Tuesday, 9 February 2016

Nipo kwenye daladala naelekea Mbagala, daladala limejaa kiasi hata pa kukanyaga hakuna kama mnavyojuwa daladala za Mbagala na maeneo mengine zinavyo jaa.

Kwa bahati sikufanikiwa kupata siti ya kukaa, kwa hiyo nikalazimika nisimame tu. Ajabu karibia viti vyote vilikuwa vimekaliwa na wanawake, nikajiuliza fujo zote zile za kugombea basi na midume na midevu yetu tumekosa viti kweli wanawake hawa ni makomandoo wa jeshi si mchezo.

Pembeni kulikuwa na wadada wawili wamekaa na kwa kuwaangalia haraka haraka nikahisi kuwa wanajuana maana mazungumzo yao tu nilihisi hivyo.

Mdada mmoja alikuwa anamlalamikia mwenzake kuwa hana bahati kila akipata mchumba baada ya siku mbili tu anakimbiwa, hajui tatizo ni nini!

Mazungumzo yao yakawa yanaendelea wakizungumza ili na lile na wakafikia mpaka kupeana ushauri wa kwenda kwa mtaalam wa mambo ili afanyiwe mambo labda akipewa power benki anaweza kubahatika kuwa na mtu wa kudumu naye japo mwezi, tena mwanamume ambaye sio feki feki yaani real man si mali ya mchina.

Nilipo waangalia vizuri nikashindwa kuwaelewa jinsi walivyo, kwa sababu sikuona hata kitu kimoja kwenye mwili wake kuwa ni cha asili yake, yaani hapo sina maana ya mavazi lahasha nina maanisha vitu alivyo zaliwa navyo kama vile nywele si zao, wamevaa manywele ya bandia zamani tukisema nywele za maiti.

Ngozi ya uso si zao, nahisi rangi yao ya asili ni nyeusi lakini wamekuwa na rangi mbili kama vidonge vya tetasakrini.
Kope za kubandika, kucha za kubandika, midomo imewekwa rangi nyekundu si nyekundu maana imechanganyika na na rangi ya samawati sijui buluu haya twende kazi, nahisi utakuwa ni ule wino wa kupigia kura.

Nilipofika safari yangu, kuna jamaa niliyeshuka naye akanambia kaka naona ulikuwa unawashangalia wale wadada, nikamwambia ni kweli maana nahisi si binadamu wa kawaida, mtu gani ana marangi mengi kama bendera ya tafa. Jamaa akacheka na kunifahamisha kuwa hao wana hafadhali maana kuna wengine hata naniu si zao, yaani yaani zile naniu za kulishia watoto, wengine wanaita manyonyo, nayo pia uwa si zao na si hizo tu hata makalio siku hizi wanaagiza kutoka China, nikashangaa sasa kama hata makalio wanaagiza kutoka China mbona wachina wenyewe hawana makalio makubwa au ndio wameyakata na kuwauzia hawa wa kwetu, jamaa akacheka sana, akanambia hapana, hao wanaweka masiponji maalumu au wengine wanatumia dawa maalumu za kukuzia makalio.

Nikabakia najiuliza, sasa ni mwanamume gani ambaye ni real man ataoa mwanamke feki maana kila kitu ni cha kubandika maana ukiwaangalia hao wadada zetu wa siku hizi wamekuwa kama midoli ya kuchezea, kisha wao wanaweka masharti ya kuolewa na real man, yaani kweli kuna mwanamume wa kweli wa kuoa midoli, maana mimi sioni tofauti ya hawa wadada na midoli zamani tukiita wanasesere, nahisi hata hao wanaseserere wana afadhali.

Tafuteni tu midoli wenzenu, hao real man wataoa real woman.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!