Monday, 27 June 2016


Kuna baadhi ya wanao jihita waislam kwa makusudi kabisa na kwa malengo yao maalumu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwashawishi watu wawaunge mkono watu hawa.

Na matokeo yake vijana wengi wameishia kukamatwa na vyombo vya usalama na kuozea jela.

Watu hawa wapo sana kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram, Twitter n.k.

Baadhi ya watu huvaa ngozi za urafiki au uswahiba na watakuomba urafiki na wewe utawaongeza kwenye orodha ya watu utakaokuwa ukiwasiliana nao baada hapo wanajidai na kujionesha kuwa wao wana uchungu sana na Uislam na ni wanaharakati wa dini ya Kiislamu, haswa hizi zama za utumiaji wa mitandao.

Watataka kujuwa msimamo wako kuhusiana na harakati mbalimbali za Kiislamu na kisha wataanza kukushawishi kuhusiana na harakati za ISIS au Alshabab, lengo haswa ni kuwatafuta watu wanao waunga mkono Alshabab na ISIS.

Ukishawishika online na baadae wanaweza hata kuwasiliana na wewe kwenye simu na baada ya hapo watakushawishi mkutane sehemu.

Kwa nchi za Ulaya na Amerika, wanaweza hata kujidai kukutafutia nyenzo za kukuwezesha kufanya uharifu au kukutafutia safari ya kwenye Somalia au Syria.

Watu awa kumbe ni wanafiki kwa njia hii wanaweza kuwakomoa au kuwaangamiza wengine katika jamii kuonekana kama ni wasaliti.

Watakacho kifanya baada ya kukuingiza mkenge ni kukuuza kwenye vyombo vya usalama kisha unakamatwa na kukufungulia kesi ya ugahidi.

Haya mambo yanafanyika sana kwa nchi za Afrika Mashariki haswa Kenya na Tanzania wamesha anza kitambo hii tabia ya kuwaingiza mkenge vijana wengi na haswa walioko vyuo vikuu, vijana walio kwenye harakati za dawah na kadharika.

Kwa nchi hizi za Afrika Mashariki ni kutaka kuwaonyesha wahisani wao kuwa pesa walizowapa zinafanyakazi na ugaidi unashughulikiwa kama ipaswavyo.

Kwa nchi za Ulaya na Amerika lengo lao ni kutaka kuwaonyesha raiya zao ambao ndio walipa kodi kuwa janga la ugaidi ni la kweli na  walengwa ni wao dhidi ya Uislamu.

Baada ya hapo serikali zao zitakapokuwa zikipeleka majeshi kwenye nchi za Kislamu na haswa zenye mafuta na kuporomosha mabomu, kwa kisingizio cha kutafuta magaidi, kumbe lengo ni kuiba rasilimali haswa mafuta na kusiwe na kelele kutoka kwa raiya zao.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!