Saturday 31 December 2016

KALENDA IPI YA MATUMIZI YA KILA SIKU, TUNAYOIFUATA, MILADIA AU AL HIJRIA!?

Wengi wetu tumekuwa tukikumbushana kuhusiana na kusheherekea au kutojihusisha aidha na sikukuu au matukio ambayo si ya Kiislamu, kama vile Mwaka mpya n.k.

Waislamu tunakatazana kusheherekea Mwaka Mpya, ni kweli si jambo lililo jema kusheherekea kwa kuwa halipo kwenye sikukuu za Kiislamu.

Lakini bado kuna swali la kujiuliza, je vipi kuhusu kutumia kalenda hii ya mwaka ambao tunakatazwa tusiusheherekee, je inajuzu kutumia kalenda ya Miladia (Gregorian calendar) kwenye shughuli zetu za kila siku?

Je vipi kuhusiana na siku za Majuma au wiki, ambazo nazo majina yake hayana asili na imani za Kiislamu, kama vile tunavyotumia majina ya siku, kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili ambazo kwa wazungumzao Kiswahili kuna mchanganyiko ndani yake, vipi wale Waislamu ambao wanazungumza Lugha nyingine kama vile Kiingereza, je nao wanapaswa kutumia majina hayo hayo au badala yake?

Kwanini tunakuwa Waislamu MATUKIO, tunasubiri mpaka litokee jambo ndio TUNAKURUPUKA kutaka KULITATUA.. Tumekuwa watu wa mamamuzi ya Kimatukio badala ya kujipanga na kuwa na mpangilio wa kimaisha kulingana na Uislamu wetu!?

Hapa naomba mnielewe kitu kimoja, sina maan kuwa nahalalisha Waislamu washerekee Sikukuu au matukio yanayo endana na kalenda ya Miladia, lah hasha, bali tunapoipigania haki (kweli) basi tusichague la kulipigania au siku maalum, bali ndio uwe utamaduni wetu, kuanzia uko majumbani, kwenye madrasa zetu na hata shule zetu na kwenye shughuli zetu za kila siku.

Haya ya kusubiria litokee kisha ndio tutumiane kuwa ili sio au lile ndilo ilihali masiku ya kawaida hakuna anayekumbuka chochote linatutia katika wakati mgumu sana na haswa vijana wetu ambao ndio tunao wategemea katika harakati za kila siku na siku zijazo.

Tunaweza kujiuliza maswali machache tu... Kwanini Miladia na si Hijiria!?

- Kwanini tukiulizwa UMRI tunataja kulingana na kalenda ya Miladia na si Hijiria!?
- Kwanini tukiulizwa TAREHE tunataja kulingana na kalenda ya Miladia na si Hijiria!?
- Kwanini tukiulizwa SIKU tunataja kulingana na kalenda ya Miladia na si Hijiria!?
- Kwanini tukiweka MIHADI tunapanga kulingana na kalenda ya Miladia na si Hijiria!?

Wapi tulipo potelea, wapi tulipo simamia na wapi tunapo elekea, kwanini tusijizoeshe kwa kile kilicho chetu?

TUJIPANGE la Sivyo Tusilalamike TUTAKAPOPANGWA na Hayo MATUKIO, Yanayopangwa na Hao Wenye KUYAPANGA.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!