Sunday, 15 November 2015

NI NANI MMILIKI WA ISIS?

Vyombo vya habari vya kimagharibi, vimeshehena habari iliyotokea hivi karibuni uko paris Ufaransa. Kuna madai kuwa kundi la kigaidi la ISIS ndio lililo husika na shambulio ilo.

Watu wengi ambao si wafuatiliaji mambo kwa kina, kwa haraka kabisa bila kufikiria wanakubali kuwa hao wanaoitwa ISIS ni kundi la Kiislam ambalo lina lengo la kuweka utawala wa Kiislam uko Iraq na Sham (Syria).

Lakini wafuatiliaji wa matukio wamekwisha gundua zamani sana tangia siku ya kwanza kuwa kundi ili halina uhusiano wowote na Uislam, ispokuwa ni kundi ambalo lipo chini ya serikali hizo za kimagharibi likijificha chini ya kivuli (shadowy terrorist group).

Taarifa mbalimbali za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa nchi za Uingereza (UK) Amerika (USA), Ufaransa na baadhi ya nchi zilizo chini ya NATO, ndizo zenye kuwafadhili kwa hali na mali hao ISIS.

Matukio mengi ya Kigaidi yanayofanywa na ISIS ni matukio yaliyopangwa kwa ukamilifu kabisa na majasusi wanchi hizi zenye kuwafadhili watu awa na haswa wakiongozwa na kuratibiwa na Anglo-American Intelligence apparatus.

Malengo yao haswa ni kijiografia na kisiasa duniani kote kwa sababu nchi hizi hazitaki kuingia zenyewe waziwazi kwa kuogopa hasara na lawama za raiya zao.

Na ISIS wapo hapo wakiwakilisha uhalali wa nchi za kimagharibi ili wawape sababu za kuvamia nchi za Kiislam kwa kisingizio cha kuwatafuta ISIS.

Mnapaswa kujuwa kuwa hizi nchi haziwezi kuishi bila ya kuwa na adui atakayewapa sababu ya kuendelea kuchukuwa rasilimali za nchi wanazozitaka.

Ugaidi huu unaofanyika nchi za mashariki ya kati na nch za ulaya ni biashara na kazi ya mikono ya hayo mataifa kwa malengo yao maalum.

Tafadhali angalia makala na viungo vya tovuti kwa lugha ya Kiingereza kwa habari zaidi juu ya asili ya ISIS:

>> Bonyeza HAPA

>> Bonyeza HAPA


Maelezo na hizo tovuti pamoja na hiyo video hapo juu ni ushahidi wa kutosha kuhitimisha kwamba mashambulizi Paris ni mashambulizi uongo (false flag attacks), kwa lengo la kujipatia uhalali wa kuendelea kuzishambulia nchi zenye Waislam wengi na wakati huo huo kuwapa wakati mgumu Waislam wanaoishi nchi za Ulaya na Marekani.

Swali dogo tu, Urusi ilipoamua kutuma mabomu ya masafa ya mbali, nchi za Uingereza na Marekani zilikuja juu kwa sababu wanaogopa mipango yao kutofanikiwa.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!