA YA MWEZI WA RAMADHANI
1443 / 2022

Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Tarehe 1 Ramadhan 1443, Sawa na arehe 2 Mwezi wa Nne Mwaka 20202.

Kwa niaba ya familia yangu tunatoa salamu zetu za kuwatakia waumini wenzetu wa dini ya kiislamu mfungo mwema.

Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unakuja wakati ambao kuna janga la ugonjwa wa tauni (Covid-19). Vita na machafuko ya kiubaguzi kwa ndugu zetu katika Iymaan uko Bangladesh ambako ni makazi ya wakimbizi milioni moja wa kabila la Warohingya kutoka Myanmar. Bila kuwasahau ndugu zetu kutoka Somalia, Iraq, Palestine, Syria, Afghanistan na kwengine kote duniani.

katika dunia ambayo kila uchao tunashuhudia machungu na mateso ya binadamu pamoja na kukata tamaa, huku watu takribani milioni 70 wakiwa wamefurushwa makwao, uvumilivu na huruma ambavyo ni maadili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote ule.

Kwa mantiki hiyo, tutumie mwezi huu wa kujitafakari kwa kukumbuka watu waliopoteza maisha kwenye gonjwa la Korona na wale wote waliokimbia nchi zao wakisaka usalama na hifadhi nchi nyingine...

Tuwakumbuke kwenye dua zetu ndugu, jamaa na marafiki waliopotea maisha kutokana na ugonjwa wa Korona, na tumuombe MwenyeziMungu atuepushe ugonjwa huo.

Tunawatakia Waislamu wote Ramadhani ya Baraka na tawfiyq ya kutekeleza 'ibaadah za aina mbalimbali kwa wingi na kutakabaliwa ibada zetu tuchume thawabu tele, na madhambi kughufuriwa, na kudiriki tuipate Laylatul-Qadr na kuachwa huru kutokanana na Moto. Pia tunamuomba Allah Atuhifadhi na maradhi yaliyosambaa na Atuepushe na kila shari 
Aamiyn.


Tukikamate kwa Magego, Kile Kinacho Tuunganisha Kuliko Kile Kinacho Tutenganisha.


Ndugu yenu katika Iymaan

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!