TUJIEPUSHENI NA MAKUNDI HAYA
Al-shabaab na ISIS ni Makundi ya Kigaidi
Miaka hii ya karibuni kumejitokeza baadhi ya watu, wakijitambulisha kwa mabandiko na mapicha mbalimbali ya wapiganaji walioko uko Somalia, (Al-shabab) Syria na Iraq, kwa jina maarufu ISIS.
Kwa mtazamo wa juu kwa juu, unaweza kuona kuwa watu hao wanapigania kuwepo na serikali ya Kiislam kwa maana ya khilafa na kabla ya hapo walijitangazia kuwepo kwa Majimbo ya Kiislam yaani Islamic State.
Kuna baadhi ya wanao jiita waislam kwa makusudi kabisa na kwa malengo yao maalumu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwashawishi watu wawaunge mkono wauwaji hao.
Wakati huohuo makundi haya yameweze kupata kuungwa mkono na baadhi ya Waislam wasio jitambua au kuelewa kinacho endelea. Wanayanasibisha makundi haya na Uislam eti yanapigana Jihad kwa manufaa ya Uislam duniani.
Matokeo yake vijana wengi wameishia kukamatwa na vyombo vya usalama na kuozea jela.
Hapo hapo wamesahau kuwa ISIS (Islamic State of Iraq and Syria) au ISIL (Islamic State of Iraq and the Levant) Neno Levant hapa linakusanya nchi Lebanon, Syria, and Israel. Wenyewe wanapigana kwa malengo mengine na uku wakijitambulisha kutaka kuzikomboa nchi zilizoko kwenye majina yao ambazo ni Iraq, Lebanon, Syria, na Israel.
Lakini ajabu utawakuta vijana wachache wasio jitambua, wanashinda kwenye mitandao ya kijamii, wakiwaunga mkono ISIS.
Haiwezekani kwa Muislam awe anauwa Waislam wenzake kisha ajitambe kuwa yeye ni Muislam, kisha watokee watu wawaunge mkono uku wakiwa na vijisimu vyao vya mkononi na wakijifanya kuwataka watu wakapigane upande wa Isis au Al-shabab.
Waislam wachache awa ambao wanatumiliwa na nchi za Kimagharibi ili kuonyesha kuwa wanapiga vita Ugaidi, lengo ni kuwaridhisha wananchi wao ambao ndio walipa kodi kuwa wanapiga vita ugaidi si nje ya nchi tu, hata ndani ya nchi zao.
Ndio ikaundwa program maalum ya kuwafundisha baadhi ya mashushu, ili kutafuta nani na nani wanaelekea kuwaunga mkono ISIS na magaidi wengine.
Wakatengenezwa Waislam wasio jitambua au wenye kuendekeza matumbo yao, wakakesha mitandaoni na kujifanya kuwa wana uchungu sana na Uislam na wanawaunga mkono ISIS, ili hali wao wenyewe hata uwanja wa vita hawaujui unafananaje.
Mashushu awa uwa hawakamatwi, hata wakijitokeza hadharani na kuonyesha wazi kuunga mkono harakati za ISIS, Wanao kamatwa ni wale walioingia mkenge na kudhani kuwa wanakwenda kwenye JIhadi ya kweli kumbe ni kanyaboya.
Mashushu hao, wakisha wapata watu ambao wanaona kuwa wanawaunga mkono Al-shabaab au ISIS haraka sana wanawaripoti kwa mabwana zao na mara uishia jela.
Na hii ndio mbinu zinazotumika hivi sasa za kujifanya wanapambana na siasa kali (extremist) lakini kwa kuwa hakuna Uislam wa namna hiyo ndio kukawa na watu maalum kama hao ambao kazi yao ni kuangalia nani na nani wanaweza kuwashawishi.
Wakisha wapata uweza hata kuwapa mafunzo na mbinu hafifu za hapa na pale, kisha kuwapatia tiketi za kugushi na kuwaelekeza waende viwanja vya ndege ili waende Syria au Somalia.
Lakini ghafla vijana hao ujikuta wapo mikononi mwa vyombo vya usalama na habari zao kuandikwa kwenye vyombo vya habari kuwa ni magaidi walikuwa wanakwenda Syria kusaidia ISIS au Somalia kujiunga na Al-shabab.
Na raiya wa nchi za ulaya wakiona hivyo uona kuwa serikali zao zinafanya kazi vyema za kuwalinda na magaidi wa nje ya nchi na hata wa ndani ya nchi.
Hii inafanyika sana kwenye nchi za Uisngereza, Ufaransa na Marekani na nchi zile zinazopiga vita Uislam kivitendo.
Ukikutana nao vibaraka hawa wa kimagharibi, utasikia wakisema ISIS wanauwa Makafiri, Wanafiki na Washirikina, sasa tunawauliza, kama mtume angeua Makafiri na Washirikina wote wa MAKKAH, kisha Waislam waliokuja Afrika nao wangeua Makafiri na Washirikina wote walio wakuta, sijui mimi na wewe kama leo tungekua hapa.
Ni jambo lililo wazi kabisa babu wa babu zetu wangekuwa maiti na hata mimi na wewe tusingepata hata hii nafasi ya kuwa Waislam, maana ukiangalia wengi tunaweza kukuta Mababu zetu walisilimu kwa kuona tabia njema za hao walikuja na Uislam na ndio wakaupenda na kusilimu.
Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa makundi haya, utaweza kugundua kuwa makundi yote haya ni zao la Mmarekani na lengo ni kudhoofisha nchi zenye Waislam wengi ili wapate kuchukua kiurahisi rasilimali za nchi husika kama vile mafuta.
Ndio tukaona uko Iraq walipoweza kuangusha serikali jambo la kwanza kufanya ni kulinda kwa nguvu zote vyanzo vyote vya mafuta, na wakafanya hivyo hivyo nchini Libya.
Sasa hivi Syria kila leo inatafutiwa sababu ya kupigwa mabomu ya maangamizi, wanasubiri Syria ianguke rasmi kisha utaona wanapeleka majeshi kujifanya kuweka mambo sawa kumbe wanafata wanao yataka.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?