Thursday, 1 June 2017


 WINTER & SUMMER.

Nchi nyingi za Ulaya haswa ulaya ya Magharibi (Western Countries), majira yao ya nyakati yanatofautiana kulingana na vipindi vinne vya majira. Ambavyo ni Summer Kiangazi (Majira ya Joto), Autumn majira ya kupukutika kwa majini, Winter majira ya baridi na
Spring majira ya kuchipua kwa majani.

Masaa ya ufungaji wa Mwenzi wa Ramadhani, yanategemea na majira yalioko wakati husika. Vipindi viwili muhimu ambavyo uangaliwa sana ni wakati wa kipindi cha Baridi (Winter) na Kipindi cha majira ya joto (Summer).

Vipindi viwili hivi vinatofautiana sana kwenye muda wa kufunga na kufungua Swaumu.

Wakati wa majira ya joto (Summer), Waislamu wanafunga Ramadhani kwa kipindi kirefu sana, kuanzia saa 16 mpaka saa zisizo pungua 22 kwa baadhi ya nchi kila siku.

Naa kwa kipindi cha majira ya Baridi (Winter) saa za kufunga zinakuwa chache mno, kuna nchi wanafunga saa zisizo zidi 4 kwa siku na kuna nchi ufunga hadi masaa 7 tu.

Jambo ambalo linawakwaza wenyeji asilia wa nchi hizo ambao si Waislamu na haswa kipindi cha majira ya joto ni kuona Waislamu wakifunga kwa muda mrefu sana, wao uona ni kijitesa kwa Muislamu kufunga muda wote huo.

Wengi wao wanacho kiangalia haswa ni tamaa ya nafsi na kuona kuwa ni vigumu kwa mtu kukaa muda mrefu bila kula ni kujitesa tu. Wengi wao uangalia tu juu ya umbo la Mwanadamu, kuwa anatakiwa kula na kunywa na hakuna sababu ya kujizuiya na ajabu zaidi uona pale Muislamu anapojizuiya mchana wa Ramadhani kufanya tendo la jimai.

Wanasahau kuishughulisha akili yao kuangalia faida waipatao wafungaji Kiroho na Kimwili.

Watu wengi wafatiliao mambo ya afya haswa madaktari wa afya ya mwili, wanakubaliana kuwa kufunga kwa masiku kadhaa, kuna faida nyingi kimwili na haswa kwenye maswala ya afya ya mwili na hata Kiroho.

Vilevile kwa nchi zenye masaa mengi ya mchana kipindi cha joto (Summer) kuna hikma yake, na wakati wa majira ya Baridi (Winter) kipindi ambacho mchana uwa mfupi pia kuna hikma yake.

Kwa kuangalia hitajio la Binadamu la kuhitaji nishati ndani ya mwili wake, hapa tunazungumzia yale mafuta yaliohifadhiwa mwilini kwa maana ya Lehemu (cholesterol), Lehemu usaidia mambo mengi sana mwilini na kwa kipindi cha baridi ndio hitajio lake uwa kubwa sana kwenye mwili wa binadamu kwa sababu ndipo Lehemu hutumika kwa faida nyingi mwilini.

Na ndio utaona nchi za Ulaya na Amerika muda wao wa kufunga kipindi cha Baridi (Winter) huwa kifupi sana na hii upelekea faida kwenye mwili kwa kuzuiya matumizi makubwa ya Lehemu mwilini kwa sababu mtu anapofunga, mwili ujirekebisha na kutumia Lehemu kurutubisha mwili.

Na kwa kipindi cha joto, Lehemu inatakiwa isihifadhiwe sana mwilini na ndipo mtu anapofunga basi ile Lehemu utumika kurutubisha mwili na mwili unajikuta kuwa haiweki hakiba nyingi ya Lehemu, sababu yake itumika sana itapelekea mwili kuwa na joto na nishati nyingi ambazo zinaweza kumpelekea mtu kupata matatizo ya kiafya.
Ndio ukaona kipindi cha majira ya Joto Mwezi wa ramadhani unakuwa ni mrefu sana na kwa nchi za Ulaya funga umalizika baada ya masaa yasiopungua 16 mpaka saa 20 za kufunga na ile Lehemu iliyokusanywa mwilini takribani mwaka mzima ndipo hapo inapotumika kwa wingi. 

Na kwa kipindi cha majira ya Baridi (Winter) saa za kufunga ni chache sana Kuanzia Masaa 3 Mpaka saba tu, kulingana na mazingira ya nchi kijiografia na hapa ndipo Lehemu hutumika kidogo kwa sababu hitajio lake mwilini ni kubwa.

Na ndio MenyeziMungu anatuambia kwenye Qur'an
...Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

Qur'an Sura Al- Baqara (2):184

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!