Tuesday, 19 April 2016

Kwanini Wakati Mwingine Ngozi ya Mwili Uwasha Baada ya Kukoga


  • Kwanini tunakoga na sababu zinazotufanya tukoge
  • Kwanini unapomaliza kugoka baadhi ya watu uwashwa mwili na kusabaisha kujikuna?

Wengi ufikiria kuwa kukoga ni hali ya kujimwagia tu maji kisha basi, huyoo unajfuta maji na kuendelea na hamsini zako. Hapana, kukoga kuna hatua zake ambazo ukizifuata utajikuta unatakata na kuburudisha mwili wako na kuifanya ngozi yako kuwa yenye afya tele. Faida hii utaipata pale utakapozingatia mambo ambao unaweza kuyaona kuwa hayana msingi au ni mambo madogomadogo.

Kwa ufupi kukoga ni kuosha viungo vyote vya mwili, kuanzia kichwani mpaka nyayoni.

Kwanza  kabisa ni vema uwe umetayarisha baadhi ya vitu muhimu, kama vile sabuni ya kukogea, mafuta ya zeituni (olive oil) kama huna unaweza kutumia mafuta ya nazi yasio na harufu kali au mafuta yoyote yale kama vile baby oil, maji aidha ya vuguvugu au yaliopoa yasiwe ya baridi kiasi ya kushindwa kuyaoga, kitu ingine unaweza kutumia dodoki au spongi na jiwe la kusugulia miguu (si lazima).

Epuka sana kutumia sabani za manukato zenye harufu kali mara kwa mara kwa sababu wataalamu wa afya ya ngozi wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi kunachangia kutokea kwa mzio (allergy) pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi. Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.

Unapoanza kukoga kwanza kabisa hakikisha unajimwagia maji ili sehemu zote za mwili wako hakikisha maji yanafika kila kona ya mwili.

Hakikisha maji yanaingia katika nywele kwa kugusa ngozi ya kichwa na haswa kina dada ambao wanavaa nywele za bandia au waliosuka kwa kutumia viongezeo vya nywele. Hakikisha maji yanafika chini ya kwapa, masikioni, pembeni mwa sehemu za siri, katika vidole vya mguu na sehemu zozote nyingine za mwili zilizokuwa wepesi kusugua.

Kisha jipake sabuni yako mwili mzima, ukianzia kichwani na nyuma ya masikio, mikononi na kwenye makwapa, pia jitahidi kupaka sabuni nyuma ya mgongo, sehemu za siri na kushuka mpaka miguuni na kwenye nyayo.

Kisha chukua dodoki laki na kujisugua polepole kuanzia shingoni na kifuani, kutelemka mikononi na chini ya makwapa, kwenye tumbo na mgongoni kisha kuelekea chini kwenye viungo vya siri (Usitumie nguvu sana). Baada ya hapo unasugua miguu yako na kwenye nyayo unaweza kutumia jiwe la kusugulia kama huna basi waweza kutumia dodoki lako.

Baada ya kuhakikisha kuwa umejisugua vizuri, utajimwagia maji mwili mzima, hakikisha povu lote la sababu linaondoka mwilini, baada ya povu kuondoka mwilini kama unatumia bomba la kuogea unaweza kujisafisha na kujisugua taratibu kwa kutumia viganja vya mikono ili kuondoa mabaki ya ngozi laini (dead skin).

Ukisha maliza na kuhakikisha umetakata, kabla ya kujipangusa maji, jipake mafuta yako uliyoyatayarisha, hakikisha unajipaka mwili mzima, jipake mengi tu. Baada ya hapo unaweza kujimwagia tena maji uku ukijisugua taratibu kwa kuyasambaza yale mafuta ulojipaka.

Kisha unaweza kutoka na kujifuta kwa taulo kwa namna ya kukausha maji na si kwa kujisugua kiasi ya taulo kuondoka na mabaka mabaka. (Mabaka au weusi unao uona kwenye taulo si uchavu, bali ni ngozi mfu (dead skin) ambao kwa binadamu ni kitu cha kawaida na ipo kila siku.

Baada ya hapo ndio unaweza kujipaka mafuta yako kwa nchi za baridi unaweza kujipaka mafuta mazito na kwa nchi za joto ukiwa na lotion za mwili si vibaya kutumia.

KUWASHWA BAADA YA KUOGA

Zaidi ya kukogea sabuni zenye manukato makali kiasi ya kusababisha mwili kuwasha, tatizo jingine linalochangia mwili kuwasha wakati wa kuoga ni kutokutumia kiasi cha kutosha cha maji ya kunywa kila siku.

Hali hiyo inafanya mwili kuwa na upungufu wa maji na kuathiri vibaya afya ya ngozi na uwezo wake wa kuondosha sumu mwilini.
Ngozi isiyokuwa na afya njema inashindwa kutunza kiasi cha kutosha cha unyevu na kusababisha ukavu. Ngozi inapokuwa kavu husisimka kupita kiasi wakati wa kuoga na kusababisha muwasho.

Sababu ya mwili kuwasha baada ya kuoga ni kuishi katika hali ya msongo wa mawazo inayosababishwa na hofu, wasiwasi na sononi.

Tatizo jingine linalosisimua mwili na kusababisha muwasho wakati wa kuoga ni kujisugua kupita kiasi au kujisugua wakati wa kujifuta kwa taulo baada ya kuoga.

Kwa kawaida seli za ngozi zilizokufa, jasho na vumbi ndivyo vinasababisha mwili kuchafuka. Lakini uchafu huo huondoka mwilini tunapooga na nguvu nyingi hazihitajiki ili kuondosha uchafu na taka mwili juu ya ngozi. Matumizi ya nguvu nyingi na kusugua ngozi sana, husababisha madhara kwenye ngozi na kusababisha muwasho au ukavu wa ngozi kwa kuondosha mafuta yanayolinda usalama wa ngozi.

Watu wenye tatizo hili wanaweza kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuoga ili kupasha mwili joto au kupaka lotion ili kuifanya ngozi kuwa na unyevu na kupunguza hali ya ukavu wa ngozi.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu nyingine ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu, vumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini. Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho pindi mwili unapopata msisimuko, hali ambayo hujulikana kama mzio.

Kama hali ya kuwasha kwa mwili baada ya kuoga itaendelea basi unashauriwa kumuona daktari wa magonjwa ya ngozi kwa ushauri zaidi.

Ni matumain yangu utakuwa umefaidika na maelezo haya.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!