Saturday, 6 January 2018

ULAJI WA MIHOGO MIBICHI

USABABISHA UHANITHI


• Mihogo Mibichi Usababisha Uhanithi.
• Ugonjwa wa Tezi Kwenye Shingo.
• Maumivu ya Tumbo na Kichwa.

Mihogo ni jamii ya mizizi na ni chakula kinacholiwa sana ulimwenguni, haswa nchi za Afrika, Ulaya na Amerika ya kusini.

Ulaji wa mihogo haswa kwa wakaazi wa Afrika Mashariki, umekuwa mkubwa sana, haswa miji ya Pwani ya Afrika Mashariki, kwa dhana kuwa ukila mihogo mibichi na ukichanganya na Karanga mbichi na Nazi, kunaongeza nguvu za kiume na wingi wa manii.

Dhana hii, imepelekea mpaka wafanyibiashara ndogondogo haswa kina mama, kutembeza mihogo mibichi na kuwauzia watu na haswa wanaume.

Licha ya faida mbalimbali ya ulaji wa mihogo lakini pia kuna hatari kubwa sana haswa mihogo inapoliwa mibichi.

Kwenye gram 100 ya kipande cha muhogo hutoa kalori 160, kunapatiakana Asilimi 60% Maji, Asilimia 38% wanga (carbohydrates), Asilimia 1% protini, 25% ya Thamani ya Kila siku (Daily Value) ya vitamini C. Muhogo uliopikwa umung’unywa vizuri tumboni kiasi cha zaidi ya asilimia 75%.

Faida zipo kadhaa, lakini si kwa ulaji wa mihogo mibichi, kwa sababu kwenye mihogo kunapatikana sumu inayojulikana kwa jina la Cyanide.

Sumu hii ya Cyanide [link] inapoingia kwenye mwili wa mtu usababisha madhara mengi, yakiwemo kutapika, kichefuchefu, kizunguzungu, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, ugonjwa wa Tezi kwenye shingo (goiters) na hata kupata ugonjwa wa kupooza unaojulikana kwa jina la KONZO na wakati mwingine kama mihogo mibichi italiwa kwa wingi huweza kusababisha hata kifo.

Watu wengi wanaweza kushaa kusikia kuwa ulaji wa mihogo mibichi inamadhara, ukweli ni kwamba, kwenye mihogo aidha ilio michungu au ile hisio michungu, aina zote za mihogo ina sumu (Cynade) sumu ambayo usababisha madhara mengi kama mihogo italiwa bila kupikwa.

Tatizo kubwa kabisa kwenye mihogo ni huu ugonjwa wa kupooza aina ya KONZO, ni ugonjwa unapatikana sana kwenye maeneo ambayo wakaazi wake wanakula sana mihogo na haswa kama italiwa ikiwa mibichi au kuto tayarishwa vizuri.

UGONJWA WA KONZO

Konzo ni ugonjwa unao athiri neva za mwili wa mlaji wa mihogo mibichi au hisiyo tayarishwa vizuri na kupelekea mlaji kupata ugonjwa wa kupooza kwa neva na kusababisha misuri kushindwa kuhimili mwili na uwezo wa kutembea kuwa wa tabu.

Ugonjwa huu kwa kuwa unaathiri neva za mwili, umfanya mgonjwa kushindwa kutembea vizuri kwa sababu misuri yake imekuwa dhaifu na inashindwa kuhimili uzito wa mwili, kiasi kupelekea maumivu kwenye misuri ya muathirika.

Neva zinapo athirika upelekea mtu kupooza na kupoteza hisia kwenye viungo mfano sehemu za uume/uke wa muhathirika na hii usababisha uhanithi (Uume Kushindwa Kusimama/kupoteza nguvu za kiume) kwa wanaume na kwa upande wa wanawake  kwa sababu ya kuathirika kwa neva zake za hisia na upelekea kukosa hamu na kushindwa kuhisi raha ya tendo la ndoa/jimai.

Wanaume wengi wanaopenda kula mihogo mibichi, wanakabiliwa na hatari ya kutoweza tendo la jimai aidha kwa kushindwa kusimama au kutoweza kuhisi na kulifurahia tendo la jimai.

Mihogo haipaswi kuliwa ikiwa mibichi, mihogo iliyo salama ni ile iliyopikwa vizuri na kuiva aidha kuchomwa, kukaangwa au kuchemshwa ndio huwa salama kuliwa.

Konzo Effect

Facts About Cyanide

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!