Wednesday, 9 November 2016

Unaweza kushanga kwa kusema kwangu neno Hongera kwa rais mpya wa Marekani Donald John Trump! Rais ambaye atakabidhiwa madaraka ya kuongoza taifa la Marekani ifikapo Tarehe 20th Januari 2017, na kuwa Rais wa 45 wa nchi ya Amerika.

Nimempa haki yake ya kumpongeza kwa kushinda kwake na kuchaguliwa kuwa rais Amerika kwa sababu kadhaa binafsi.

Sababu kubwa kabsia ya mimi kusema neno Hongera kwa sababu Donald John Trump amekuwa mkweli kwa yale anayo yaamini kuwa ni kweli na kwenye kampeni zake hakuwa mtu wa kuficha ficha kile anacho kiamini.

Wengi wetu tunamuona Donald John Trump kama mropokaji asiyejali kile anachokizungumza, lakini si kweli anajuwa nini alichokuwa anakizungumza na hakuwa mnafiki kuficha hisia zake kama walivyo marais wengine waliomtangulia akiwemo mpinzani wake Mwanamama Hillary Clinton.

Donald John Trump, amekuwa akitoa shutuma nyingi kuhusiana na mwenendo mzima wa kiulimwengu kuhusiana na makundi kadhaa ya watu, hakuwa akijali kama maneno yake kama yatakuumiza au lah, yeye alisema wazi bila mawaa.

Amekuwa akipinga wazi karibia vamizi zote za nchi za kiarabu, kuanzia Iraq na kule Libya, japokuwa kauli zake zimekuwa zina utata kama kweli alipinga vamizi zile au lah, lakini yote hayo anaonyesha kuwa labda kwa kuunga kwake mkono kulikuwa ni kwa sababu za kichama au shinikizo fulani.

Wengi wanasema kuwa anawapinga Waislamu, ndio anawapinga wale wenye kushirikiana na tawala ambazo wanatumika kuwadhuru wengine katika mambo kadhaa.

Ukiangalia historia utaona makundi kadhaa yanayopigana kwa jina la Jihadi, aidha yanapata ufadhili wa moja kwa moja kutoka shirika la kijasusi la Kimarekani CIA au kupitia njia za panya, kiasi cha kuuchafua Uislamu kuwa ni dini ya Umwagaji damu. Japokuwa makundi haya mengi hayaungwi mkono na Waislamu wengi, lakini chumvi kidogo uweza kuharibu radha ya chakula kilicho kingi.

Vilevile kuna swala zima la Wamarekani wenye asili ya Afrika, ambao yeye anaona kuwa wengi wao wamekuwa ni mzigo tu wa taifa kwa kukosa kwao mwelekeo wa maisha na ndio utaona jela nyingi za Marekani asilimia kubwa ni Wamarekani wenye asili ya Kiafika, ukilinganisha na idadi ya Wamarekani wenye asili ya nchi za ulaya.

Idadi ya Waamerika wenye asili ya kiafrika ni asilimia 13% ya idadi ya Wamarekani wote, walioko jela ni asilimia 37.6% ya Wafungwa wote ukilinganisha na Wamarekani wenye asili nyingize, japokuwa kuna asilimia 58.7% ya wafungwa wenye asili ya Kizungu, lakini ukichukuwa idadi ya raia weusi kwa idadi ya raia weupe kuwa na asilimia 37.6% ya wafungwa weusi ni kubwa sana kwa sababu Wamarekani wenye asili ya Kiafrika idadi yao kwa nchi nzima ni asilimia 13% tu wa Raia wote wa marekani na asilimia 77% ni Wamarekani weupe.

Wamarekani weusi licha ya idadi yao kuwa ndogo lakini ndio wanao ongoza kwa kuuliwa kwa ubishi au kwa jinahi, mfano mauwaji ya Wamarekani weusi jijini chicago asilimia 71% ni Wamarekani wenye asili ya Kiafrika.

Kwa nchi ya Kimarekani ili ni tatizo kwa sababu, kwanza imeshindwa kuwafanya awa wengine kuweza kujitegemea kiasi cha kutengeneza kundi kubwa sana la watu wasio na kazi na kuongezeka kwa jinahi nyingi zinazofanywa na Wamarekani weusi na wale wenye asili ya Kihispania pamoja na Kimexico.

Rais huyu anyetarajiwa hakuishia hapo tu, aliwasema hata viongozi na wafalme wanaotawala bara letu la Afrika na kutishia kuwa tunapaswa kutawaliwa upya kwa sababu Waafrika sisi hatuwezi kujitawala wenyewe na ni kweli. Japokuwa ukweli huu unauma sana kiasi cha kumuona huyu Donald John Trump ni Bepari anayetaka kurejesha ukoloni upya.

Huyu mtu amedhamilia kwenye kutekeleza ile kauri mbiu iliyoko kwenye pesa yao inayosema hivi... IN GOD WE TRUST. Unaweza kushangaa nchi ya Amerika kuandika maneno hayo kwenye pesa zao, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa maana ya maneno hayo ni IN Gold-Oil-Diamond WE TRUST.

Ni kwamba wao wanaamini popote kwenye Dhahabu, (GOLD), penye Petroli (OIL) na penye Almasi (DIAMOND) ndipo kwenye maslahi yao.

Kama nchi yoyote duniani haina maslahi na Amerika, basi na Amerika hana shida napo na hata kukitokea tatizo la kiutawala serikali ya Washingtoni haiangaiki wala kushtuka, lakini kwa nchi zenye rasilimali kama hivyo viwakilishi vitatu, yaani Dhahabu, (GOLD), Petroli (OIL) na Almasi (DIAMOND), basi rais yeyote ajae anatakiwa afanye juhudi kuvimilikisha kwa nchi ya Amerika.

Na sisi Waswahili tuna msemo wetu mmoja kuwa unasema hivi.. 'Bora adui umjuaye kuliko rafiki mnafiki' Kwa sababu ukiwa na rafiki mnafiki utaweza kujuwa kuwa ndio adui yako anaye kuangamizi kisirisiri, ila mtu kama Donald Trump, yeye yupo wazi, ukikasirika sawa ukinuna sawa, ila yeye atasema waziwazi lile lililoko kichwani kwake kukuhusu...!

Yawezekana safari hii Wamarekani nao wamempata Magufuli wao ambae amedhamilia kikweli kweli kupigania hali za Wamarekani...!

Kama uchaguzi wa Amerika ungekuwa unafata utaratibu wa idadi ya kura zilizoopigwa basi leo hii nchi ya Amerika ingeingia kwenye historia ya dunia kwa kuwa na rais wa kwanza Mwanamke Hilary Clinton.

Lakini Amerika wana utaratibu tofauti wa upigaji kura, wao wanaangalia idadi ya majimbo yalio kukubali na si idadi ya kura zilizopigwa.

Jambo ili pia liliwahi kutokea mwaka 2000 pale mgombea urais Al Gore kushinda kwa kuwa na kura nyingi za wananchi lakini akapoteza nafasi yake kwa kuwa na idadi ndogo ya majimbo yaliyo mchagua.

Sisi wengine na nchi zetu hatuna cha afadhali, yeyote atakaye tawala nchini Amerika, atakuwa pale kwa maslahi ya Wamarekani kwanza kabla ya sisi wengine wote.

Basi na tufanye subara kuona kitakachojiri kwenye utawala wake hapo atakapokabidhiwa rasmi madaraka ya Urais hapo Mwezi January tarehe 20 mwaka 2017

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!