Hivi karibuni, kwa makusudi, ilitumwa na kusambazwa Tangazo la UNESCO kuwa Uislamu ndiyo dini ya amani kuliko zote, na ikatolewa CERTIFICATE kama Utambuzi wa UNESCO kwa Uislamu.
Mtumaji wa ile Certificate yaliambatanisha na maelezo kwa makusudi ili aangalie kama kuna mtu yeyote atagundua lengo na madhumuni ya ujumbe ule, uwe ni kweli umetolewa na UNESCO au lah.
Kwa masikitiko makubwa hakuna aliyegutuka na badala yake, watu wengi wakishangilia na kujipongeza takriban 99.9%
INASIKITISHA!
Hii ndiyo hali tuliyofikishwa Waislamu duniani kwamba UKWELI na SIFA NZURI ni ule unaotoka kwa WASIOKUWA Waislamum au Taasisi zisizohusiana ndewe wala sikio na Uislamu!
Akili zetu zote zimeelekezwa NCHI ZA MAGHARIBI kuwa Jema ni lile wanalolisema WAO, na OVU ni lile wanaloamua WAO kuwa ni OVU. Na hivyo, wanapokuja kuamua kuwa jambo fulani la Uislamu SI HAKI, tunakuwa mstari wa mbele kupiga makelele na kufanya maandamano, ya amani au ya jazba na fujo, KUMBE TULIKWISHA WAKUBALI KUWA WAO NDIO WAAMUZI WA LIPI JEMA NA LIPI OVU!
Na KASUMBA hii imo hata katika mambo ya kidunia. Ufisadi ni ule unaotambuliwa na AMNESTY INTERNATIONAL tu. Hivyo, tunaekewa nchi gani ndiyo fisadi kuliko zote, na kuekewa points za ukubwa na uchache wa ufisadi wa nchi.
Nchi fisadi zote ziko kwenye nchi zinazoendelea, hata Uchina. Na nchi zisizokuwa na Ufisadi, zote ziko Magharibi. Na sisi huitikia AMEEN na kutumia maamuzi hayo juu ya nafsi zetu.
Vivyo hivyo, katika mambo mengine, yawe ya utawala bora demokrasia, uchaguzi nk.
Chochote kile ambacho hakijapata certificate ya "WAUNGWANA" wa Magharibi, au HAKIKUSIMAMIWA nao, hakiko sawa.
Sasa wanajaribu kujiingiza katika mambo ya Dini. Na sisi tunashangilia na kuwapa kibali kuwa wawe waamuzi wa Dini zetu, na hasa Uislamu!
Tusije kulia na kupiga kelele na kuandamana mabarabarani watapokuja kutoa certificate kwamba Uislamu ndio dini kandamizi zaidi kuliko zote kuhusu ndoa za jinsia moja!
Maana kitachowazuia kufanya hivyo ni nini, ikiwa mmesha wakubali kuwa WAO ndio Waamuzi wa Jema na Ovu, Haki na Dhuluma, Uhuru na Utumwa, nk.
Uislamu hauhitaji certificate ya UNESCO wala UN wala EU kuthibitisha kuwa ni Dini ya Amani kuliko zote.
Na tukiwa wajinga tukikubali uamuzi wao huo; maana tutakuwa tunawaambia mnaweza kutuamulia mambo mengine vile vile kwakutupa certificate kama ni haki au dhuluma.
Hilo ndilo wanalolilenga.
TUWE NA TAHADHARI.
Tusicheze ngoma tusiyoijua mwanzo wake wala mwisho wake!
Tusishangilie Wimbo tusioujua maana yake!
Turudi kwenye Kitabu chetu, kisicho na shaka yoyote, wala batili, si ndani yake, wala si nje yake kwenye Sunna za Mtume wetu ﷺ.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?