Monday, 13 February 2017


Hatuja sahau maneno yako, Misikiti na Madrassa kuwa Makanisa na Sunday School

Hivi karibuni kwenye ili sakala la kuwaita na kuwakamata aidha wale wanao tuhumiwa kuwa ni watumiaji na wauzaji wa madawa ya kulevya, mmoja kati ya hao walioitwa uko Kituo cha kati cha Polisi, alikuwa Josephat Gwajima.

Gwajima anajulikana na wafuasi wake kama Askofu Mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Duniani. Alipokamatwa na kutoka kwa dhamana, akahamua kuwaelezea wafuasi wake yale yaliyojili uko polisi.

Jambo moja alilolizungumza ni kuhusu watuhumiwa wengine, walioko mahabusi, yeye aliwataja kama Waislamu na Waarabu tena Wakurugenzi wa makampuni.

Na wapo uko kawaacha mahabusu na hawana wa kuwatetea eti kwa kuwa ni Waislamu kwa maana kuwa Uislamu wao ndio umewaponza.

Ukisikiliza hiyo audio na ukiwa na fikra za kiuonevu au za kiudhalili unaweza kusema kuwa aliyoyazungumza ni kweli. Lakini ukikaa na kutafakali kauli yake, utagundua tu kuwa lengo lake haswa ni kuwachochea Waislamu. Yaani anatengeneza ushawishi wa kisaikolojia dhidi ya Waislamu ili wapate kujihisi Udhalili (inferiority complex).

Na lengo lake ni kutaka kuwachochea Waislamu waonekane kuwa wanaonewa na hawana mtetezi...! Ili hali kila mtu anashuhudia kuwa kila alieitwa kituo cha polisi aidha kapewa dhamana kulingana na makosa yake na kuna ambao wamefikishwa mahakamani kulingana na makosa yake.

QUR'AN SURAT AL H'UJURAAT 49:6
Enyi mlio amini! Akikujieni fasiki (mpotovu) na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda

Hapa Waislamu tuna taadhalishwa na MwenyeziMUngu kuwa akitujia mtu ambaye yuko nje ya sharia ya MwenyeziMungu (si Muislamu) akatupatia habari yoyote, basi tuichunguze kwanza ili kujuwa undani wake na ukweli wake, kwa kuchelea tusije tukawaletea au kujiletea madhara, kwa kutojua hali yao. Hapo tena baada ya kwisha dhihiri kuwa hawana makosa tukaingia katika majuto ya daima, mkatamani yasingeli kuwa. 

Hao walioitwa uko Polisi ni Raiya kama raiya wengine tu na wala hawakuitwa kwa kuwa ni Waislamu au Wakristo au wapagani.
Walioitwa wengi ni waanga wa matumizi ya madawa ya kulevya na wengine wanahisiwa kuwa ni wauzaji, na wengi wao wamepatiwa dhamana kulingana na makosa yao au kwa Polisi kuendelea na uchunguzi...!

Gwajima ametawaliwa na chuki ndani ya nafsi yake, anaongea lakini ndani ya nafsi yake kunawaka moto dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Waislamu bado hatuja sahau zile kauli zake za chuki dhidi ya Uislamu, kipindi kile cha uchaguzi aliponukuliwa akisema kuwa...
"...ameota kuwa kuna siku nuru ya bwana (akimaanisha Yesu) itaangaza Tanzania Misikiti yote itavunjwa na kuwa Makanisa na Madrasa kuvunjwa kuwa Sunday school na Masheikh na Maimamu kukimbizana kwenda mbele ya msalaba wa Bwana Yesu Kristo"
Maneno haya ya Gwajima yakitazamwa kwa idadi ni machache sana, lakini kwa uzito wake ni mabaya tena yenye hatari kubwa kwa Waislamu na Taifa kwa ujumla.

Waislamu tuliyasikia matamko yale na kwa kuwa Waislamu tunajuwa kuwa anasumbuliwa na ile chuki ndani ya nafsi yake na Waislamu hatusumbuki na watu duni kama Gwajima.

Binafsi kama wewe ni Muuzaji wa Madawa ya kulevya nasema kuwa siwaonei huruma watu hao, wawe ni Waislamu au Wakristo au Wapagani au maarufu au mzuri wa sura kwa namna ya kipekee, as long yeye ameamua kuingia kwenye biashara ya kuuza madawa ya kulevya huyo ni adui yangu na kwa jamii nzima ya Watanzania na ulimwengu kwa ujumla.

Gwajima Kama hausiki na haya madude kwa namna moja au nyingine basi anafaidika nayo na kwa kusema maneno yale lengo lake ni kupoteza maboya ili aonekane ni mwema upande wa Waislamu na Watanzania kumbe ni mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo.

Lengo la mtu huyu ni kutafuta kusifiwa kuwa kajitoa muhanga kutetea jamii hisio na mtetezi, tukiwa na fikra hizi nchi hii itaendelea kuangamia kila upande.

Watanzania bado hatujapona kwenye lile gonjwa la kuwa na viongozi mafisadi, na tupo kwenye balaa la baadhi ya viongozi na raiya wachache wanakimbilia kuuza madawa ya kulevya ili kuangamiza walalahoi wenzao, halafu anatokea kiumbe duni mmoja kwa kutaka kwake sifa anataka kuwakoroga Waislamu kwa maneno yake ya kiubaguzi wa kidini, eti Waislamu hawana Mtetezi, alokwambia kuwa Waislamu hawana mtetezi nani, ilhali tayari sisi tunamuabudu Allah Subhanahu wa Ta'ala, ambaye ndio mlinzi na mwangalizi wa kila kiumbe!?

Hao wanao jihusisha na hayo madawa kama ikitokea kuwa ni Waislamu basi nao watakuwa wanakwenda kinyume na Uislamu kwa sababu kwenye Uislamu ulevi wa aina yoyote ule ni haramu.

QUR'AN SURAT BAQALA 2:219
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi MwenyeziMungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri.

Madawa ya kulevya yana madhara makubwa sana, kwa kuharibu siha na kupoteza akili na mali, na kuleta chuki na uadui baina ya watu. Japokuwa wauzaji wa hayo madawa pengine na watumiaji wanaona kuna manufaa, aidha kwa kupata fedha na kujipumbaza kwa watumiaji. Lakini madhara yake kwa jamii ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Mimi sioni sababu ya kuwaonea huruma kwa watu ambao wamekamatwa kwa kubeba madaya ya kulevya au kuuza, kwa sababu wanapelekea kuharibu nguvukazi ya taifa letu, ambalo linategemea vijana.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!