Thursday, 14 March 2019


Uchunguzi wa BBC Umebaini Matumizi ya Ugoro Ukeni

Baadhi ya wanawake kutoka mkoa wa Tabora nchini Tanzania wamekiri kuweka tumbaku katika sehemu zao za siri ili kupunguza hamu ya kufanya mapenzi (Jimai), huo ni uchunguzi uliofanywa na shirika la utangazaji la BBC.

Tabia hii ya wanawake kuweka Ugoro kwenye sehemu zao za siri umekuwa ni maarufu sana haswa kwa wanawake ambao hawaja olewa, wajane na wale walio olewa ila wanaishi mbali na waume zao.

Madaktari wameonya kwamba tabia hii ya wanawake kuweka ugoro sehemu za siri si salama kiafya na kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya kizazi na matatizo mengine ya kiafya (Hakuna utafiti rasmi kuthibitisha).

Wanawake wengi huko Tabora, ambao ni wajane, na wale ambao hawapo kwenye mahusiano au waume zao wapo mbali nao, wanatumia njia hii ili kupunguza hamu ya kufanya mapenzi.

Zaituni Shaban (mjane), anasema tangia mumewe kufariki, hajawahi kujisikia haja ya kupata mume mwingine.
"Naweka tu ugoro kwenye sehemu zangu za siri mara mbili kwa wiki. Hivi sasa, sina mpenzi wa kijinsia, na sijawahi kujisikia haja ya kuwa na mume, tangia kifo cha mume wangu miaka michache iliyopita," anasema Bi Shaban.
Mwanamke mwingine, Asha (sio jina lake halisi), anasema ameigeukia tumbaku "...na imeua kabisa hamu yangu ya jimai kwa sababu tangu nilipotelekezwa nikiwa mjamzito, sitaki kusikia chochote kutoka kwa wanaume na haswa swala la ngono".

"Ugoro unanitoshereza kabisa. Ninapotumia hamu yangu yote ya ngono hufa" alisema Asha.

Wanawake wengi wanasema mara nyingi wanachukua majani ya tumbaku ghafi, uyasaga na kuchanganya na mafuta ya Vaseline au Petroleum jelly na Magadi soda (au Majivu) ili kufanya mchanganyiko ywenye ufanisi.

Wanawake wengi walizungumza na BBC, walisema kwamba sehemu zao za siri uwasha kwa muda baada ya kutumia mchanganyiko huo.
"Mara nyingi mimi huweka tumbaku katika sehemu zangu za siri mara mbili kwa wiki. Inakaa huko kwa dakika chache kabla ya kuiondoa kwa kuosha. Baada ya hapo, huwa nasikia muwasho kwa muda na baada ya hapo hisia za kufanya mapenzi uniondoka. Hakuna madhara yoyote yatokanayo na mchanganyiko huu ninaoujua mimi..."anasema Zaituni Shaban.
Wanawake hao kwa ujumla wanasema kwamba tumbaku uwarizisha kwenye hisia za kufanya mapenzi.

Wanaume katika Kijiji cha Ugala huko Tabora walipo hojiwa walisema hawajui kwamba wanawake katika mkoa huo wanatumia tumbaku katika sehemu zao za siri.

"Nimesikia sana huu uvumi kuhusu hii tabia ya wanawake kutumia tumbaku, lakini nilipowauliza, mara nyingi wananiambia: Hiyo ni siri yetu," alisema Mzee Usantu, mwenyeji wa Kijiji cha Ugala.

Madaktari wanawaonya wanawake dhidi ya kutumia tumbaku katika sehemu zao za siri kwa sababu inaweza kusababisha kansa ya mlango wa uzazi.
"Hakuna utafiti thabiti uliofanywa ili kujua haswa madhara ya tumbaku katika sehemu za siri za mwanamke. Hata hivyo, wengi wa wagonjwa wetu wa saratani ya kizazi wanatoka mkoani Tabora, na tukiwauliza wengi wao wanakubali kuwa wamekua wakitumia tumbaku kuweka sehemu zao siri, japo mara moja katika maisha yao," anasema daktari mmoja ambaye alizungumza na BBC.
Source:
Pulselive

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!