Friday, 30 June 2017

JE NA WEWE UNASUMBULIWA NA TATIZO LA UTEJA?

Unaweza kukataa kuwa wewe si TEJA, kwa sababu tu, umewahi kuwaona watu walio athirika na matumizi ya madawa ya kulevya haswa vijana, jinsi walivyo dhohofika.

Ukiwaangalia MATEJA WA MADAWA YA KULEVYA, wanapoyakosa kutumia madawa, mihili yao uingia kwenye taharuki na hofu inayoambatana na mbabaiko wa moyo kupaparika.

Wanakuwa ni wenye hasira na wakati mwingine wapo tayari hata kukwapua mali za watu ili wakanunue madawa hili watulizane na nafsi zao.

Lakini hata wewe na mimi, wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana tunaweza kujikuta tupo kwenye kundi la UTEJA ambao si rasmi, lakini limekuwa ni tatizo lililo wakumba watu wengi.

Waweza kukataa kuwa wewe si TEJA, sawa tunaweza kukubalia...

MASWALI YA KUJIULIZA...

1. Je Ulishawahi kupoteza SIMU yako au Kuhisahau Mahali?

2. Je, ile hali nawe haikukupata ya taharuki na hofu inayo ambatana na mbabaiko wa nafi/moyo kupaparika na kukosa raha kuliko pitiliza?

3. Je, simu zetu atupandi nazo vitandani na kuwa ndio ktu cha mwisho kukitumia kabla usingizi haujatupitia?

4. Je, ni mara ngapi umeamka saa nane za usiku na kitu cha kwanza ni kufungua simu yako na kuiangalia?

5. Je, ni mara ngapi umejikuta unaingia msalani, kisha ukakumbuka kuwa simu umeiwacha mezani ukairejea na kuingia nayo chooni.

6. Je, ni mara ngapi katika nusu saa umeifungua simu yako hata kama hakuna meseji iliyoingia?

7. Je, ukuwahi kupata wasiwasi labda simu mbovu kwa kuwa tu, saa nzima imepita bila meseji kuingia kwenye simu yako?

8. Ni mara ngapi umekuwa kwenye nyumba ya IBADA na kabla ya kuanza Kuswali, ukajikuta unaangalia kwanza simu kama kuna meseji?

9. Na ni mara ngapi umefungua simu yako mara tu baada ya kumaliza swala na kitu cha kwanza kikawa ni simu?

10. Je, waweza kukaa saa ishirini na nne (24) bila ya kuwa na simu yako?

11. Fikiria tena, kisha tafakari kwa kina ni mara ngapi umehisi kuikosa SIMU YAKO!

Kama hayo yamekukuta, basi ujuwe na wewe ni TEJA!

Kwa sababu SIMU nazo ni KASUMBA ya KIDIGITARI (Electronic Cocaine/Digital Heroin).

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!