Tuesday 14 June 2016

MATUKIO YA MAUWAJI YALIOPANGWA NA SERIKALI.

Ukiwa mtu usiyependa kutafakari hali halisi ya siasa za kimagharibi haswa nchi za Ulaya na Marekani, unaweza kudhani kuwa serikali haziwezi kupanga matukio ya kuuwa raiya zake.

Ukiwa na fikra hizo, basi utakuwa si mfuatiliaji wa matukio ya kigaidi, yanayotokea sehemu mbalimbali haswa kwa nchi za ulaya na Marekani, na kisha kusingizia walengwa maalumu kwa malengo yalioko tayari hewani.

Sababu ni nini, KWANZA ni kuhakikisha wananchi hawasahau kuwa serikali yao ipo vitani wakipambana na magaidi, na hao magaidi wakati wowote wanaweza kuvamiwa mahali popote wakati wowote katika miji ya yao.

PILI ni kuhakikisha kuwa raiya waendelee kuwa na hofu ya jinamizi la ugaidi haswa makundi kama ISIS au ugaidi wa Kiislamu, (Zio-Islamic Terrorism) ni tishio la kweli la ustaarabu wa Kimagharibi.

TATU watambue kuwa maeneo mbalimbali kama vile mashuleni, majumba ya sinema, klabu za usiku, na sehemu mbalimbali za starehe na makundi mbalimbali ya kijamii kama vile mashoga, nk. Wanakuwa ni walengwa wakuu katika jamii, ili kila mtu awezwe kuguswa pindi tu matukio ya mauwaji yanapotokea.

NNE, kuondoa kila mwonekano mzuri wa Uislam au Waislamu, pale itakapotokea Uislamu kutajwa kwa namna yoyote nzuri, basi kupatikane jambo lingine litakalohamsha hisia hasi dhidi ya Waisamu au Uislam.

Katika mfano mmoja wapo ni habari ya kifo cha aliyekuwa Bingwa wa Dunia wa mchezo wa Ngumi, Mohammed Ali. Mambo mengi yameongelewa kuhusu Bingwa huyu alieaga dunia hivi karibuni, na kwa namna moja au nyingine watu wengi walisha anza kuutazama Uislamu kwa jicho lingine.

TANO, matukio yote ya kutengenezwa na kutolewa idadi ya watu wengi waliopoteza maisha, uwezi kuonyeshwa maiti za watu waliokufa, japo kuwaonyesha wakiwa wamefunikwa shuka ili kuonyesha hishima kwa mahiti na ndugu wa waanga. Siku zote utolewa tu idadi ya watu bila kuonyesha uthibitisho wa kweli.

Hapa vilevile ni njia nyingine ya kuwaelekeza watu wasishughulike na mambo mengine muhimu ya kiserikali haswa yahusuyo mustakabari wao na maisha yao na serikali ipate nafasi ya kuweka sheria na taratibu mpya dhidi ya wananchi kwa kisingizio cha ugaidi.

Tukiliangalia tukio lililo tokea hivi karibuni kwenye mji wa Orlando nchini Marekani, tunaona kwamba halina tofauti na matukio mengine yanayopangwa na serikali (False Flag) ili kuwatisha wananchi na kuongeza hisia kali ili serikali ipate nafasi kutekeleza agenda zake za siri na za dhahiri.

KUNA MAMBO KADHAA YA KUANGALIA HAPA:

Kwanza Muhusika ni mfanyakazi kwenye kampuni ya Kiingerza ihitwayo Group 4 Security (G4S): G4S ni kampuni kubwa sana ya Kimataifa ya Uingereza ya ulinzi binafsi, iliyo na sifa mbaya kiutendaji. Ni kampuni yenye mahusiano ya karibu sana na Israel, vilevile wana mahusiano na mashirika ya kijajusi na kintelejisia (security-intellignece apparatus) na nchi za Marekani, Uingereza na Uzayu yaani US-UK-Zionist axis (CIA, MI6, Mossad).

Kwa mfano, G4S ilikuwa ikiisaidia serikali ya Israel kusimamia wafungwa walioko kwenye magereza ya Kiyahudi na hata kuwasafirisha kutoka nchi nyingine kwenda Israel kabla ya kujitoa hivi karibuni kutokana kuvuja kwa habari kuwa G4S wana tenda kutoka serikali ya Kiyahudi. (shukrani kwa wana harakati wa BDS ).

Mtuhumiwa wa mauaji kwenye Club ya Mashoga anaitwa Omar Mateen, mwenye umri wa miaka 29 Muislamu, kabla ya kifo chake alikuwa ni mfanyakazi G4S tangu mwaka 2007. Japokuwa wafanyakazi wenzake walikuwa wakimuona kama mtu hasie eleweka na mwenye akili zisizo sawa (unhinged and unstable), lakini bado alipata kazi na kuajiliwa.
Ukiasoma toleo la mtandaoni la jimbo la Washington blog, limeelezea kuwa:

Kampuni ya G4S ndio walikuwa na jukumu la ulinzi kwenye maghorofa pacha maalufu kama 9/11 pamoja na ulinzi shirikishi kule Guantanamo: soma hapa Terrorism and G4S: Was Orlando Another False Flag?

