Friday, 1 March 2019

ELIMU YA MAHUSIANO NA (NGONO) JINSIA

Relationship Sexuality Education; RSE

 • Tunapaswa Kuruhusu Watoto katika Matamasha ya (Ngono) Wakaa Uchi?
 • Je Elimu ya Ngono Kufundishwa Mashuleni kuanzia Shule za Msingi darasa la Pili.

Nilikuwa nimekaa naangalia vipindi kwenye Luninga, taarifa za habari na mambo kadhaa yanayojiri ulimwenguni. Moja ya kipindi kilichovuta usikivu wangu, kilikuwa kinahusu mjadala wa wapendao kukaa uchi, wanao jihita Naturist, yaani wanaoitakidi kuwa binadamu asili yake ni kukaa uchi ni iwe haki ya kila mtu, wakiwemo wanafamilia pamoja na watoto wanaopendelea kwenda uchi na iwe haki kisheria kuwashirikisha watoto...

Mjadala huu, umenikumbusha ule mjadala wa mashoga, na kampeni zao za kutaka kila mtu aunge mkono harakati za kishoga za liwati na usagaji na hata ndoa za jinsia moja.

Kiasi sasa ndoa za jinsia moja zimehalalishwa kwenye baaadhi ya nchi za Ulaya, ikiwemo nchi za Ubelgiji (Belgium), Denmark, Ufini (Finland), Ufaransa (France), Uingereza, Ireland na nchi zingine za Amerika na Kiafrika pia ikiongozwa na nchi ya Afrika Kusini.

Awa awa karne chache tu nyuma, babu zao (Walami) walitawanyika duniani na haswa nchi za Kiafrika na kukuta baadhi ya watu (si wote) wakitembea uku wamevaa upatu tu, kusitiri viungo binafsi, wakawaona kuwa si wastaarabu na washezi. Wakawapa nguo na kuwashinikizia kuamini imani mpya.

Waafrika kama ilivyo asili yetu ni uungwana na kuwapenda wageni wakakubali baadhi ya ustaarabu wa hao Walami, baadhi wakaamini...

Leo hii, ustaarabu ule, umebakia kwa Waafrika na Ushenzi ule ule wa mababu wa Kilami, umekuja na umerejea kwa kasi sana kwenye hizi nchi za Kilami, kiasi ya kwamba, mwanamke akijistiri anaonekana yupo kinyume na ustaarabu wa dunia na ukiwa uungi mkono harakati za mashoga na wasagaji, basi waonekana wewe si mstaarabu tena mbaguzi, na unaweza hata kupata misukosuko na hata kutengwa na taasisi za Kiserikali na hata binafsi.

Kama haitoshi, hivi sasa kwenye hizi nchi zikiongozwa na Uingereza na Marekani, wamekuja na mtaala mpya wa Kielimu, kwamba watoto kuanzia shule za Msingi na sekondari ni lazima wafundishwe elimu ya Mahusiano na Elimu ya Jinsia - Ngono (Relationships and Sexuality Education ). Na ni somo la lazima, si hiyari.

Watoto watafundishwa mengi, yakiwemo kukubali uwepo wa familia tofauti tofauti kwa maana ya familia iliyo ya jinsia mbili (Mke na Mume) na ile inayojengwa na jinsia moja aidha mume/mume au mke/mke na mengine mengi kuhusiana na mahusiano ya Kingono.

Wengi wanaweza kusema, hayo ni ya uko Ughaibuni, lakini wasisahau kwamba, dunia hii ndogo, michanganyiko ya mila na tamaduni mbalimbali ndizo zinazojenga jamii na ni moja kati ya Utandawazi (globalization).

Haya yanayofanyika sasa kwenye hizi nchi za Kimagharibi, hayaishii kwenye hizo nchi tu, tumeshuhudia matishio kadhaa ya kiuchumi kwa nchi ambazo hazitoi haki za usawa kwa mashoga na wasagaji.

Kama nchi hairuhusu Ushoga basi ina hatari ya kuwekewa vikwanzo na nchi zinazo endeshwa na mashoga na kwa wale wazamiji wanataka kuishi hizi nchi, kiasi wamepata kisingizio, wanachofanya ni kusema tu kuwa wao ni mashoga na wamekimbia manyanyaso kwenye nchi zao, basi haraka sana wanakumbatiwa na kukubaliwa kupewa hifadhi.

Na sasa hivi kwenye hizi nchi zetu zinazoitwa dunia ya tatu, kampeni ndogo ndogo za chini chini zimeanza kuchipua, lengo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa elimu ya ngono inapaswa kufundishwa kuanzia madarasa ya chini kabisa ya shule za msingi aidha kuanzia darasa la pili au la tatu kama si chekechekea.

Tutasikia visa vingi kutoka kwa mawakala wa ngono na mashoga, tutasimuliwa simulizi za kutunga na hata zile zenye ukweli nusu ili kuhalalisha elimu ya ngono ianze kufundishwa kuanzia aidha chekechea au shule za msingi kuanzia darasa la kwanza au la pili.

Tusipo kuwa makini, basi tutaingizwa kwenye ulimwengu wa manyani wa kutembelea utupu, tukibaki kuchekena kicheko cha (Ashamkumu si Matusi) "Nyani haoni Kundule.

Je tutawalinda vipi Watoto zetu, maana sasa ni Hamkani si Shwari tena

Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki...
Q 7:33

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!