Saturday, 11 August 2018

MINARA YA MAWE (Georgia Guidestones)
YA AJABU JIMBONI GEORGIA MAREKANI
(Miongozo - Maelekezo ya Kwenye Mawe ya Georgia)
Moja ya Lugha zilizotumika ni KISWAHILI.

Minara hiyo ya mawe ya Georgia ya iliyochongwa kwa kutumia madini ya graniti ilikamilika kujengwa mwaka 1980 na iko katika mkoa wa Elbert, kwenye jimbo la Georgia, nchini Marekani. Mawe hayo yana ukubwa wa futi 19 na nchi 3 sawa na mita 5.87na yana uzito wa jumla ya Paundi 237,746 sawa na kilogram 107,840.

Yanapatikana umbali wa kilomita 145 Mashariki mwa Atlanta, na umbali wa kilomita 15 kaskazini mwa katikati ya Elberton. Minara hiyo pia ipo umbali mfupi kutokea mashariki mwa barabara kuu ya Georgia (Georgia Highway 77 - Hartwell Highway), na ina weza kuonekana kutoka kwenye barabara hiyo. Ishara ndogo kando ya barabara zinaonyesha wapi mawe hayo yalipo kwa kibao kilicho andikwa "Guidestones Rd."

Kwenye minara hiyo kuna Seti ya miongozo 10 (guidelines) iiliyochongwa kwenye mawe hayo kwa kutumia lugha nane za kisasa, ambazo ni Kiingereza (English), Kihispaniola (Spanish), Kiswahili, Kihindi, Kiebrania Hebrew, Kiarabu (Arabic), Kichina (Chinese) na Kirusi (Russian).

Na jumbe fupi zimeandikwa kwa juu ya minara katika lugha nne za kale ambazo ni Kibabeli (Babylonian - in cuneiform script), Kigiriki cha kale (Classical Greek), Kisanskrit Lugha ya kale ya Kihindu (Sanskrit) na lugha ya kale ya Kimisri (Ancient Egyptian - hieroglyphs).

Mnamo Juni 1979, mwanamume mwenye kutumia jina bandia (pseudonym) la Robert C. Christian aliwasili kwenye Kampuni ya Kuchonga Graniti au Matale (Elberton Granite Finishing Company) kwa niaba ya kikundi kidogo cha Wamarekani waaminifu (loyal Americans), na kuagiza achongewe Minara ya mawe makubwa ya madini ya Graniti. Akawaambia kwamba mawe  hayo yatatumika kama dira, kalenda na saa, na lazima yawe na uwezo wa stahimilia matukio ya majanga ya kiasili.

Mtu aliyemkuta akijulikana kwa jina la Joe Fendley alidhani kuwa Christian alikuwa na upungufu wa akili na alijaribu kumkatisha tamaa kwa kumuonyera gharama kubwa kubwa zitakazo karibiana nazo kwenye mradi huo ambao kampuni hiyo ingemtoza, kwa sababu kungehitajika zana maalumu za kuchongea mawe hayo lakini mtu yule aliendelea kushikilia kuwa anahitaji achongewe mawe makubwa ili aweke ujumbe uliokusudiwa kutoka kwa watu walomtuma.

Mwishowe alikubaliwa na kutakiwa aonane na mtunza mahesabu wao ili aweze kulipia gharama. Wakati wa kutoa malipo, Christian alielezea kwamba yeye anawakilisha kikundi ambacho kilikuwa kikipanga mipango ya mwongozo kwa miaka 20 ijayo, na ni kundi ambalo halitaki lijulikane na yeyote yule.

Christian alileta michoro na vipimo (model) yaani mfano mdogo wa hayo mawe yatakavyo kaa au yatakavyokua akiambatanisha na vidokezo vya kurasa kumi vya vipimo vya eneo husika.

