Sunday, 13 November 2016

Alipomuoa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi yake, watu walisema inakuwaje kijana kama yule anaenda kumuoa mwanamke mkubwa namna hiyo kwani wadogo hakuna?

Alipoenda kumuoa mwanamke mwenye umri mdogo zaidi yake pia wakasema inakuwaje anaenda kumuoa mwanamke mdogo kama yule kwani wa saizi yake hakuna?

Pia alipooa wale wa saizi yake ambapo wengi walikuwa ni wajane, wakasema inakuwaje aoe wajane kwani wa kawaida hakuna?

Maneno yote waliyoyasema watu juu ya kuoa mwenye umri mkubwa, kumuoa mwenye umri mdogo, na hata kuwaoa hao wajane yalizimika baada ya kuona mfumo mzuri wa maisha ambao Mtume Muhammad (Rahma na amani ziwe juu yake) alivyoishi na wake zake hao.

Ulikuwa ni mfumo ambao kila mmoja alitamani aishi na mkewe. Watu walimzonga ili awafunze jinsi ya kuishi na wake zao katika ndoa na wanawake nao waliwazonga wake zake hao ili wapate mawili matatu ya jinsi ya kuishi na waume zao katika ndoa.

Kwa ufupi tunaweza sema "Yalikuwa ni maisha bora ya ndoa ambayo ulimwengu haujawahi shuhudia."

Maisha Yaliyotawaliwa na amani, upendo, furaha, uvumilivu, huruma, heshima na mazuri mengi (Hapa siyataji).

My Dears, yoyote utakaye ingia nae kwenye ndoa watu watasema. Wapo watakao zungumzia umri, watakao zungumzia rangi, watakao zungumzia kipato, watakao zungumzia elimu, watakao zungumzia kabila na vingine vingi. (Hapa sivitaji).

Ila kitakacho wanyamazisha midomo yao ni mfumo wenu wa maisha mtakaoishi ndani ya ndoa hiyo.

Inabidi mtafute mfumo utakaowafanya watu wawe na hamu ya kuishi kama nyinyi na wapende kujifunza siri ya mafanikio yenu katika ndoa.

Vinginevyo maneno yataendelea kusemwa... Na kusemwa... Na kusemwa... Na kuseeeemwaaaa....

Mwisho wa siku yatawaingia akilini na kujikuta mnaiharibu ndoa yenu kwa maneno ya watu.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!