Saturday, 9 July 2016

Miaka ile ya enzi zile, tulikuwa tukikaa tukizunguka moto tukisimuliawa Ngano, Liwaya, Hadithi na simulizi mbalimbali za kimaisha.

Watoto wa rika mbalimbali, walikuwa wakikusanyika kipindi cha jioni kumshhikiliza Bibi au Babu au mtu mzima mmoja akisimulia visa vya kusimumua, visa vya kishujaa, visa vilivyoweza kuamsha hisia chanya kwa vijana na wasiwe wavivu katika maisha yao.

Miaka ikasonga mbele vijana na wasichana wakakuwa na wengine wakaanza kujitegemea, wapo walio olewa na wapo walio oa. Wakakuta dunia imesonga mbele kimaendeleo, dunia ikawa imepata aina mpya za telnolojia mbalimbali.

Wengi wakawa waajiliwa kwenye viwanda na wengine wakawa wafanyakazi serikalini. Walipozaa watoto wao, wazazi wale wapya wakajikuta wamekamatika na shughuli za kutafuta maisha, wakakosa tena muda wa kukaa na watoto zao kuwasimulia hadithi au Ngano au Liwaya mbalimbali.

Chombo pekee kilichoweza kupeleka habari kwa haraka, japokuwa ilibidi umuombe opereta akuunganishe kilikuwa simu za mikonga, hakika chombo hhiki kilisaidia sana, japokuwa ni wachache mno walioweza kukimilhhiki na haswa maafisa wakubwa wa serikali.

Ilikuwa chombo hhiki kiitwacho simu za mikonga, unaweza kuomba kwa opereta, saa moja asubuhi akuunganishie namba fulani, ukasubiri baada ya saa moja nzima ndio simu yako inaita na kuambiwa sasa waweza kuongea umekwisha unganishwa tayari.

Na hata hivyo maongezi hakuzidi hata dakika tano, ni kiasi cha kutoa taarifa muhimu tu kama vile habari za vifo au harusi.

Chombo hhiki simu za mikonga, hakikuwa maarufu sana, labda kwa kuwa umilhhiki wake ulikuwa ni wa tabu, lakini binadamu hakuchoka, ndipo baadae nafasi ile muhimu ikachukuliwa na chombo kingine ambacho kilikuja kupata umaarufu szaidi.

Chombo hhiki kiliwaunganisha ndugu, jamaa na marafhhiki kwa kuweza kutumiana salamu na habari muhimu katika maisha yao ya kila siku. Chombo ambacho kiliweza kuleta changamoto kubwa kwenye harakati mbalimbali za kimaisha, chombo hhiki kiliitwa Radio.

Enzi zile Radio ilikuwa kifaa muhimu sana cha kuhabarishana, hakukuitajika tena tarishi au mjumbe kutoka serikalini kupita na ngoma yake kuwahabarisha wanachi matukio muhimu, uku akirindima kwa maneno ya "...La Mgamboo... La Mgambo Lhhikilia Lina jambo...!"

Nafasi ile adimu ikachukuliwa na chombo hhiki kiitwacho Radio, hakika chombo hhhiki kilikuwa muhimu sana kwa maisha ya watu wengi haswa wafanyakazi na wakulima ambao hawakuwa na nafasi kubwa ya kukaa na familia zao na kusimuliana matukio mbalimbali.

Ilikuwa tu hhikifika jioni familia hhikikaa pamoja na kushhikiliza vipindi mbalimbali vilivyorushwa na watangazaji, ilikuwa raha sana pale unaposhhikia jina lako lhhikitajwa kuwa umesalimiwa na ndugu yako au rafhhiki yako anayeishi mji mwingine mbali kabisa na unapoishi. Na hata wakati mwingine uliweza kuhabarishwa taarifa za misiba ya ndugu na jamaa wanao kuhusu na wasio kuhusu.

Ilikuwa kila baada ya taarifa ya Habari na mazungumzo baada ya habari, tukikaa kimya kushhikiliza matangazo ya vifo, maana tulichelea labda tunaweza kushhikia habari za ndugu na jamaa wanao tuhusu kupitia chombo hhiki kidogo cha mawasiliano.

