Wednesday, 28 September 2016

STAIRWAY TO HEAVEN (NJIA YA MBINGUNI)

Ile Sanamu ambayo inaonyesha Muislam yupo chini amesujudu kisha anafata padri wa kikatoliki alafu Myahudi, iliwekwa kwenye maonyesho mjini Madrid mwaka 2010 na ikapewa jina la "Njia ya mbiguni" (Stairway to Heaven).

Lakini sanamu lile baada ya kuonyeshwa ilileta utata mkubwa mpaka msanii aliyeitengeneza mwenye asili ya Uhispania Eugenio Merino, alipojitetea kwa kusema kuwa, kazi yake haikuwa na lengo la kudhalilisha dini yoyote ile, bali ni kuonyesha mshikamano wa dini tatu, pamoja katika jitihada za pamoja za kumfikia Mungu, na watu wasifikirie vibaya.

Lakini ukiangalia kwa karibu, utaona kwamba kwenye hayo masanamu matatu kuna vitabu vya dini tatu vikiwa vimewekwa tofauti na imani ya kila sanamu.

Hapo Myahudi utaona anaomba kwa kutumia Qur'an, Mkristo amekamata Torati na Muslim pembeni yake kuna Biblia.

Sanamu hizo zililalamikiwa na wengi wakiwemo Wayahudi wenyewe, Wakristo na Waislamu, kwa sababu inasemekana kuna maana zaidi ya hiyo iliyojificha, ukizingatia kuwa msanii ni kutoka Uhispania, na nchi hiyo iliwahi kutawaliwa na Uislamu kwa kipindi kirefu.

Wapo wanaosema kwamba dhamira ni kudharirisha Uislamu ndio maana sanamu inayo muwakilisha Muislamu ikawekwa chini, na ni sawa na kusema kuwa Waislamu wamelala na anapaswa kunyanyuka ili hao walio juu wote wanyanyuke.

Ila kuna wanaosema kuwa hapo si kudharirisha Uislamu, bali ni kuonyesha kuwa Uislamu ndio msingi wa dini zote na ndio nguzo ambayo dini zingine zimeegemea hapo na siku nguzo ikitikisika tu, basi dini zingine zote zitadondoka na ndio maana Myahudi aliyeoko juu kakamata akiomba kwa kutumia Qur'an kwa sababu anajuwa manufaa yake.

Padre wa kikatoliki aliye katikati uku akiwa ameshika Taurati amefumba macho akiomba huyo wa chini asitingishike wala kunyanyuka na huyo wa juu aendelee kuomba ili kuweka mambo sawa.

Japokuwa tafasiri zinaweza kutofautiana kulingana na mazingira na uoni wa mtu, lakini tunaweza kujiuliza na sisi ni vipi Myahudi awe kakamata Qur'an, Padri wa kikatoliki awe kakamata Tourati na Muislam kasujudu na pembeni yake kuna biblia?

Sanamu ya "Njia ya mbiguni" (Stairway to Heaven) iliuzwa kwa €45,000 (Euro) kwa raiya wa Ubelgiji mwenye asili ya Kiyahudi.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!