Kabla ya tukio la 9/11 kampuni ya Securicor, ndio walikuwa na tenda ya kusimamia usalama kwenye viwanja vyote vitatu vilivyohusika kwenye tukio la 9/11 kabla ya G4S kabla ya kuchukuwa wao miezi tisa kabla ya tukio la 9/11 na baadae kupata tenda ya ulinzi kwenye jela ya Guantanamo Bay. G4S Sells Guantanamo Bay Service Unit for $135m

Ajabu ni kwamba, wauwaji wote ambao wanahusika na matukio haya ya kigaidi, uwa wanajulikana na FBI kabla ya matukio husika, kwa ufupi FBI wanakuwa tayari wanawajua.

Ndio maana tunasema kuwa matukio haya ni ya uongo, kwa sababu wauaji wanakuwa wapo chini ya uangalizi wa FBI au mashirika mengine ya kijajusi.

FBI walisha wahi kumuhoji mara mbili muuwaji; na wakafanya tathmini ya uwezo wa kiakili, na hii inathibitisha kuwa, FBI ni maarufu kwa matukio kama haya "sting operations", ambapo huwa ina tengeneza matukio bandia ya kigaidi kwa kutaka kuwaonyesha wananchi kuwa wapo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Ugaidi. Na wanafanya juu chini kuhakikisha usalama wao, na wakati huo huo kwa kukosa matukio ya kweli matokeo yake ndio inatengeneza matukio kama haya ya kuchezea akili za watu, ili kutaka kuthibitisha kuwa ugaidi upo.

Habari zilizo na uthibitisho, zinasema kwamba Omar Mateen, yeye binafsi alikuwa ni shoga, tena alikuwa ni mteja mzuri kwenye club hiyo ya mashoga.

Muuwaji huyu aliwahi hata kujaribu kuanzish programu ya mashoga (gay-dating App). Zaidi ya hayo, yeye amezaliwa na kukulia Amerika. Aliyekuwa Mke wake, baba na jamaa zake wa karibu wote walidai kuwa yeye haikuwa mtu wa dini hata kidogo.

Mashoga wenzake wanasema kuwa alikuwa mlevi na mtu wa fujo, pindi tu anapolewa au kuudhiwa kidogo na mara nyingi amekuwa akitolewa nje ya klabu hiyo kwa ukorofi wake.

Wafanyakazi wenzake na marafiki zake wanaeleza kuwa alikuwa mtu apendae kukaa peke yake peke yake, hakuwa mtu wa kujichanganya na jamii, na mara nyingi alikuwa mtu mwenye kauli za vitisho dhidi ya watu wengine.

Mke wake alimkimbia kwa sababu ya kumpigwa mara kwa mara. Na bado, vyombo vya habari vinaendelea kumuhusisha mtu huyu na 'Uislamu' ilihali hakuwa na Uislamu wowote kwenye matendo na tabia zake.

Kwanza ni shoga aliyechanganyikiwa kiakili (deranged psychopathic) mtu ambaye alikuwa akipambana na utambulisho wake wa kijinsia.

Pili mtu huyu ametumika tu kuziba kashfa kibao za serikali ya Marekani kuhusiana na mambo mengi ya kijamii, haswa umilikifu wa siraha kwa raiya na mambo mengi ya kijamii yasio pendeza kwa raiya wa Marekani.

Kila utakapo sikia matukio ya Ugaidi, basi utaambiwa kuwa muuwaji amekwisha uwawa, kwa sababu kuna msemo mmoja wa kiingereza usemao "Dead men tell no tales". Wafu hawasemi.

Omar Mateen amekwisha uwawa kwa kupigwa risasi, hivyo hatutasikia ushahidi wake. Hii si mara ya kwanza kutokea kwa muuwaji kuwawa, na hii ni kuthibitisha kuwa mashimo yanafukiwa ili kusiwepo ufatiliaji, kwa sababu akiwa hai anaweza kusema ukweli.

Habari zingine zinasema kuwa Omar Mateen ni muungaji mmkono wa makundi ya kigaidi kama vile ISIS, kumuunganisha Omar na ISIS ni kuendeleza mwenendo uleule wa kuwatisha watu kuwa kuna majinamizi yanayotishia amani ndani na nje ya Marekani na Washirika wake.

Tuna shuhudia tena kwa mara nyingine karata turufu ya kuwatishia Wamarekani inatumika kwa mara nyingine tena ili kuwaonyesha Wamarekani kuwa ISIS wapo na wamedhamiria kweli.

Wanasahau kuwa kwa sasa ni dhahiri iliyo wazi watu wengi wanatambua kuwa ISIS-IS-ISIL-Daesh ni US-Israeli creation. zao la Israel na Marekali.

Habari zingine zinasema, kulikuwa na mazoezi ya uokowaji miezi mitatu nyuma kwenye sehemu ya tukio <Link
Ndani ya nchi ya Marekani na Ulaya ya Magharibi, utokea matukio kadhaa ya mauwaji na ni mengi sana kulinganisha na matukio yano wahusu wenye majina ya Kiislamu.

Kuna matukia yanayofanywa na Wayahudi wenye misimamo mikali, Wahispania na wahusika wa madawa ya kulevya au wana harakati tu wa mkono wa kushoto (Leftists). Lakini ajabu uwezi kuona yakipewa kipaumbele kama vile wanavyo yapa kipaumbele matukio yanayo wahusu wenye majina ya Mashariki ya Kati.

Muislamu ataitwa Gaidi, lakini Mayahudi au Wahispania au hata wana harakati mbalimbali hawata waita Magaidi, bali kiradikali yaani "Radical or lonely worf" na majina mengine kuwaonyesha kuwa wamechanganyikiwa tu kimaisha.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!