Makaratasi yakionyesha ardhi ya ekari tano ilinunuliwa na Christian mnamo Oktoba 1, 1979, kutoka kwa mmiliki wa awali wa shamba bwana Wayne Mullinex. Mullinex na watoto wake walipewa haki ya maisha ya kulisha mifugo yao kwenye eneo husika.

Minara ilikamilika mwezi Machi 22, 1980, mbele ya watazamaji wapatao mia 100 au 400 waliudhuria ufunguzi wake. Christian baadaye alihamisha umiliki wa ardhi pamoja na hiyo minara kwa uongozi kwa mkoa wa Elbert.

Kufikia mwaka 2008, Minara hiyo ya mawe yaliharibiwa kwa kupigwa rangi na kuchorwa graffiti yenye kauli mbiu Kifo kwa utaratibu mpya wa dunia (Death to the new world order).

Gazeti la wired nchini Marekani liliandika kuwa uharibifu huo kuwa ni "tendo la kwanza kubwa la uharibifu katika historia ya 'guidestones' (the first serious act of vandalism in the guidestones' history").

Mnamo Septemba 2014, mfanyakazi wa idara ya matengenezo ya mkoa wa Elbert  aliwasiliana na FBI wakati mawe hayo yalipoharibiwa kwa michoro ya graffiti moja ya maneno yalioandikwa kwenye hayo mawe ni  "Mimi ni Isis, mungumke wa upendo" (I Am Isis, goddess of love).

Ujumbe au Amri kumi zolizoandikwa kwenye Mawe hayo ni haya, Lugha ya Kiswahili na Kiingereza.


LUGHA YA KISWAHILI ILIYOTUMIKA

1. DUMISHA BINADAMU CHINI YA MILIONI (MIA) TANO (500, 000,000) KULINGANA NA ASILI YA MAKAZI YAO.

2. ONGOZA UZAZI KWA HEKIMA ENEZA AFYA NA USTAWI KWA WOTE.

3. TUNGA LUGHA MPYA YA KUUNGANISHA BINADAMU

4. TULIZA HAMAKI -- DINI -- MILA -- MAMBO YOTE NI KWA AKILI NA BUSARA 

5. LINDA WATU NA MATAIFA KWA SHERIA NA HAKI ZA MAHAKAMA

6. MATAIFA YOTE YAJITAWALE NA YATATUE MATATIZO YAO KWENYE KORTI LA ULIMWENGU.

7. ACHILIA MATAWALA MADHALUMU

8. LINGANISHA HAKI ZA WATU NA ZA MATAIFA 

9. TUNZA UKWELI UZURI NA UPENDO TAFUTA USIKIZANO WA: DAIMA 

10. KUSIWE NA MARADHI MABAYA DUNIANI IPE MAUMBILE NAFASI IPE MAUMBILE NAFASI

LUGHA YA KIINGEREZA ILIYOTUMIKA.

1. MAINTAIN HUMANITY UNDER 500,000,000 IN PERPETUAL BALANCE WITH NATURE.

2. GUIDE REPRODUCTION WISELY — IMPROVING FITNESS AND DIVERSITY.

3. UNITE HUMANITY WITH A LIVING NEW LANGUAGE.

4. RULE PASSION — FAITH — TRADITION — AND ALL THINGS WITH TEMPERED REASON.

5. PROTECT PEOPLE AND NATIONS WITH FAIR LAWS AND JUST COURTS.

6. LET ALL NATIONS RULE INTERNALLY RESOLVING EXTERNAL DISPUTES IN A WORLD COURT.

7. AVOID PETTY LAWS AND USELESS OFFICIALS.

8. BALANCE PERSONAL RIGHTS WITH SOCIAL DUTIES.

9. PRIZE TRUTH — BEAUTY — LOVE — SEEKING HARMONY WITH THE INFINITE.

10. BE NOT A CANCER ON THE EARTH — LEAVE ROOM FOR NATURE — LEAVE ROOM FOR NATURE.

Coordinates34°13′55″N 82°53′40″W

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!