Monday 18 January 2016

Nakumbuka zamani mtu akitaka kuvua nguo hadharani, watu watakuja haraka na haswa kama ni mtaani basi majirani wanakusitiri kabla hujajiumbua zaidi.

Kila mtu alikuwa anajuwa wazi kuwa ni chizi (Punguani) tu anaeweza kuvua nguo hadharani. Lakiini siku hizi hata sielewi wananchi wamekumbwa na maswahibu yepi! Kwenye shughuli ndio kabisa dada zetu utawakuta wamevaa madera, lakini yanaonyesha jiografia yote na mipaka yote ya mwili, yaani milima na mabonde, misitu na mapori yote yanaonekana hivi...!

Haitoshi uko mitaani, siku hizi kumekuwa na mashindano rasmi ya kutembea nusu uchi, yaani utawakuta watu wanalipia mapesa kibao kisa kwenda kuangalia wenda uchi...!

Uko mitaani nako ndio kabisaa, maana hata wanaume nao utawaona wakitembea suruwali ziko chini ya makalio yao.

Nyimbo zao basi uko kwenye Runinga, balaa, yaani hata kuelezea mashindwa, yani uwezi angalia na mkweo au watoto zako...!

Swali ninalo jiuliza na sipati jibu ni hili, je machizi siku hizi wamezidi!?

Na kwa kuwa hakuna anaewasaidia kujistiri ina maana machizi wamekuwa wengi kuliko wenye akili?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!