Sunday, 10 December 2017

WAHALIFU WANAPO PONGEZWA.
Tunasahau Uhalifu Walioutenda
Waombe Radhi na Kuwataka Msamaha Waanga wa Ubakaji Ule.

Nilikuwa nimekaa mbele ya luninga, nikiangalia kipindi cha maadhimisho ya shere za uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba 2017.

Katika moja ya matukio kadhaa yaliojiri siku hii ni pamoja na tamko rasmi la rais wa Tanzania la kusamehe waarifu mbalimbali wasio pungua 1,821 walioko vifungoni kwenye kuta za magereza ya Tanzania na wengine 8157 wamepunguziwa adhabu.

Katika moja la tamko ambalo baadae lilihamsha msisimko kwa baadhi ya wasikilizaji ni lile la kuachiwa kwa Mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

Kesi hya Nguza Viking na wanae iliwashtua watu wengi na haswa mashabiki wa mwanamuziki huyo anayepiga muziki wa nyimbo za Rhumba.

Wanamuziki hao waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya kuwabaka na kuwanajisi watoto.

Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni mjini Dar es Salaam.

Wanamuziki hao wamekaa jela tangu walipohukumiwa adhabu hiyo Juni 5, 2004.

Nakumbuka mwaka 2010 walikata rufaa na rufaa yao kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na baada ya kupitiwa tena, hukumu ile ikapelekea watoto wake wawili Nguza Mashine na Francis Nguza kuachiwa huru kwa kuonekana kuwa hawana makosa.

Lakini yeye Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Washtakiwa hawa hawakukata tamaa, Tarehe 30 Oktoba 2017, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.

Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, imeendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.

Na Majaji walithibitisha kwa kusema kuwa waarifu hao wawili wa ubakaji wa watoto wa shule ya msingi matukio yaliofanyika mwaka 2003 kuwa wana hatia na wanastahiri adhabu waliyokuwa wanaitumikia.

Rais ametoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali wakati akihutubia maadhimisho ya shehere za Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Dodoma.

Nimekaa nikajiuliza maswali kadhaa wa kadha kuhusiana na kadhia nzima ya tukio ili la kuachiwa huru kwa waarifu hawa.

Nikamkumbuka jirani yangu mmoja pale Sinza Palestina, ambaye mtoto wake alikuwa ni mmoja wa waanga wa ubakaji ule.

Hivi leo atakaposikia kuwa Babu Seya na mtoto wake wamesamehewa atajisikiaje?

Je ni nini hatima ya wale watoto waliobakwa?

Je familia za waanga nao waliombwa msamaha kiasi wakaridhia kuwa wabakaji wale wasamehewe?

Watoto waliobakwa wataendelea kuwa na kumbukumbu na vidonda visivyo pona ndani ya nafsi zao kwa maisha yao yote mpaka wanaingia makaburini.

Hakuna ambaye anaweza kuwalipia kwa vitendo walivyofanyiwa na familia ya Nguza.

Sitaki nieleweke vibaya kuwa labda napingana na amri ya Rais ya kuwasamehe wafungwa kadhaa, lakini ili la kuwasamehe wafungwa wa ubakaji na mauwaji, ni tofauti na msamaha wa uharifu mwingine kama wa wizi wa mali za umma na binafsi.

Mfungwa wa ubakaji aliyehukumiwa kifungo cha maisha anaporudi uraiyani, je atakwenda kuwaomba msamaha waanga wa vitendo vyake?

Rais kawasamehe kwa kutumia uwezo aliopewa na katiba ya nchi ya kusamehe mfungwa yoyote yule alnayekidhi vigezo vya kusamehewa.

Basi kwa kusamehewa uko kwa Mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ nao waonyeshe uungwana kwa kuwaomba radhi wale watoto na familia zao kwa vitendo walivyo wafanyia.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!