Friday, 7 October 2016

Alikuwa ni mdudu chungu aliyekuwa kwenye shughuli zake. Ghafla akaliona Jeshi kubwa la nabii Suleyman linakuja.

Ilimbidi aachane na kazi zake ili afanye kazi ya kutoa Tangazo kwa wadudu chungu wengine waingie mashimoni mwao ili wasije kukanyagwa na Jeshi la Nabii Suleyman na wote wakafanikiwa kuingia mashimoni.

Kama mdudu chungu huyu angesema aendelee na kazi zake hali ya kuwa jeshi ameshaliona, basi yeye angekanyagwa na wengine wangekanyagwa pia. Na kama angesema akimbie peke yake, yeye angepona ila wenzake wangekanyagwa na angeishi maisha ya upweke bila wenzake, maisha yake yote na angekufa kwa upweke wa sononi kwa kuwakosa wenzake.

Mdudu chungu yule, mbali na yeye kuendelea kuishi, pia alisababisha wengine pia waishi.

Wenye nia ya dhati ya kuwaokoa wanao angamia huku wakiwa hawajaui kinacho waangamiza, huwa wanaacha yao na kushughulikia hao wanaoangamia. Mwisho wa siku wanapona wao na pia husababisha wengine wapone.

Haiwezekani yao yanyooke yetu yapo mashakani, halafu waseme wapo kwa ajili yetu. 

Wafuatiliaji wa mambo wamenielewa...!

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!