Thursday, 3 March 2016

Tunazibembenda akili zetu kwa makusudi!

Nasaha za Kichaa, Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa

Kwa wenye akili wengi wanaweza kushangaa na kichwa cha bandiko ili, watashangaa zaidi pale watakapo gundua kuwa mwandishi wake ni Mimi Mwendawazimu Kichaa aliyechanganyikiwa, Maana ukiwa na akili za Kichaa aliye changanyikiwa kama mimi, uoni tabu kuongea kile kilicho moyoni mwako kwa namna ambayo kichaa chako na uwendawazimu wako unavyo kutuma.

Kama wewe ni mmoja wapo wa wenye akili, usishangae na kichwa cha habari hapo juu, kwa sababu kimeandikwa na Kichaa Mwenye Wazimu. 

Jambo moja unalotakiwa kufanya ni kutafakari kidogo ndipo utagundua kuwa neno baleghe lina maana ya kukomaa aidha kimwili (biologically) au ukomavu wa kiakili (intellectual maturity) na hata kiroho (spiritual).

Kama ilivyo kuwa na umuhimu wa mwili kubaleghe kimwili (Kibailojia) vilevile kuna umuhimu kwa binadamu na haswa vijana Kubaleghe kiakili kwa sababu ni kitu muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya kijamii. Vijana wengi tuna baleghe ya kimwili tu, huku tukikosa baleghe ya kiakili, na kiroho.

Ukosefu wa baleghe ya kiakili ni janga la kwanza kabisa kwa vijana wetu!

Kwa Kukosa baleghe ya Kiakili na Kiroho, ndiko kunako pelekea wengi wetu kukosa kuhishimiana katika majadiliano yetu na haswa tunapotumia mitandao ya kijamii.

Kuto kukomaa huku kunaletwa na kuzibemenda akili zetu na kuathili mioyo yetu kiasi cha kutoweza kuona thamani ya majadiliano yetu na kuhishimiana kwetu.

Tunacho angalia ni kuwa nimemshinda fulani, nimekuwa maarufu kwa kumtukana fulani au kwa kuwakufurisha watu fulani au kwa kuwashusha thamani kina fulani.

Tumeamua kwa makusudi kabisa kuzibemenda akili zetu na hatukubali mtu yoyote mwenye mawazo yanakwenda tofauti na yetu, kiasi cha kuwa vipofu wa akili kwa kushindwa kuona au kutambua kuwa binadamu tuna uwezo tofauti katika kuyakabili mambo mbalimbali katika jamii inayotuzunguka.

Wenye akili mnashindwa kuelewa kuwa, sisi WendaWazimu na Vichaa tulio changanyikiwa, ndio watu pekee ambao tunaruhusiwa kuto tumia akili zetu, kwa nyinyi mlio na akili kwa kuto tumia akili zenu ni kutunyang'anya haki yetu ya msingi kwa sababu sisi ni vichaa na zaidi ya hapo tumechanganyikiwa.

Ajabu ya nyinyi ambao mna akili, hamkubali tena kujifunza kutoka kwa wenzenu wenye akili kama nyinyi au wenye mitazamo tofauti na yenu, hamzisomi tena hoja zao, hata kama zina ukweli au hazina ukweli. Mnacho kiangalia ni kile ambacho mnakiona kuwa ni sawa kwa akili zenu na hata kama si sawa mnakibeba tu hivyo hivyo kama kilivyo, hamjali tena, mnacho kijali ni kitu kimoja tu, kuwa maarufu hata kwa kupinga ukweli ambao kila kukicha mnaukimbia.

Siku mtakapokubali kuwasikilia wale mnao waona kuwa ni maasimu wenu, ndipo mtakapo gundua kuwa wale ambao mkiwaona kuwa ni maasimu wetu kumbe ni ndugu, jamaa na marafiki zenu na wanacho kieleza aidha kina manufaa na ukweli ndani yake au tofauti yenu ni ndogo sana na si tofauti ya kuwafanya muwachukie na kuwaona kuwa ni maadui zenu.

Ikiwa kwa sababu ya upuuzi wenu hamutaweza kuona sura zenu hasa katika kioo cha vitendo vyenu, mtakuwa mmefanya kosa kubwa lisilosameheka. Kabla ya lolote lile, ni wajibu kwenu kwanza kuzichungua hali zenu za kiroho na kuziona waziwazi sura zenu za ndani, ili mweze kuzitambua aibu zilizoota mizizi na kustawi katika dhamiri zenu bila ya nyinyi wenyewe kufahamu. 

Na nyinyi wenyewe ndio mnaoweza kuikata mizizi ya sifa mbaya katika nafsi zenu kwa kufanya uchunguzi na jitihada, na kuzizuia (nafsi) zisidhihirishe ubaya wake katika mazingira ya maisha yenu.

Hakika mmeshafanya makosa na mnaendelea kufanya makosa, mnajitenga na tabia za Kiislam na mnatufundisha sisi wendawazimu mambo mabaya na hata kwa vizazi vyetu na vyenu nyie wenye akili kwa maana ya watoto zetu sote.

Hakika tunakitenga kizazi na Uislam. Hawakukosea wale waliosema: "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."

Na kwa kweli wanatusoma kwa haya tunayo yaandika kwenye mitandao.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!