MATOKEO YA MITIHANI YA SHULE
TUZIKUMBUKE NA NAFSI ZETU.
Tusijisahau na sisi Matokeo yetu Uko Akhera
Leo wengi tumeshughulishwa na kutaka kujuwa matokeo ya vijana wetu wa darasa la kumi na mbili (12) yaani form four.
Kwa wale ambao wamefanya vizuri ni furaha kwao na kwa wazazi wao, ndugu, jamaa na marafiki.
Na kwa wale ambao hawakufanya vizuri ni uzuni kwao na kwa wazazi wao, ndugu, jamaa na marafiki.
Lakini furaha hii na uzuni hizo athali yake ni hapa hapa duniani tu na ni ya muda tu, waliofaulu na wasio faulu wanaweza kufanikiwa kimaisha uko mbeleni au kutofanikiwa kwa sababu bado watakabiliwa na mitihani mingine aidha ya kimasomo au ya kimaisha.
Juhudi zao ndizo zinaweza kuwa sababu ya wao kufaulu tena na hata wale ambao hawakufanya vizuri wanaweza kujikuta wanafanya vizuri na kupata furaha waliyoikosa uko nyuma.
Hali hii inahakisi maisha halisi ya Muislamu na binadamu wote kiujumla, jinsi tunavyoishi na kukabiliana na changamoto za kila siku katika maisha yetu ndio mitihani yetu ya kidunia, aidha tunaimudu au tutaishindwa kuimudu, yote hayo ni juhudi zetu na wakati huo huo tukitegemea rehma za Muumba wetu katika maisha yetu ya kila siku.
Tukiweza kufata vema mwongozo aliotuachia Mtume Muhammad (salla Allahu 'alayhi wa-sallam) na kuambatana nao kidhati kabisa, basi nafasi ya sisi kufaulu na kupelekea furaha ni kubwa sana, lakini tukiwacha Qur'an na Hadith na kufata matamanio yetu, basi tutakuwa kama wale ambao leo hii kila wakiangalia mbao za matangazo ya matokeo ya mitihani wanatingisha vichwa na kuuma vidole vyao kwa kuona kuwa hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Uzuri wa mitihani hii ya shule, kuna kurudia mitihani, kuna kuendelea na shule za kulipia na unaweza kujikuta unafanya vizuri tena na kuwa na furaha kama ile waliokuwa nao wengine.
Swali la kujiuliza Muislamu, ni vipi ikifika siku ya Malipo na ukajikuta unapokea matokeo yako ya mitihani kwa mkono wa shoto kwa maana kitabu chako kinaonyesha mapato ya matendo yako ni hasi (Negative)?
Uko hakuna kurudia mitihani wala kwenda kwenye shule za binafsi za kulipia, hapo ni mawili tu, umefanya jitihada na kwa rehma zake Allah akakuingiza kwenye pepo yake na uko ndiko kufaulu haswa, au ukajikuta ukuweza kufaulu na ukaelekezwa kwenye moto wa jahanam kuwa ndio makazi yako na uko ndio kufeli kikwelikweli maana hakuna kukata rufaa wala kurudia mitihani.
QUR'AN SURAT MUH'AMMAD 47:15
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?
QUR'AN SURAT AL-GHAASHIYAH 88:1-4
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? Siku hiyo nyuso zitainama, Zikifanya kazi, nazo taabani. Ziingie katika Moto unao waka.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?