Tuesday, 2 February 2016

UNAFIKI WA NCHI ZA ULAYA NA AMERIKA.

Kushoto ni Mtoto aliyeathirika na Kirusi cha Zika

Kirusi cha Zika kina mahusiano ya karibu na kirusi kinachosababisha homa ya dengue, Homa ya Manjano (yellow fever). Iki Kirusi kimegunduliwa miaka ya 40.

Wataalam wa afya wanahisi kirusi hiki kilianzia aidha nchi za Kiafrika au Asia, na inasemekana Mwaka 1947 kwenye msitu wa Zika nchini Uganda karibu na Ziwa Viktoria, walichua aina ya nyani wenye mikia mifupi wakati kwa ajili ya utafiti wa chanjo ya Homa ya Manjano (yellow fever).

Baadae wakaja kugundua kuwa njani waliokuwa wakiwafanyia majaribio wamepata aina ya homa tofauti na Homa ya Manjano, ndipo homa hio wakaita Zika na vijidudu vilivyo sababisha hiyo homa ambavyo kwa asili vinatokana na virusi vya Homa ya Manjano wakavipa jina Zika Virus, hii ilikuwa miaka ya 1950.

Baadae kwenye miaka ya 60, alipatikana mgonjwa nchini Nigeria na ugonjwa ukaenea inakisiwa ni kuanzia miaka ile ya 1950 mpaka 1981.

Baadae wagonjwa kadhaa wakaanza kupatikana kwenye nchi za Kiafrika kama vile Afrika ya Kati, Misri, Sierra Leone, Tanzania, na Uganda. Na nchi zilizo Asia kama vile India, Indonesia, Malaysia, Philippines, Thailand, na Vietnam.

Kirusi hiki kinasambazwa na aina fulani ya Mbu na haswa kipindi cha mchana. Kirusi hiki kinaambukiza na kama mama ni mja mzito basi Kondo lake au mfuko wa Kizazi uathirika na mtoto aliyeko tumboni naye uathirika kwenye ubongo wake na mtoto uzaliwa akiwa mwenye matatizo ya kiakili.

Miaka yote hoyo hakuna nchi yoyote ya Ulaya au shirika lolote la Kimataifa, lililothubutu kusema chochote au kuchukuwa hatua yoyote kudhibiti kuenea kwa kirusi hiki, kwa sababu hakikuwepo kwenye nchi za Ulaya na Amerika.

Mwaka 2014, kirusi au wagonjwa walianza kupatikana kwenye nchi zilizo kwenye ukanda wa Bahari ya Pacific haswa nchi zinazojulikana kama French Polynesia.

Nchi ambazo ugonjwa huu umeenea ni New Zealand, Samoa, Tonga, Cook Islands, Tuvalu, Tokelau, Niue, Wallis, Futuna, Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon, na Fiji.

Baadae mwaka 2015 nchi za Mexico, Amerika ya Kati, nchi za Karibbeian, Amerika ya Kusini kama vile Brazir, Kirusi cha Zika kimetangazwa kuwa ni Janga la Kitaifa.

Mwezi December mwaka 2015, nchi za Ulaya (European) kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchi za Ulaya (European Centre for Disease Prevention and Control) Wameweza kutoa ripoti kamili jinsi kirusi iki kinavyo athiri binadamu na hatua za kuchukua haswa kwa wamama wajawazito.

Na hii imetokana kuwa nchi za Ulaya na Amerika kuna wagonjwa ambao wameathirika na kirusi iki, kama vile tulivyo shuhudia wagonjwa wa Ebola walipopatikana nchi za Ulaya na Amerika, ndio nchi hizi zikazibduka na kuona kuwa ili ni tatizo la nchi zote Ulimwenguni na si nchi za Kiafrika na Asia tu peke yake.

Hapa ndio utaona kuwa hizi nchi kama janga alija wakuta, mashirika ya Kimataifa kama vile shirika la Afya Duniani, WHO (World Health Organisation). Uwa awachukulii kuwa haya majanga yanayoikumba Afika au Nchi zilizo Eshia (Asia) yanaweza kufika kwenye nchi za Ulaya na Amerika. Ni mpaka pale wakipatikana wagonjwa kwenye nchi zao ndio utaona kuwa wakichukua hatua za kudhibiti na hata kufanya uchunguzi wa kina jinsi ya kuzuia au kutibu kwa magonjwa husika.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!