Na si Radio tu ambayo ilikuwa imeweza kuwakutanisha watu, vilevile kulikuwa na kitu kimoja khhikitumika sana kupelekeana salamu na habari za kifamilia na haswa kama ilikuwa haifai kutumia chombo cha habari kama vile Radio. Hapo tuliendelea kutumia njia ambayo ilikuwa hhikiendelea kutumia tangia binadamu alipoanza kujua kusoma na kuandika, nayo ni utumiaji wa Barua au waraka.

Maisha yakaendelea mbele Bara la Afrika nalo halikubaki nyuma watu wake wakazidi kupata maendeleo, kidogo kidogo kikaja chombo kipya cha kupatanishana habari na matukio. Hapo ndipo kikaingia kwenye baadhi ya majumba na haswa wale waliokuwa na uwezo wa kifedha.

Hakika chombo hhhiki, kilileta mambo kwelikweli, maana kina sie ambao hatukuwa na uwezo nacho ilitubidi tuwe na marafhhiki hata kwa kulazimisha ili nasi tuweze kudoea majumbani mwao kwenda kukiangali.

Chombo hhhiki kilikuwa na maajabu yake, maana kiliweza kuonyesha binadamu na matendo yake na tena wakati mwingine kilionyesha watu walioishi mbali sana na bara la Afrika. Ajabu sana chombo hhhiki kiliweza hata kuonyesha baadhi ya watu ambao walikwisha farhhiki zamani.

Chombo kipyaa kiliendelea kupata sifa nzuri na mbaya, kilipata sifa nzuri pale baadhi ya wazazi walipoweza kurudi majumbani mwao mapema na kukaa na familia zao kwa pamoja na kukikodolea macho.

Na wakati huo huo kiliweza kusababisha baadhi ya watu kuchelewa kurudi majumbani mwao kwa sababu aidha walipitia kwenye vilabu vya pombe au majumbani mwa marafhhiki au ndugu zao waliokuwa na uwezo wa kumilhhiki chombo hhhiki.

Chombo hhhiki ambacho tulhhikijuwa kwa jina la Televisheni na baadae tukakipa jina la Runinga, bado kiliweza kutuunganisha vizuri tu.

Watu waliweza kukaa na ndugu, kutembeleana kukaongezeka na haswa ukiwa nacho basi nyumbani kwako hakutakosa wageni, aidha wawe majilani zako na watoto zao, marafhhiki waishio mbali na wewe na hata ndugu kutoka mikoani waliweza kufunga safari na kuja kukaa kwako masiku kadhaa wa kadha.

Wale watoto watundu waliokuwa hawapendi kukoga, waliweza kukubali kukoga kwa kuwa tu, kama hawakukoga basi hawakukaribishwa kenye majumba ambayo wanamilhhiki kifaa hhhiki, na hata kama nyumbani kwako kilikuwemo, basi kilikuwa ni fimbo tosha kwa watoto wasioshhikia, maana akileta ubishi au ukahidi ilikuwa ni kumwambia tu, leo hutotizama tiivii, basi kama maajabu vile utaona mtoto mwenyewe anaelekea, kama kuutumwa dukani atakwenda kama kukoga atakoga hata mara tatu kwa siku.

Na kwa wale watu wazima, kama uliwahi kugombana na rafikio au nduguyo, ilikuwa rahisi sana kuombwa au kwa wewe kumuomba muyamalize ili muendelee kuishi kama zamani, kwa kuwa tu aidha wewe au yeye alikuwa anamiliki chombo hiki cha maajabu kilichoweza kuwaonyesha watu na wakifanya mambo mbalimbali ya kufurahisha na hata ya kusikitisha.

Maisha hayakusimamia hapo tu, Bara la Afrika likazizima kwa maendeleo na haswa wakaazi wa Afrika ya Mashariki hawakubakia nyuma, walienda sambasamba na maendeleo hayo.

