Sunday 15 November 2015


Tumeshuhudia kwenye luninga zetu na mitandaoni mashambulizi ya mabomu na risasi za rasharasha zilizofanyika kwenye kumbi za michezo na kiwanya cha mpira uko Ufaransa jijini Parisi.

Tukio ambalo limekamata habari kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, kwenye lunginga na kwenye tovuti mbali mbali zimetumwa picha kadhaa zikionyesha matukio hayo.

Na baadhi ya picha ni za kushangaza sana kiasi cha kutilia shaka tukio zima la huo unaosemekena kuwa ni ugaidi. Hali ilianza kutia shaka pale zilipo okotwa pasi ya kusafiria (Passport) inayosemekana kuwa ni ya mmoja wa hao magaidi aliyejitoa muhanga.

Kwa mtu aliye makini anaweza kujiuliza mara mbilimbili, hivi mtu ambaye anakwenda kwenye kujitoa muhanga kwanini abebe pasi yake ya kusafiria na kwanini kila tukio la aina hii zidondoshwe pasi za kusafiria.

Kama mtakumbuka lile tukio lililopita lililo husu ofisi za wachora katuni Charles Hebdo nako kulidondoshwa pasi ya kusafiria, uko Marekani tukio la Bostoni nako alikadhalika walidondosha kitambulisho kuonyesha kuwa wao ni magahidi. Tunaweza kusema kuwa labda ndio staili yao, lakini haileti maana kwa mwalifu kufanya kitendo kama iko, tena basi ajabu mtu anajilipua, mwili wake unatawanyika vipande vipande kiasi cha kutoweza kutambulikana tena, lakini ajabu ya ulimwengu pasi ya kusafiria inapona tena haina hata chembe ya damu.


Haikutosha jambo ilo, baada ya tukio ilo la jijini Parisi, ndege za kivita zisizopungua kumi za Ufaransa zimefanya mashambulizi kwenye kambi za ISIS uko Raqqa Syria, walilenga shabaha yao kwenye makao makuu ya Daesh eneo ambalo ndio command post.

Shambulio lingine limefanywa kwenye kituo cha mafunzo na uandikishaji wa wapiganaji wa ISIL ambapo pia ndio kuna ghala la siraha pamoja na mafunzo.

Tunaweza kusema kuwa Ufaransa wamelipa kisasi, la hii si kisasi bali ni tukio ambalo lilikwisha ratibiwa siku nyingi ila kulikuwa kunatafutwa sababu tu ya kushambulia. Tunapaswa kujiuliza kama kweli hawa watu wanapigana na magaidi, ili eneo kweli walikuwa hawalijui? Na kwa nini lisishambuliwe siku zote hizo wasubiri mpaka limetokea shambulio ndio wamepata hamasa ya kushambulia uko Raqqa?

Hapa kuna mchezo unafanya na kina sie ambao hatupendi kutafakari matukio tunaona kuwa ni sawa tu, lakini kama haitoshi katika picha mabazo zimetumwa kwenye mitandao ya habari, kuna picha moja ya ajabu sana. Kuna picha ya Mwanamke au ni msichana ambaye taswira yake imeshapata kuonekana kwenye matukio kadhaa ya kigaidi yaliokwisha pita.

Huyo msichana alikwisha pigwa picha kwenye tukio la kuuwawa baadhi ya wanafunzi shuleni uko Marekani, pia ameonekana kwenye tukio la kule Boston Marekani kwenye mashindano ya marathon miaka michache iliyopita, haikutosha matukio hayo mawili msichana huyo huyo ameonekana kwenye tukio la Paris ufaransa akiwa ni mmoja wa waanga wa mashambulizi. Tunajiuliza kote uko alikuwa anafanya nini, je haileti tafakali kwenye vichwa vyetu kuwa awa watu wanatuchezea akili zetu?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!