Friday 17 June 2016

NANYI MASHEKH NAFASI HII YA KUFUTURISHWA MMEITUMIA KUFIKISHA MALALAMIKO YA WAISLAMU?

Hivi karibuni tumeshuhudia na kusoma kwenye vyombo vya habari, kuwa Rais Jonh Pombe Magufuri, amewahalika viongozi wa dini na Madhehebu mbalimbali jijini Dar es Salaam, kama si nchi nzima, kwenda kufuturu Ikulu.

Naam, nao bila ya kujivunga, tukawaona kwenye picha za video wakiwa kwenye foleni ya chakula cha jioni, unashangaa kwa kuita chakula cha jioni, ndio ni chakula cha jioni, tatizo lako ni nini!?

Wacha nirudi kwenye mada yangu, nimeuliza swali la msingi kabisa kwa kuhoji tena kwa herufi kubwa, "MAGUFURI: PESA YA KUFUTURISHA UMEITOA WAPI?"

Kila mtu hapa atakumbuka kuwa tarehe 27 Novemba 2015, tulisoma taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutoka kwa aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue ikimesema kuwa "...afisa yeyote wa serikali anayepanga kuchapisha au kutengeneza kadi kama hizo anafaa kufanya hivyo "kwa gharama zake mwenyewe"

Yaani nina maanisha kuwa "Serikali ya Tanzania imepiga marufuku utengenezaji wa kadi za Krismasi na Mwaka Mpya kwa gharama ya serikali au pesa za umma."

Na tukapewa sababu za msingi kabisa kwamba 

"...Fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele

Lakini ajabu, tumeona Rais kwa Makusudi kabisa ametumia pesa za Walipa kodi, kuwanunua Masheikh chakula cha jioni, ndio nikauliza pesa kapata wapi?

Wengine wanaweza kujiuliza, kwani Waislamu hawalipi kodi? Jibu lake ni fupi tu, "WANALIPA" Lakini Waislamu sisi tulisha wahi kuilalamikia serikali kwa kuwapendelea Wakristo kwa kutumia pesa za serikali na kununulia kadi za Krisimasi na matumizi mengine ya kidini. Lakini leo ajabu tunaona tena kwa makusudi kabisa rais na waziri Mkuu wake wametumia pesa za walipa kodi wakiwemo Waislamu, Wakristo na Wapagani kuwanunulia Masheikh chakula cha jioni.

Kama kweli Rais Magufuri ulikuwa na niya njema, basi ungewaita watoto yatima na wazee wasio na uwezo wa kujikimu na kuwapatia njia mbadaya ya kuweza kujikumu na si hiwe zawadi ya Mwezi wa Ramadhani tu, bali wawezeshwe haswa ili kupunguza lindi la umasikini na si kuwaita Masheikh ambao wanao uwezo wa kujinunulia futari kwa mwaka mzima, ukawaacha masikini wakilala na njaa.

Swali kwa Masheikh, Je hii ndio HAKI Mlizokuwa mkizipigania na kuitaka serikali kututimizia sisi Waislamu!?

Je mlipokwenda uko Ikulu kula chakula cha jioni, mlimfikishia Rais malalamiko ya Waislamu ambayo kila leo kama si miaka na miaka wakiilalamikia serikali kwa dhulma kadhaa wa kadha?

Kuna mengi ambayo Waislamu wanailalamikia serikali kwa kutokuwa makini kwenye chaguzi zake za viongozi uko serikalini.

Waislamu wamekuwa wakitoa malalamiko yao mengi wanayofanyiwa na serikali tena kwa ushahidi wa dhahiri, lakini matokeo yake badala ya kuangalia na kuyafanyia kazi malalamiko yenyewe wanamfanyia kazi msemaji, wanamtukana, wanamkejeli ili aonekane mtu mbaya katika jamii, atengwe na adharauliwe.

Narudia tena swali langu kwa Mahseikh mliokwenda Ikulu kula chakula cha Jioni,

"...mlimfikishia Rais malalamiko ya Waislamu ambayo kila leo kama si miaka na miaka wakiilalamikia serikali kwa dhulma kadhaa wa kadha?"

Tumeshuhudia Masheikh wetu wakidhalilishwa, kukamatwa kama wahalifu na kupewa majina ya ajabu ajabu ilimradi wahalalishe ubaya kwao.

Kuna malalamiko ya unyama, udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahakamani jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Nawauliza nyie Masheikh mliokwenda kula chakula cha jionu kule Ikulu,

"...mlimfikishia Rais malalamiko ya Waislamu ambayo kila leo kama si miaka na miaka wakiilalamikia serikali kwa dhulma kadhaa wa kadha?"

Nawaomba Masheikh wetu wenye kujielewa, ni bora wawaelimisha na kuwashauri viongozi wetu hawa na wale watarajiwa, kuwa badala ya kuandaa "futari za kisiasa" zisizo na tija mbele ya MwenyeziMungu, wangepeleka huruma yao kwa akina mama, watoto na watu wazima wanaoteseka kwa vile waume zao na vijana wao wanaowategemea wapo ndani. Wapeleke "futari zao za kisasia" katika familia hizo.

Walio madarakani wakionyesha mfano huo, hapana shaka na waliotangaza nia watafuata nyayo. Na hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa familia za watuhumiwa hao, japo haitaondoa dhambi ya "kuwafunga" watu kwa tuhuma tu.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!