Chombo hiki Runinga au kwa kifupi tivii, kilipozidi kupata umaarufu, watu wengi wakawa na uwezo wa kukimiliki, labda tu kwa kuwa sasa kiliweza kupatikana kwa urahisi, si kama miaka ile ya mwanzo mwanzo, maana sasa wale jamaa wanao fanana sana wenye majina ya ajabu ajabu yasioweza hata kutamkika vyema, walianza kuvitengeneza kwa wingi sana na kuviuza kwa kina sie tusio na uwezo mkubwa.

Runinga za bei rahisi zikamiminika toka nchi alozaliwa Mwenyekiti Mao, zikaenea madukani, wengi tukazipata kwa mikopo na kulipa polepole, mradi tu nasisi tuwe nazo, hatukujali kama ni za rangi hiwe nyeusi au nyeupe, wenyewe wataalamu wakiita kaladi au bleki endi waiti, sisi tulizichukuwa na kuziweka majumbani mwetu.

Hakika majumba mengi ya kina siye yalijaa furaha siku ambayo kifaa hiki kilipo ingia majumbani mwetu. Kikawa ndio kibla kipya cha watu wengi, watoto walikoga vizuri na kuvaa nguo safi, wale ambao awakupenda kutumwa waliwauliza wazazi au walezi wao kama kuna chochote wanataka kuwatuma gengeni au dukani basi wawatume kabisa ili wasikose au kupitwa na vipindi vya kwenye Runinga.

Wengi wetu tulio bahatika kuwa na Runinga japo ya ukubwa wa inchi 15, hatukuwa tena na muda wa kuwatembelea majirani au ndugu au jamaa zetu. Tufate nini tena ilihali nasi tunamiliki Runinga?

Kidogo kidogo, tukaanza kujitenga na jamaa zetu, rafiki zetu, na hata ndugu zetu, maana kila mmoja alikuwa akitoka kazini anarudi nyumbani na kukaa na familia yake na hata siku za mapumziko tulikuwa bize kwenye Runinga.

Nani atoke kwenda kwa jirani au ndugu yake au jamaa yake kisha hakose vipindi avipendavyo na haswa zile tamsilia zenye kuendelea zisizo na mwisho...

Maisha yaliendelea, Runinga ikishindana na Radio na haswa pale Radio zilipoanza kutumia frikyuensi (Fri - Kyu - ensi) za EfuEm, maana kukazaliwa vituo vya Radio bila kujali uzazi wa mpango, vituo vikazaliwa vingi kama vile panya pori. Kila kona na kila mkoa kulikuwa na Radio za EfuEmu kadhaa wa kadha.

Wakati huo huo kukaanza kuenea kwa kifaa kipya kiitwacho simu ya mkononi, yaani Rununu, wakati kinaanza kuingia ni watu wachache mno ndio walikimiliki na haswa wafanyibiashara wakubwa wakubwa na wale wa kati na kati.

Wengi wetu tuliojifanya tunazo, tulibakia kukibeba tu na kila tukitaka kupiga, tulichokuwa tukifanya ni kubipu na kusubiri aliyebipiwa kupiga. Na kama unao uwezo kidogo wa muda wa maongezi kwenye simu yako ya analojia, basi utapiga na kuongea sekunde zisizo zidi kumi na kisha unaangalia salio. Wapo wale kina sie ambao tulipenda kubipu na kisha kuangalia salio maana unaweza kukukuta kasi ya aliyebipiwa ni kubwa kwenye kupokea kuliko ya aliyebipu.

Mara chombo hiki kiitwacho simu ya mkononi (Rununu) au Kilongalonga, kikabadilika ghafla bin vuu, badala ya kuwa analogi kikawa digitali, hapo sasa ndio balaa likaanza kidogo kidogo.

Hapo ndio Wabongo tulipoanza kuonyesha kuwa sisi tunajuwa kukitumia kifaa hiki, tulihakikisha kuwa hata kama hatuna ugomvi basi tutatafuta bifu na marafiki, ndugu na jamaa, na kutumiana meseji za matusi kedekede.

Tulikuwa na tabia ya kwenda studio au kuwatafuta wapiga picha kutufotoa picha za kumbukumbu, tena tukikaa kwa pozi hizi na zile. Wakati mwingine tukisubiri mpaka wiku ili kupata picha zetu.

