Sunday, 17 May 2015Assalamu Alaiykum wa rRahmatullah wa Barakatuh.

Kuna Maana Yoyote kwa Dua Kutojibiwa?

MwenyeziMungu Katika Quran, anasema wazi kabisa kuwa yeye anajibu sala na maombi ya waja wake wanapo muomba:

"Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka."(Qur’an 2: 186)

MwenyeziMungu anatujua vyema waja wake, na anajua tunayo yafanya na tunayo yawacha. Na Mwenyezi Mungu yupo karibu nasi sana anajua tunayo yaficha na tunayo yatangaza na tunayo yawacha. Hii ni dalili tosha kuwa Sala, dua na maombi yetu yanafika, kwa sababu yeye pekee ndiye anaye pokea hayo maombi. Tunachopaswa kufanya ni kuamini na kutii, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuongoka kwetu.

Katika ayah nyingine: " Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni..."(Qur’an 40:60).

Ayat hizo hapo juu, zinatuhakikishia kuwa MwenyeziMungu anajibu maombi ya wale wamuombao, kwa kila ombi liwe kubwa au dogo, kwa sauti au kwa kimoyomoyo, MwenyeziMungu amesha weka ahadi ya kujibu maombi yetu.

MwenyeziMungu ndiye mwenye kumiliki mambo yetu yote, nasi tukimuomba atatupa tu! Ila wale wanao takabari hata wakakataa kumuomba hao ndio wenye hasara maana siku ya hisabu wataingia Jahannamu wakiwa madhalili wanyonge.

Na ndio kuna wale wenye kuomba asubuhi na jioni, kuna wenye kukesha usiku kucha wakiomba na kuna ambao awana chochote wanachokiomba kwa MwenyeziMungu, ila wanatamani kupata iki na kile na yeye uwapa bila ya wao kufungua midomo au kuwazia jambo lolote la kheri.

Lakini mbona wakati mwingine MwenyeziMungu atupi kile tunacho kiomba kwake. Je tunakosea katika sala na dua zetu, kiasi cha MwenyeziMungu kutotupa tukiombacho?

Jibu lake ni "La hapana" MwenyeziMungu ajatunyima na wala hatotunyima kwa kila tukiombacho. Wala hatupaswi kuwa na huzuni au kukata tamaa kwa jambo ambalo tumeliomba na hatujalipata bado. Wala hatupaswi kufikiria kuwa MwenyeziMungu anatunyima, hapana.

Binadamu tumeumbwa hali ya kuwa tuna papara kwa kila tukitakacho, ni MwenyeziMungu pekee ndio mwenye kujuwa ghaibu kwa maana ya mambo yajayo.

Tunapo omba wengi tunatarajia kupata papo hapo au baada ya masiku machache tu, basi tuwe tayari tushajibiwa maombi yetu. Lakini tunasahahu kuwa MwenyeziMungu ndio mwenye kujuwa kila jambo litakalo sibu siku za mbele, vipi litakuwa na lile ambalo halitakuwa vipi lingekuwa kama lisinge kuwa na lile ambalo halikuwa vipi lingekuwa.

MwenyeziMungu anatuambia katika Qur’an:

"Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!" (Qur’an 89: 15-16).

Hayo ndio utujia kwenye bongo zetu mara tu tunapojaribiwa au kuhisi dua zetu hazija jibiwa.

Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya! Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!

Waislam tunapaswa kumshukuru MwenyeziMungu  kwa kila jambo, aidha kwa tunaloliona kuwa linatupendeza au linatuchukiza, kwa sababu hatujui hikma iliyoko kwenye jambo ilo.

Na kwanini tunasahau mambo mengi ambayo tunaruzukiwa bila ya sisi kuyaomba au tunahisi kuwa ni haki yetu na tunapoyakosa basi tunahisi kuwa tunadhurumiwa? Hakika MwenyeziMungu hamdhurumu mtu yoyote, bali sisi wenyewe binadamu ndio tunajidhurumu nafsi zetu kwa matendo yetu. Na subra zimetupitia mbali. MwenyeziMungu anatukumbusha kwenye Qur’an kwa kusema:

 Ila wale walio subiri wakatenda mema. Hao watapata msamaha na ujira mkubwa!" (Qur’an 22:11)

Basi tunapo omba tunapaswa kuwa na subira na hata kama tupo kwenye dhiki na mashaka makubwa, tunapaswa kuwa na subira na kushikamana katika kutenda mema aidha wakati wa faraji au shida. tukishikamana na hayo tumeahidiwa msamaha wa dhambi zetu, na pia tutapata ujira mkubwa kwa vitendo vyetu vizuri.

Kwa mujibu wa Mtume (saw), wakati mtu anapo muomba MwenyeziMungu, upata moja ya mambo matatu:

• Ombi lako ujibiwa mara moja, ukapata kile unacho kiomba, kwa namna ile ambayo MwenyeziMungu anaona inafaa.

• Majibu ya maombi yako uwekwa mpaka siku ya Hukumu, maombi yako yakawa ndio sababu ya kusamehewa dhambi zako.

• MwenyeziMungu uzuiya au kutokupa kile ukiombacho kwa sababu ya madhara yaliyoko (yaliyojificha) kwenye kile unacho kiomba.

Basi tunapaswa Kuomba kwa kutawasali dua zetu kwa kuziunganisha na vitendo vyema, ili iwe sababu ya kujibiwa dua mapema, aidha hapa duniani au siku ya hisabu.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!