WANAVYO SHUGHULIKIWA WAKWEPA KODI
Baada ya uchaguzi kwisha na Rais kukabidhiwa rasmi jukumu la kuongoza nchi, Rais Magufuri ameonyesha vile utendaji wake wa kazi kivitendo na tumeshuhudia jitihada zake katika kurekebisha baadhi ya wizara idara mbalimbali za serikali.
Wanao mfahamu John Pombe Magufuri, haswa wale ambao walibahatika kufanya naye kazi hawaoni ajabu katika utendaji wake wa kazi. Kabla ya kuwa Rais wa Tanzania, Magufuri alishakuwa waziri na kufanyakazi kwenye wizara kadhaa na matokeo yake wengi wameyaona na wameyafurahia.
Rais Magufuri tangia kwenye kampeni zake, kauli mbiu yake ilikuwa ni "Hapa Kazi tu" ikimaanisha kuwa serikali atakayo iongoza yeye itawajibika kusimamia kwa kila hali kile ambacho yeye anakiamini kuwa kitasaidia Watanzania katika kujikwamua kiuchumi.
Tumeshuhudia kwa masiku machache tu tangia alipoapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, jinsi anavyo yaendea mambo kwa mwendo kasi ya kuwabana wakwepa kodi za serikali na kuwabana watu ambao wanahujumu uchumi kisawasawa kwa lengo la kurejesha pesa zinazoibwa kwenye kodi na kuondoa matumizi yasio ya lazima kwenye wizara na maofisi ya serikali. Kwa kweli ni jambo zuri sana, ila inapaswa pia kuangalia upande wa pili.
Hapa ninacho hofia si uko serikalini la hasha, bali upande wa wafanyibiashara waletao bidhaa aidha mikoani au nje ya nchi, kwa maana athari itakayo patikana kwenye bei ya bidhaa ambazo waletaji wake ndio hao wanaobanwa kikamilifu ili walipe kodi inayo husika.
Bidhaa nyingi ambazo zimelipwa kodi ndogo zina uwezekano wa kuuzwa kwa bei ya chini, na zile ambazo zimelipiwa kodi kamilifu kuna uwezekano wa kuuzwa ghali na ili ndio linaweza kutokea na kusababisha mfumuko wa bei kwa walaji.
Nahofia kuna uwezekano kwa serikali kurudi miaka thelathini nyuma kipindi ambacho serikali ndio walikuwa wapangaji wa bei za bidhaa na si kama hivi sasa wafanyibiashara wanajipangia bei au wanategemea soko la bidhaa lipo vipi...!
Vilevile anapaswa kuwa makini sana na mtandao wa viongozi mafisadi, kwa sababu ndio wanaolengwa, nao wanaweza kutengeneza uadui na kupanga njama za kuhujumu jitihada zake, kwa kukwamisha baadhi ya mambo.
Hali inaweza kuwa mbaya bidhaa zikakosekana kisha ulanguzi na maduka bubu kama zilivyokuwa store bubu za bia enzi ya Nyerere zikarejea tena...!
Ninacho kiona mimi kwa Rais wetu huyu ni jitihada zake kurejesha heshima kwenye kila wizara na hata watakapochaguliwa mawaziri wakute kila wizara zipo safi kiasi chake na hata atakayeshika uwaziri au ukatibu wa wizara husika ajuwe kuwa kinachotakiwa ni utendaji ulio tukuka na si uzembe uzembe kama ilivyokuwa uko nyuma.
Umakini ni muhimu anatakiwa awatumie wasomi mbalimbali kulingana na jambo husika kama vile mambo ya uchumi na fedha, elimu na teknolojia, nakadhalika. Tena akiona mtu anafaa hata kama yupo upande wa upinzani si vibaya kumuweka mahali akapatengeneza vizuri kwa manufaa ya nchi na watanzania kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?