Wednesday 25 November 2015


UELEWA MBAYA WA SUBRA NA UVUMILIVU KWENYE NDOA.

Wengi wetu tunapoingia kwenye mahusiano ya ndoa, kama umebahatika basi ushauri wa kwanza kupewa ni kuambiwa kuwa “Ndoa ni Subra na uvumilivu. Kama ni mwanaume/mwanamke uambiwa amfanyie subra na kumvumilia mkewe/mumewe na hii maana yake ni kwamba, chochote kitakacho tokea basi akivumilie na kukifanyia subra.

JE HIYO NDIO SUBRA NA UVUMILIVU INAOKUSUDIWA?

Kwenye mahusiano ya ndoa ni makutano ya watu wawili waliolelewa au waliotoka kwenye mazingira na wakati mwingie tamaduni na asili tofauti, na hii ufanya watu awa wawe na tabia tofauti na matarajio tofauti. Na wawili awa wanapoamua kukaa pamoja basi bila shaka tutarajie mgongano wa kifikra/kimawazo, kiutamaduni na hata kimaslahi.

Muungano huu una uwezekano wa kuwa na migogoro kutokana na tabia tofauti za wana ndoa.
Sasa basi kama kukitokea kasoro au kutofahamiana kwenye jambo husika nini kifanyike, Je ni kulinyamazia tatizo kwa kulivumilia na kulifanyia subra?

Wengi wa wanandoa aidha wanaume au wanawake uchukulia kwa maana tofauni neno “UVUMILIFU NA SUBRA” kwa kufikiria kwamba kama kuna kosa limefanyika basi ni kulinyamazia tu na litapita na maisha yataendelea kama kawaida.

Wanasahau kuwa ndoa ni sawa na karatasi nyeupe ambao inawakilisha mahusiano ya ndoa yao na kila tendo au neno ambalo si nzuri ni sawa na kalamu ya risasi (Penseli) ambayo inakifutio chake, kukitumia kifutio au kutokitumia ni juu ya wahusika wenyewe.

kukaa kimya au kwa Kiswahili cha mtaani “Kumezea” jambo lenye maudhi si kwamba litakuwa limefutika kwenye moyo, la hasha, jambo ilo uendelea kuwepo umo siku zote za maisha ya wanandoa. Na kila linaponyamaziwa jambo lenye kuchukiza au lenye maudhi, basi uungana na lile lililopita na hii usababisha kuendelea kujikusanyia maudhi kwenye moyo na akili ya muhusika kila leo, kwenye chumba cha uvumilifu na subra.

Matokeo yake maudhi na kero zile zinapofikia kujaza ile karatasi nyeupe ndio utokea miripuko ya magomvi na majibishano yasiokwisha kwenye ndoa, 

kiasi hata wakija wasuruhishi na wana ndoa hao wakiulizwa tatizo ni nini, wakakosa jinsi ya kujieleza zaidi ya maneno kama vile “...Huyu hana adabu, huyu mjeuri huyu... au Ananionea tu

Ukiuliza ni vipi kakosa adabu au ujerui wake ni nini, jibu lake san asana utasikia “...Aaah, basi tu mjeuri huyu hana adabu

Wanandoa awa wamesahau kuwa zile kero na maneno madogo madogo ambayo yangewezwa kurekebishwa tangia awali, kwa kuyaongelea baina yao mapema yangekwisha futika kwenye karatasi ile, lakini waliyazarau kwa kuona tu ni mambo madogo madogo, wakasahau kuwa madogo madogo ukuwa kiasi ukasahau jinsi yalivyokuwa hapo nyuma.

Ndio utaona wanandoa wengine uishi pamoja kwenye ndoa bila furaha wala amani kwa kuwa tu wamepata watoto na wanaishi kwa sababu ya watoto zao au wazazi wao, ila wao wenyewe hawana raha ya ndoa yao.

Suluhisho la matatizo ya ndoa ni kila siku, kila linapotokea jambo ambalo halikumpendeza mmoja wa wana ndoa basi linapaswa lizungumzwe kwa namna nzuri. Na si kwa namna ya ukali au kwa namna ya kejeri na masimango. Kwa sababu lisipo zungumzwa kwa kisingizio cha uvumilivu au subra matokeo yake uchochea sumu ambayo mwishowe uleta madhara kwenye ndoa na matokeo yake ndoa uvunjika au kuishi kwenye ndoa yenye magomvi kila kukicha.

Tunapaswa kufahamu kuwa neno subrana uvumilivu lina maana ya kusubiri ns livumilia pale tunaporekebishana kwenye kila jambo linalosibu kwenye maisha ya ndoa na si kuliacha likamea na kuwa jiti kubwa lenye majinamizi ya kuangamiza ndoa zetu.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!