Thursday 25 August 2016

SWALI KWA MAHUJAJI WETU

Niliuliza ili swali wengi wakajalibu kujibu kwa majibu mbalimbali, wapo waliosema tutaletewa Kofia, wapo waliosema tutalewa maji ya zamzam nakadhalika nakadhalika.

Japokuwa swali liliwahusu mahujaji wetu lakini haikuwa vibaya kwa wengine kujaribu kuchemsha akili zao na kujaribu kujibu swali lile.

Kiukweli kabisa nimewalenga ndugu zetu mahujaji, kwa sababu wao ndio waliobahatika kuitwa kwenye nyumba tukufu hapa duniani, wakiwa uko kwenye hija watatembelea miji miwili mitukufu, Makkah na Madina. Miji ambayo kila moyo wa Muislamu unatamani siku moja kuitikia wito huo ulio mtukufu.

Nimeharakisha kuwauliza kabla wengi wao hawajapanda ndee kuelekea uko, ili wasije kusema kuwa hatukuwahi kuwaagiza chochote kitu.

Zawadi ninazo ziulizia mimi si hizi zawadi zitakazo kwisha na kuchaka na kuchoka. Tukiletewa Kofia, tasbihi, Uturi au miswala na maji ya zamazam, vitakwisha na kuchakaa na tutasahau kama tuliletewa zawadi.

Hizi ni zawadi ambazo faida yake kwa jamii ni kwa mtu moja mmoja, zawadi ninazo ziulizia kwa mahujaji watuletee ni  zile ambazo hazitachakaa na kwisha. Ni zawadi ambazo zitaleta uhai na matumaini katika nyoyo zetu waislamu kwa ujumla.

Nawakumbusha kuwa wakiwa uko kwenye ibada tukufu wajifunze na wakija uku kwetu wawe walimu kwetu sisi ambao hatukubahatika kuitwa kwenye wito huo wa hija.

Tutafurahi na kufarijika watakapo tuletea wema na utii wa AbiBakr Sidiq (ra) [Abdullah ibn Abi Quhaafah]. Bila kusahau uadilifu wa Umar ibn Al-Khattab (ra). Pamoja na maadili na ukarimu wa Uthman ibn Affan (ra). Bila kusahau ujasiri na ushujaa wa Ali ibn Abi-Talib (ra).

Hizo ndio zawadi ninazoziomba watuletee ndugu zao ambao hatukubahatika kuwepo kwenye wito huo mtukufu kabisa. 

Mtakaporejea mje mkiwa na hamasa kama zama za Mtume (saw) kutoka nyoyoni mwenu kuupa Ulimwengu wa Kiislamu ambao kwa sasa unakabiliwa na shida nyingi na maumivu yasiokwisha!

Msiseme kuwa hatukuwakumbusha, kwa sababu safari hii hatujachelewa wala nyinyi hamjachelewa, mtakaporudi salama tuna ahidi kuwa nasi tutazipokea tunu hizo kwa mikono miwili, kwa sababu ndizo zawadi na tunu pekee zitakazobadili mustakabari mzima wa maisha yetu katika dunia hii tunayopita tu.

Hatuhitaji tena Kofia, tasbihi, Uturi au miswala na maji ya zamazam kwa sabau vitakwisha na kuchakaa, japokuwa mkituletea vitu hivyo hatuta vikataa, tutavipokea na kuwashukuru, lakini mnapaswa kukumbuka jambo ili moja...

Msije sema kuwa hatuja wakumbusha...!

KUTULETA ZAWADI KUTOKA HIJJA.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!