Thursday, 26 November 2015

Swali kwa walio kwenda HIJJA

Linaweza kuonekana ni jambo la ajabu kwa jinsi swali lilivyo, labda tu kwa kuwa hatuna mazoea ya kuulizana nini tumeletewa, pindi mmoja wetu anapotoka safari. Na wakati mwingine linaweza kuonekana kuwa ni utovu wa adabu au ukosefu wa hishma pale unapo muuliza mtu kuwa kaleta zawadi gani uko alipotoka.

Lakini tunapaswa kujuwa hapa wanao ulizwa ni wale tu ambao wametoka HIJJAH, safari ambayo ni mwito kutoka kwa Muumba wetu.

Nimewalenga wao kwa sababu ndio waliorejea kutoka kwenye nyumba tukufu hapa duniani, wamerejea kutoka Makkah na Madina, sehemu ambayo kila moyo wa Muislamu unatamani siku moja kuitikia wito huo ulio mtukufu.

Wengine wanaweza kusema kuwa nimechelewa kuuliza kwa sababu zawadi zote walizoleta zimekwisha gawiwa na hata hao waliozawadiwa usikute wamekwisha zitumia na si ajabu nyingi katika hizo zimekwisha malizika.

Ndugu, jamaa na marafiki zao wanaweza kusema kuwa mbona mimi nimeletewa iki na kile mfano wapo walioletewa Kofia, tasbihi, Uturi na miswala lakini hivi vyote vitakwisha au vitachakaa na kuchoka.

Zawadi ninazo ziulizia mimi si zile ambazo zitachakaa na kwisha lahasha bali ni zile zawadi ambazo hazita chakaa wala kwisha ni zawadi ambazo zitaleta uhai na matumaini katika nyoyo zetu.

Je ni zawadi gani za kiroho mlizozijaza nyoyoni mwenu mkatuzawadia na sisi?
  • Je, mmetuletea wema na utii wa AbiBakr Sidiq (ra) [Abdullah ibn Abi Quhaafah]?
  • Au uadilifu wa Umar ibn Al-Khattab (ra)?
  • Au mmetuletea maadili na ukarimu wa Uthman ibn Affan (ra).
  • Je mtatuwakilishia ujasiri na ushujaa wa Ali ibn Abi-Talib (ra)?

Je hizo ndio miongoni mwa zawadi mlizozileta, Je mtaweza kutoa hamasa ya zama za Mtume (saw) kutoka nyoyoni mwenu kuupa Ulimwengu wa Kiislamu ambao kwa sasa unakabiliwa na shida nyingi na maumivu yasiokwisha!?

Kama jibu lake litakuwa "NDIO" basi hatujachelewa wala nyinyi hamjachelewa kutugawia zawadi hizo, nasi tutazipokea tunu hizo kwa mikono miwili, kwa sababu ndizo zawadi na tunu pekee zitakazobadili mustakabari mzima wa maisha yetu katika dunia hii tunayopita tu.

Basi fanyeni hima kutugawia!

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!