Thursday, 10 November 2016

MAJIMBO KADHAA USA YAANDAMANA KUPINGA USHINDI WA TRUMP
Califonia wataka kujitenga na Amerika, CalExit

Maelfu ya waandamaji wameandamana leo kwenye miji mbalimbali ya Marekani kupinga ushindi wa Trump uku wakisema “Not my president," kwa maana ya “Si rais wangu," maeneo kadhaa kama vile Berkeley na Oakland wameonesha hasira zao dhidi ya mgombea urais aliyeshinda Donald J. Trump, maeneo mengine ambayo maandamano yamefanyika ni Pittsburgh, Seattle na Portland, Ore.

Miji mingine kama vile Pennsylvania mpaka California, Oregon na Washington State, mamia ya waandamaji wameonekana mitaani wakipinga kuchaguliwa kwake na wengine walipo hojiwa wamesema kuwa "That’s not my president". yaani "Huyu si rais wangu". na wakaongeza kwa kusema kuwa "Hatuwezi tu kukaa kimya na kumwachia awe rais mtu mbaguzi wa rangi na mbaguzi wa jinsia" Amenukuliwa kijana mmoja kwa jina la Adam Braver, mwenye umri wa miaka 22 anayesomea political science kwenye chuo kikuu cha California, (University of California). Na wanataka kujitenga na umoja huo wa majimbo ya Marekani na wameita harakati hiyo ya kutaka kujitenga kwa jina la 'Calexit'
"Ulimwengu mzima tunaonekana kuwa Wamarekani ni wabaya" amenukuliwa tena kijana mwanafunzi huyo akisema kwa hasira. na akamalizia kwa kusema kuwa "Huu ni mwanzo tu wa harakati za CalExit.

source:

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!