Thursday 12 March 2020


MAISHA YA UGHAIBUNI

YAMEINGIWA NA HOFU JUU YA HOFU.

Watu wamepata HOFU kubwa na Kuanza Kununua bidhaa kwa Wingi.
Ajabu ni kwamba, Karatasi za Chooni (Toilet Paper) ndizo zinaongoza kwa kununuliwa kwa wingi.
Mazungumzo na Fikra Nasaha

Nchi za Ulaya na Amerika ni nchi ambazo zimeingia katika hofu kubwa kutokana na tishio la virusi vya korona, kiasi ambacho cha kuhatarisha ukosefu wa baadhi ya bidhaa madukani (Panic Buy).

Hali hii inatokea aidha kwa kukosa taarifa za kutosha na kutegemea mitandao ya kijamii kupata taarifa ambazo si rasmi au kwa kuona kuwa janga ili linaweza kuchukuwa muda mrefu na kusababisha baadhi ya bidhaa kama si zote kuwa bidhaa adimu.
Hapo sasa ndipo raia wanapoingia katika hali ya hofu (Panic Mode), na kujikuta wakipapia bidhaa ambazo hata zingine hawazihitaji kwa wingi.

Ni kweli kuna haja ya kuchukuwa taadhari, lakini hizo taadhari zinapaswa zitokane na taarifa rasmi kutoka serikalini na si kama hivi inavyotokea.

Binadamu tumeingiwa na hofu kwa kuwa tu hatujui haswa kinacho endelea, labda kwa kuwa tu, ugonjwa huu, japo unatibika lakini kumekuwa na habari na picha za video nyingi mitandaoni, zikionyesha watu wakianguka, aidha kwa maradhi mengine au kwa virusi vya korona. Hakuna uhakika sana kwa kila kinachotumwa mitandaoni kikahakisi hali halisi ya mambo.
Lakini kwa kuwa wengi wetu ni watu wa kuamini kila kinachotumwa kwenye tovuti baraza, basi tunajikuta tunaingiwa na hofu ambayo si ya lazima.

Ni kweli taadhari zinachukuliwa, uku ughaibuni ninakoishi, kuna matangazo kila kona na haswa maeneno ya uduma za kijamii.
Hapa ofisini ninapofanyia kazi, kumewekwa taadhari kwa kila anayeingia ni lazima atumie Sanitaiza (sanitiser) kabla ya kuingia kwenye jengo na anapotoka nje. 
Sie tunao udumia watu na haswa uduma zinazo husisha ushikaji wa pesa, tunalazimika kuvaa soksi za mikono (Disposable Latex Gloves) na vizuizi vya mdomo.

Shule zinafungwa kwa wiki mbili na nusu, mikusanyiko ya watu imepigwa marufuku, kama vile maandamano, mikutano na mikusanyiko mingine ya kijamii.

Dawa za kusafishia mikono zimewekwa mpaka kwenye vyombo vya usafiri kama vile mabasi na treni na kila anaye abiri anapaswa kusafisha mikono kwa dawa hizo (sanitiser) ili kujikinga na kirusi cha korona.

Hayo madawa ya kusafishia mikono, vifuniko vya pua na mdomo (mask), zimekuwa bidhaa adimu kwa sasa na zikipatikana basi zinagombewa...
Uko kwenye maduka makubwa (Supermarket) vyakula vimeshaanza kuwa adimu, watu wananunua kwa wingi, dawa za watoto nazo zimekuwa za kugombea.

Watu wamekuwa na hofu kweli na hiyo Coronavirus, nakumbuka wiki hii, Jumatatu asubuhi, nimempeleka bint yangu shule, nipo ofisini kaja katibu muktasari wa shule anayosoma binti. 

Ananiletea taarifa kuwa binti katapika, ninahitajika nikamchukuwe na nirudi naye nyumbani niangalie hali yake. 

Nikatumia ujuzi wangu wa uduma ya kwanza. nikamfanyia uchunguzi wa haraka haraka, hakuwa na tatizo, yupo vizuri tu. Nikakumbuka asubuhi alikunywa maji mengi, nikajuwa ndio yalimchafua tumbo.

Hata hivyo mwalimu wake wa darasa akasisiza kuwa nirudi naye nyumbani, nami bila kipingamizi, nikaondoka naye. Lakini kabla ya kurudi nyumbani, nikapitia kazini kwangu, mana si mbali na anaposoma binti.

Sasa meneja wangu baada ya kusikia nimekwenda kumchukua mtoto, si nimemkuta mlangoni mkono mmoja kashika koti na mkono wa pili kakamata begi langu...!

Akanambia, Abu... I must send you home...!
Namuuliza why?
Akanambia... must take precautions because of this Coronavirus! akaendelea kuniambia kuwa nisijali, stiil you'll get paid. 
(Kanihakikishia kuwa nisijali kwa kuikosa hiyo siku nitalipwa tu, maan uku wengi tunalipwa kwa idadi ya saa unazofanyakazi).

Nikabakia 😨

Sikuwa na jinsi, nikajiondokea zangu home.

Nikajiuliza tu, hivi awa Korona wakihamua kuvamia nchi zetu za Kiafrika kama vile Tanzania, hali itakuwaje?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!