Sunday, 2 July 2017

TUSIHISHIE KULALAMIKA TU,
TUFANYE KAMPENI KUMUELIMISHA

Kampeni Wacha Ngono, Zingatia Masomo.

Tangia Rais Magufuli, kutoa tamko/katazo la kuto waruhusu watoto wa kike kutokubaliwa kwenye shule za serikali (Msingi na Sekondari) pindi wapatapo ujauzito, wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakilalamika kuwa tamko ilo, litamsababishia msichana huyo kukosa elimu ambayo ndio msingi wa maisha na kusababisha kuharibikiwa kimaisha.

Mengi yamezungumzwa na kampeni bado zinaendelea kupinga tamko lile.

Lakini ajabu sana kwa wanaharakati wetu hawa, sina uhakika kama wanafanya makusudi au bahati mbaya au kutokuwa na ufahamu au kutokuwa na mipango endelevu katika kadhia hii.

Wamekuwa wakinukuu misemo mbalimbali na kuna msemo mmoja maarufu, usemao kuwa "Kumuelimisha Mwanamke, ni Kuielimisha jamii".
Ni kweli lakin pia wasisahau kuwa "Kuharibika kwa mtoto wa Kike kwa kupata ujauzito akiwa bado mwanafunzi ni kuharibika kwa jamii"

Kwa sababu mimba nyingi za watoto wa shule zimekuwa zikikosa huduma ya baba, kwa wanaume wengi kukimbia majukumu yao ya ulezi.

Wengi wetu tumejikuta kwenye kupinga kauli ya rais, na kusahau aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya kuelekeza jitihada hizi za kuwatetea wanafunzi watao pata Mimba kuendelea na masomo.

Kwanini jitahada hizo hizo zistumike kuwapatia elimu wanafunzi hao wa kike na wakiume na jamii kwa ujumla kuwa swala la kufanya NGONO na watoto wa shule ni kumuharibia mwanafunzi maisha yake ya baadae.

Vilevile wanaharakati hawa wanapaswa pia kuunga mkono sheria kali dhidi ya wanaume watakao sababisha kuwajaza mimba wasichana wa shule za msingi na sekondari.

Vilevile kuna haja kubwa sana kwa wanaharakati hao, pamoja na serikali kutoa elimu na kufanya kampeni nchi nzima na haswa mashuleni, wakiwalenga Wanafunzi wa kike na Wakiume, kuwa swala la kufanya ngono ilihali ni mwanafunzi wa shule ya Msingi/Sekondari, kutawapelekea kufukuzwa shule na kukosa nafasi kwenye shule za serikali.

Kampeni zijikite kwenye kumuelimisha na mwanafunzi ajiepushe na tamaa na kulaghaiwa na wanaume watakao muomba kufanya naye ngono na anapaswa kusubiri mpaka pale atakapo maliza elimu ya sekondari kama si chuo kikuu na raha ya kufanya mapenzi ni kwenye ndoa.

Kampeni hizi zishihishie tu mashuleni, bali ziwepo pia kwenye majumba yetu ya Ibada, washirikishwe pia viongozi wa dini mbalimbali, hili wazungumze na waumini wao, kwa lugha ambayo waumini wataielewa.

Kwa sababu hakuna dini ambayo inaruhusu zinaa kwa waumini wao. Kwa kuwatumia viongozi wa dini, kampeni za kuzua ufanyaji wa ngozo mashuleni zitaweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa sana.

Wanaharakati wengi wamekuwa wakitaka watu wawe huru kwenye maamuzi yao, na haswa swala la kujamiiana, kiasi ya kwamba kumekuwa na kampeni za ugawaji wa kondom mashuleni, na hili ndio limechangia sana upatikanaji wa wanafunzi kuwa wajawazito.

Kwanini wagawe kondom mashuleni, lengo lao ni nini haswa kama si kuchangia kuiharibu jamii? Kwanini wasitumie utaalamu wao na ujuzi wao kufanya kampeni zitakazo mwepusha mtoto wa kike na mimba za kabla ya wakati?

Tutafika mahala wanaharakati wataanza kukampeni hata ndoa za jinsia moja kwa kisingizo za haki za kibinadamu za kujichagulia au kwa wale wanaojiuza kuwa walipe kodi kwa kuwa nayo ni kazi yenye kuingiza kipato.

Tuombe Mungu tusifikie uko, lakini hili tusifikie uko kuna haja kubwa sana ya kuwashirikisha viongozi wetu wa dini, kwenye hizi taasisi au NGO zinazosema kuwa zinatetea haki za kibinadamu.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!