Monday, 22 February 2016

Lengo ni kuanzisha nchi itakayoitwa “The Great Israel”

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa Uzayuni Theodor Herzl, eneo ambalo Wayahudi wanataka kutawala ni kuanzia kijito kilichoko nchini Misri mpaka mto Eufrati (Euphrates) na "Kwa mujibu wa Rabbi Fischmann," Nchi ya Ahadi ni kutoka Mto wa Misri hadi Eufrati, na kuendelea mpaka Syria na Lebanon."

Unaweza kushangaa na kujiuliza mara mbili mbili na hata kuchukua uwamuzi wa kupinga bila ya kutafakari kwa undani.

Haya yote yanathibitishwa na Maneno ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pale alopowatetea ISIS na kuwaambia wakaazi wa milima ya Golan wenye imani ya dini ya Druze uku akila kiapo cha kuwaadhibu watu hawa kwa kuwashambulia wanamgambo wa ISIS ambao walikuwa wamejeruiwa na wakiwa njiani kupelekwa hospitali nchini Israel kwa matibabu.

Benjamin Netanyahu alinukuliwa akisema kwamba hakuna mtu yoyote atakaye vumiliwa au hata kuruhusiwa kujichukua sheria mikononi kwa kuwashambulia askari wa Kiisrael walioko kwenye kundi la ISIS, kundi ilo au watu hao hawatavumiliwa kamwe. Na Serikali yake itawatafuta wakazi hao  wa Syria wanao pigana dhidi ya wanamgambo ISIS.

Wakati unajiuliza maswali unapaswa ujiulize pia, hivi vita vinavyoendelea mashariki ya kati malengo yake ni nini? Na kwa nini viongozi wanapoondolewa madarakani hakuna juhudi zozote za kimataifa kusaidia hizo nchi ili ziweze kusimama zenyewe kiutawala kama mwanzo?

Utakapokosa jibu basi ndio tuangalie historia ya Kizayuni na vita vinavyopiganwa dhidi ya Iraq, 2006 vita dhidi ya Lebanon, 2011 vita dhidi ya Libya chni ya Gadafi na vita inayoendelea nchini  Syria na hata Iraq hivi sasa na vita vya Yemen, vilevile mchakato mzima wa mabadiliko ya serikali nchini Misri. 

Haya yote hayakuja kwa bahati nasibu, ni mipango ya muda mrefu sana wa viongozi wa Kizayuni wakisaidiwa na serikali ya Marekani na nchi za Ulaya ili waweze kujitanua na kuwa taifa kubwa kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati.


Kinachofanyika sasa ni kuzidhoofisha nchi zilizoko Mashariki ya kati na hatimaye kuziondolea uwezo wa kujilinda haswa nchi jirani na Israel (nchi za Kiarabu) kama sehemu ya upanuzi wa mpango mzima wa Israel ili kupata nchi itakayoitwa " The Great Israel - Israeli kuu" na haya yameshaanza kutoka Bonde lamto  Nile mpaka Efrati.

Mpango huu ni pamoja na kuwakimbiza wakazi wa miji ya Syria ili kupatikane nafasi kubwa kwa walowezi wa kiyahudi. Vilevile kupatikane eneo jipya kwa Wapalestina, maana hata wao wataondolewa uko Palestina na kupelekwa kwenye makazi mapya yatakayoamuliwa baadae. Na hii inahusisha miji ya West Bank na ukanda wa Gaza vyote hivi vitakuwa ndani ya nchi itakayoitwa The Great Israel.

Unaweza kujiuliza labda mambo haya ni ndoto tu, la hasha, kinachoendelea sasa ni kutimiza utabili ulioko kwenye vitabu vyao na haswa maelezo yaliko kwenye kitabu cha Mwanzo, Kumbukumbu la Torati, Hesabu na Ezekiel.

Mwanzo 15: 18-21

Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai, na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

Vilevile ukisoma kwenye Kumbukumbu la Torati 1: 7, 

Geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.

Kumbukumbu 11:24

Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.

Vilevile waweza kupitia kwenye mistari hii Hesabu 34: 1-15 na Ezekiel 47: 13-20

Maeneo hayo yaliotajwa kwenye mistari hiyo hapo juu yanahusisha nchi ya Palestina, Lebanon, Syria, Jordan, Iraq, baadhi ya maeneo ya Kuwait, Saudi Arabia, U.A.E, Oman, Yemen, mpaka nchi ya Uturuki.

Angalia Ramani hapa chini:


Kwa mujibu wa makala ya kiutafiti ya Global Research iliyoandikwa na Mahdi Darius Nazemroaya mwaka 2011, lengo ni kuendelea kujipanua kwa Israel kama ilivyokuwa imepangwa na dhidi ya nchi za Mashariki ya Kati.

[The Yinon plan] ni mpango na mkakati wa kuhakikisha Israel inakuwa superpower kwenye ukanda wa mashariki ya kati.

Maelezo yalioko kwenye mpango huo inasema kuwa Israel lazima ipange upya au kuanzisha nchi mpya kisiasa (geo-political environment) na kuwa na mazingira ya kisiasa yajulikanayo kama balkanization yaani kuzifanya nchi jirani haswa za nchi za Kiarabu katika majimbo vijinchi vidogo vlivyo dhaifu.

Wana mikakati wa Kiyahudi wanaitazama Iraq kama changamoto kubwa kwao haswa  kimkakati. Na hii ndio ikapelekea kwanza Kumuondoa Sadam Hussein nchini Iraq na kisha ndio kitakuwa kitovu cha harakati zote za uhasi mashariki ya kati. Na baada ya hapo Iraq inapaswa kugawanywa vipande vipande kama ilivyo kwenye mkakati wa Yinon Plan.

Na sasa kumetolewa wito na serikali ya Israel kuigawa Iraq mafungu matatu, kuwe na nchi ya Wakurdi (Kurdish state) na nchi mbili zingine moja kwa ajili ya Waislamu wa Kishia na nyingine kwa ajili ya Waislamu wa Sunni.

Hatua ya kwanza ni kuanzisha vita kati ya nchi mbili yaan Iraq na Iran, kama ilivyojadiliwa kwenye mpango wa Yinon (Plan Yinon) na ilo jambo lipo mbioni kukamilika hivi karibuni.
--

References:

Video Links

• ISIS In Greater Israel's Scheme

• The Plan -- according to U.S. General Wesley Clark (Ret.)
 

Website links

http://realitieswatch.com/netanyahu-admits-isis-are-israeli-soldiers/








0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!