Na wataalamu wa kifaa hiki walipo ona kuwa Wabongo ni mahodari sana kwenye matumizi ya hiki kifaa, wakakiboresha zaidi na kukitia akili, wenyewe wakakiita smatifoni. Hapo ndipo balaa kubwa likaanza kuenea kwenye jamii zetu zilizokuwa zikipendana na kutembeleana.

Maana baada ya ya Runinga kuingia kwenye majumba ya watu na kukata udugu na urafiki na ujamaa wa kutembeleana, smatifoni hii ndio hikaja kumalizia kabisaaa...!

Maana utake nini tena kwenye smatifoni, kwa sababu smatifoni huyu ana kila kitu, Radio EfuEm yumo ndani ya smatifoni, Luninga yumo ndani ya smatifoni, smatifoni kakusanya kila kitu.

Kawakusanya hata wale kina Fesibuku, Twita, Skaipu, yutyubu, vaiba na huyu mwingine wasapu na wengine wengi tunao wajuwa na tusio wajuwa, mpaka kamera katuwekea, ilihali ya kwamba amehakikisha hakubakisha kitu na kukupa sababu ya kufunga safari kwenda kumtembelea kama si mzazi wako au nduguo au jamaa yako.

Hakuna tena kutembeleana, maana kila kukicha tunashinda tukibofya bofya tu, mara Skaipu, mara wasapu, mara Fesibuku, Twita, au vaiba au klabu hausi.

Hata ile hamu iliyokuwepo kabla ya familia kukaa pamoja na kuangalia Runinga, imepotea kabisa, ukibahatika kuingia kwenye majumba ya ndugu zetu au marafiki zetu, wala si jambo la kushangaza kukuta kuanzia, baba mwenye nyumba, mama mwenye nyumba, watoto na hata mfanyakazi wao wa ndani na shamba boi, wote wanavilongalonga vya smatifone, na kila mmoja anabofya tu, mara uku mara kule.

Hakuna tena mwenye muda na Runinga, labda kuwe na tukio maalumu na hata hivyo unaweza kujikuta upo peke yako kwenye kushangalia Runinga, maana hii smatifoni tayari ina uwezo wa kurusha matangazo ya Runinga.

Ndipo hapo sasa tumeshajitenga si na jamii yetu tu bali hata na familia zetu humu majumbani, hatuna tena muda hata wa kufundisha watoto, maana hata mtoto wa miaka mitano akitaka kujuwa kitu, anabofya tu, gugo na anapata majibu elfu kidogo, yawe mazuri au mabaya atajuwa mwenye.

Picha zisizo na maadili ndio zimeenea kupitia kifaa hiki cha smatifoni, maana imefikia watu badala ya kuwasaidia waliopata ajali, ukimbilia kwanza kuwafotoa foto, ili uwe wa kwanza kurusha kwenye mitandao ya kijamii.

Hata wagonjwa waliopo ICU hawajasalimika, wamiliki wengi wa teknolojia hii ya smatifoni wamekuwa wambea kwa teknolojia hii na wanahabari wasio rasmi.

Mtu atajifanya kuja nyumbani kwako au kuja kumuona mgojwa, au kuja kwenye msiba, basi nafasi hiyo ya kipekee ya kusimama na kumuombea dua mgonjwa au maiti ndio atamfotoa foto na sekunde si nyingi, mara mgojwa wa watu kajaa duniani kote ana mipira kohoni, puani na waya za vifuani, au maiti ya nduguo si ajabu ukaikuta kwenye kuta za mitandao ya kijamii, tena usishangae kuikuta haina hata stara.

Maendeleo ni neema, lakini sisi Waafrika wa Afrika Mashariki, hatutumii hizi neema vyema, tena na wakati hatuutumii ipasavyo, baadhi yetu hivi sasa hatuwezi kustaamiri dakika, tusivute simu zetu, tupigiwe au tusipigiwe, kila mmoja kainamia anapangusa kioo cha simu kama mganga na bao la kupigia ramli.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!