Unaweza kushangaa na kichwa cha habari hapo juu, ndio hata mimi ningeshangaa kwa muda, kisha ningetafakari neno ilo... "KWA NINI TUWACHANGIE FUTARI!?"
Nimeanza kwa kuuliza kwa makusudi ili kuvuta umakini wa msomaji ili kumuwezesha kutafakari vema kila anacho kitoa mwezi huu.
Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kuchuma kheri nyingi nasisi kila mmoja wetu anatamani na kutarajia kile atakacho kitoa mwezi huu, kitampatia thawabu nyingi kutoka kwa Mola wake.
Na ndio maana Mwezi wa Ramadhani kunakuwa na Matangazo mengi ya kuomba sadaka haswa za kufuturisha wale wasio na uwezo wa kupata futari.
Kwa kweli ni jambo jema sana kuwakumbuka mafukara na masikini, wakiwemo watoto yatima, wajane na wazee na hata wasiona uwezo wa kujikimu.
Lakini jambo ili zuri kwa bahati mbaya huisha pale tu, tunapomaliza kusheherekea Iydul Fitry kisha hatuwakumbuki tena mpaka Ramadhani ya mwakani.
Ninachotaka kukisema ni kwamba kwa hali hii kubwa ya kuwasaidia wale wenye kuhitaji na jinsi tunavyoishi na kukaa nao vema kwenye mwezi huu wa Ramadhani basi hata mwezi huu utakapoisha, tunapaswa kuishi nao kwa namna hii hii tunavyoishi nao kwa wema kwa sababu hao tunao waangaikia na kuwatafutia hata hiyo miezi mingine kumi na moja watakuwa ni wahitaji na tusisubiri waje kutugongea milango kutuomba, bali tuwagongee milango na kuwapa kwa kile kilicho ndani ya uwezo wetu na si kinyume chake.
Kwenye nakala yangu moja niliandika maneno haya hapa chini:
"Kwa kifupi maisha haya tunayoishi mwezi huu wa Ramadhani ndio hivi tunavyopaswa kuishi hata miezi Mingine kwa kutekeleza yale yote yanayomfurahisha MwenyeziMungu (swt); na tujiepushe kabisa na yote yasiyompendeza Allah (swt)."
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?