Tuesday 27 June 2017

WABONGO WAISHIO UGHAIBUNI WACHONGEANA

Habari za kuaminika kutoka kwenye vyanzo vya uhakika, zinasema kuwa, Wabongo waishio nchi za Ughaibuni, kama vile Uingereza, Uholanzi, Italy, Ireland, USA na nchi zingine za Walami, wamekuwa na tabia za kuchongeana kwa maafisa wa Uhamiaji.

Mtoa habari huyo, amekielezea chombo chetu cha habari kisicho rasmi, ila yenye kuaminika kuwa, kumezuka tabia ya Wabongo ambao wamekwenda Ughaibuni Kimasomo au kikazi, kugeuka na kuwa mashushu wa serikali aidha ya Bongo au kujifanya kuwa wao ni mainfoma wasio rasmi wa immigration wa hizo nchi walizokwenda kusoma.

Mtonyaji wetu alipodukuliwa na kudadisiwa zaidi aliongeza kwa kusema kuwa, "Vijana wanaokwenda kusoma ughaibuni, ujikuta muda mwingine wana maisha magumu kwa kupenda zao starehe, sasa wanapokutana na Wabongo walioko uko muda mrefu na kupata Uraiya kwa namna zao, ndipo hapo sasa wivu unapovuka mipaka na kujikuta wanafanyakazi zisizo na malipo za kuwachongea wenzao".

Mtoaaji habari, ametaadharisha sana na kuwanasihi Wabongo wenzake, wawe waangalifu sana na urafiki wa kwenye mitandao haswa WhatsApp na Facebook, pia kujuana sana na Wabongo ambao kwa namna moja au nyingine ukaazi wao ni wa utata au una kikomo maalumu, haswa wanafunzi.

Mtoa habari akazidi kuhabarisha na kusema kuwa, "usione watu wanacheka na wewe au kujitia kukuchekea, lakini ndani ya nafsi zao wanaungua kwa hasira zisizo na sababu yoyote ya maana, kwa sababu labda una uraiya na yeye jinsi ya kuupata ni utata au basi tu wameamua kuwa na roho mbaya, kiasi waonekane wamezeeka kabla ya umri wao".

Nae Mwandishi wetu kwa kuliona jambo ilo kuwa si zuri haswa ukizingatia kuwa wanao chongeana wote ni Wabongo na kufanyiana fitna kwenye vyombo visivyo husika sio poa, akaingia chimbo na kugundua kesi kadhaa wa kadhaa ambazo zimewahi kutokea hivi karibuni.
Akagundua pia, kuna watu ambao tayari wana uraiya wa Ughaibuni lakini maafisa wa immigration, wamewaendea majumbani mwao na kuwahoji uhalali wa Wabongo hao kuishi kwenye nchi hizo.

Lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya raiya yoyote wa Bongo aliyepata uraiya wa nchi za Ughaibuni ambae uraiya wake wa Ughaibuni umetiliwa shaka, zaidi ya kuulizwa vitambulisho au documents maarufu kwa jna la pepa zenye kuhalalisha ukaazi wa nchi hizo.

Tafadhali, kama una habari au mtonyo wowote ule wa wambea hao, basi usisite kutuhabarisha, majina ya wambea hao, wapo wapi na wanafanya nini katika kuwaharibia wenzao, nasi tutwaweka hewani, ili waepukwe.

Waweza kuwasiliana na chimbo la habari kwa barua pepe: ChimboChimbo nasi tutawaweka wazi wambea hao wenye kupenda kuwaharibia wenzao.

Nikiripoti kutoka chimbo la kufukua mambo... Ndimi Mwandishi na Ripota wako, K.C.M.A
Kichaa Cha Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!